......Dada anapolazimika kuolewa ili kaka asome!!!!!!!!!

......Dada anapolazimika kuolewa ili kaka asome!!!!!!!!!

Kuna jambo moja labda nadhani unashindwa kulielewa, mjadala unapowekwa mezani jaribu kutanua mawazo na kufikiria nje ya boksi.
Mimi binafsi na wengineo waliojaribu kuibua hiyo hoja hawakujilenga wenyewe, bali walijaribu kuakisi vile baadhi ya wazee wenye maisha duni walivyo na mawazo ya namna hiyo.

Wapo wazee kabisa husema, "Kwa kuwa mimi nimeshindwa maisha na kuishia kwenye ufukara, basi nitalizaa watoto wengi kwani Mungu si Mzee Mkumba atanijaalia heri kupitia wao na si haba kuwa mwanangu mmoja atajakuwa mbunge".

Mwisho wa siku wingi wa watoto unakuwa kadhia, na kama ujuavyo wa mbili huwa havai moja...watoto wote pamoja na yeye hudidimia pamoja katika lindi la ufukara.

watu8 bwana, sasa kwa hiyo wote tutanulie box upande unaofikiria wewe tu? Kama ni mjadala, angalia upande unaouona nami niangalie upande mwingine then tulete kilichopo. Jamani, si upande mmoja wa dunia ukiwa mchana mwingine utakuwa usiku? Au?

Pamoja na niliyoyasema, sibishii ulichokisema kwa sababu una-share nawe ulichowahi kusikia au kuona. On the same note, mimi nilichosikia mara nyingi nilikokulia, ni sisi walimwengu tukiwanyooshea vidole wazee wenye watoto wao waliokuwa mijini na kusema....Yule mzee usimuone vile, ana watoto tisa wote wako mjini, lakini hakuna hata mmoja anayemkumbuka hata sukari.....Mzee wa watu mwenyewe kimyaa....
 
Nakubaliana nawe kwenye mchango wako, though ninatofautiana nawe kidogo kwenye sentensi yako funguzi.

Kila binadamu anayehitaji usaidizi/msaada na asaidiwe, ila nina uhakika nikiwa na shilingi 100 sitaigawa paripassu kwa 'binadamu' wote waliochanganyika kwenye kundi moja na wazazi wangu.....

Hilo ni kosa kubwa!
Na kama ni hivyo unawashangaaje wale wanaowaprioritize wazazi kuliko binadamu mwingine?
 
I think Eiyer is a Simba SC follower...ulipoweka yale maandishi kwa Yellow he went aaaarrgghhh @#!%...but when you turned em Red...now he's happy again

#JustKidding
Teh,teh,teh,teh,teh,teh,teh,teh!!!
Mkuu sio hivyo bana!!!!!!!
Nina kadi ya Yanga

Ila kiukweli nilipata shida kukisoma alichoandika Blaine !!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Good story,...Siku hizi naona waja kivinginevingine,story za mafundisho zaidi

Kwani nilikuwaje?
Halafu hii sio story ni kweli kabisa[kama ulikuwa unamaanisha nimetunga]
 
Hivi hakunaga mwanzo mbaya na mwisho mbaya
Hii ipo kwa kiwango kidogo sana
Kwa sababu binadamu wa aina hiyo ni mpu.mbavu kupitiliza
Nasema hayo kwa sababu ni vigumu sana kumpata binadamu asiejifunza kabisa
Binadamu wa kawaida tu anaweza kujifunza kwenye kushindwa na kufikia kuweza japokuwa sinawezekana isiwe kwa viwango alivyovitaka

Ni sawa na uniambie kuna mtu ambae hajawahi kupata raha au mafanikio kwenye shughuli zake hata kidogo tu!
au mwanzo mzuri na wisho mzuri?
Hili nalo linaweza kuwa lipo lakini linafanana na hilo la kwanza nililoelezea hapo juu!!!!!!!
 
Hilo ni kosa kubwa!
Na kama ni hivyo unawashangaaje wale wanaowaprioritize wazazi kuliko binadamu mwingine?

Aisee.....Kwangu ni pata kubwa....Unaanzaje kutoka ndani ukamnunulie uniform mtoto wa jirani wakati wa kwako wanatembea 'ma------' nje?
 
Aisee.....Kwangu ni pata kubwa....Unaanzaje kutoka ndani ukamnunulie uniform mtoto wa jirani wakati wa kwako wanatembea 'ma------' nje?

Ngoja nikuambie kitu Dina
Hebu fikiria kaja kwako mtu asie na chakula ukamnyima,je ni dhambi?
Na kama ni dhambi inatofauti na dhambi ya kumnyima mwanao chakula?
Kama hazitofautiani ni kwanini?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom