Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,920
................Maisha yana mambo yake lakini binadamu nao pia tuna yetu
Huyu dada alizaliwa kwenye familia ya kimaskini kama kawaida yetu Waafrika wengi hasa wanaoishi maeneo ya vijijini,Ni mtoto wa 3 kwenye familia ya watoto 5
Mahali na jina la mhusika sitalitaja kwa sababu malum!
Yeye na kaka yake walikuwa wanasoma shue moja lakini kaka yake alikuwa yuko mbele yake kwa darasa moja,kaka yake alipohitimu elimu hiyo ya msingi,dada huyu alikuwa yupo darasa la 6
Kaka yake huyo hakuwa ni mhudhuriaji mzuri sana wa shule hivyo hata mtihani wa kumaliza elimu ya msingi nao aliufanya nusunusu na hakufaulu,baada ya kushindwa kufaulu wazazi wake waliamua kumtafutia shule ili asome lakini kikwazo kilikuwa ni uchumi wao kuwa mbovu
Ndipo waliposhauriana kuwa ule ulikuwa ni wakati muafaka wa mtoto wao wa kike aolewe ili wapate mahari itakayowawezesha kulipia gharama za mtoto wao wa kiume kusoma elimu ya sekondary
Ilikuwa ni siku ya jumanne alipotoka shule ndipo alipoitwa na kupewa taarifa ile,aliambiwa kuwa inabidi aache shule na aolewe na mchumba ameshatafutiwa ili mahari itumike kumsomesha kaka yake,binti alijaribu kupinga hilo lakini aliambiwa kuwa yeye ni mtoto wa kike hata elimu hiyo aliopata inamtosha anachotakiwa ni kuolewa ili akaanzishe familia
Dada huyu alilia sana siku hiyo kwani alikuwa anapenda shule na hakutaka aachishwe lakini hakuwa na lakufanya ilibidi tu aolewe
Dada wa watu aliolewa na maisha ya ndoa yakaanza,kaka yake alitafutiwa shule na kuanza masomo,lakini kama ilivyokuwa shule ya msingi,hakuwa mhudhuriaji mzuri wa shule na mara kwa mara alikuwa akisimamishwa shule kwa utovu wa nidhamu
Kaka yake huyu aliendelea na shule hiyo na hatimae alikuja kufukuzwa shule kwa kosa la kukutwa akivuta Bangi,na shule iliishia hapo
Kijana huyu aliamua kuondoka nyumbani nakwenda mjini, na alienda kuwa kijana wa vijiweni bila kuwa na shughuli ya kufanya na mara nyingi alikuwa akikumbana na mikono ya dola kwani alijihusisha na vibaka
Kutokana na kutokuwa na malezi mazuri,maisha ya kijana huyo yalikuja kukatishwa na kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kwa tabia yake ya wizi
Dada yake kutokana na kuolewa bila ridhaa yake maisha yake ya ndoa hayakuwa mazuri na mume aliemuoa alikuwa ni mlevi sana,maisha ya dada huyu hayakuwa ya furaha hata kidogo
Mumewe hakuwa hata akimpa matumizi ya kutosha na nyakati za masika yeye ndie alikuwa mkulima huku mumewe akiwa ni mtu wa kwenda kulewa tu na mavuno yalipokuwa yakipatikana mumewe alikuwa akiyauza na mkewe hakutakiwa kuuliza fedha zilipokuwa zinaenda
Dada huyu hayakuwa mazuri na mara nyingi alikuwa akikutana na kipigo kila mumewe akirudi nyumbani nyakati za usiku akiwa amelewa,alipokuwa akiwaambia wazazi wake hawakujali na walikuwa wakimuambia kuwa maisha ya ndoa ndivyo yalivyo
Dada huyu alikuwa kila akipata ujauzito na ulikuwa unaharibika na kutoka kila alipokuwa akipigwa na mumewe kitendo kilichozidisha hasira kwa mumewe na kumuambia ni hasara kwa kutozaa
Maisha yalikuwa magumu sana na ilifikia wakati hakuwa anakula na alikuwa anakoroga uji na kuutumia kama chakula
Dada huyu aliamua kutoroka kwa mumewe na kwenda kwa shangazi yake ambae alikuwa ndie angalau alipokuwa akimueleza matatizo yake alikuwa anamsikiliza,alipofika kwa shangazi yake alipokelewa na akaeleza nia yake ya kutokurudi kwa mumewe,shangazi yake alionekana kutokukubaliana naye lakini dada huyu ilibidi amuambie kuwa atakaa pale kwa muda kisha atarudi kwa mumewe
Maisha yalianza na ilipita miezi miwili na huyu dada aliondoka kwa shangazi yake akimuaga kuwa anarudi kwa mumewe,lakini haikuwa hivyo,dada huyu aliondoka na kwenda nyumbani kwa rafiki yake ambae walisoma wote shule ya msingi ambae alifanikiwa kukutana nae wakati akiwa kwa shangazi yake
Alipofika kwa rafiki yake huyo ambae wakati huo alikuwa yupo kidato cha 5 ilibidi atambulishwe kwa wazazi wake na rafiki yake na kuwaeleza aina ya matatizo yaliyomfanya aombe hifadhi pale
Wazazi wa rifiki yake waliahidi kumsaidia lakini wakamwambia kuwa ni lazima waitaarifu serikali ya mahali walipokuwa wanaishi pamoja na wazazi wake,dada huyu alipinga suala la wazazi wake kupewa taarifa kwa kujua kuwa atarudishwa kwa mume wake lakini wazazi wa rafiki yake walimuondoa wasiwasi kwa kumuambia kuwa kama aliyowaambia ni kweli basi hawataweza kumsumbua kwakuwa wakifanya hivyo watalifikisha suala hilo kwenye mikono ya sheria na atakuwa salama
Na kama dada huyu alivyotabiri baada ya taarifa kuwafikia wazazi wake walitaka arudi kwa mumewe lakini walipoambiwa kuwa watashtakiwa waliogopa na kumlaani mtoto wao huyo kwa kumuambia kuanzia siku ile sio mtoto wao tena
Binti hakujali
Wazazzi wa rafiki yake walimuuliza alichokuwa anataka akawaambia kuwa bado anahitaji kusoma
Sitaki kuwachosha sana kuhusiana na kilichoendelea lakini kwa ufupi binti alifanikiwa kusoma na alipata mume mwema na sasa anafanya kazi kwenye shirika moja la kigeni
Ugomvi na wazazi wake uliisha kwani binti ilibidi atafute ndugu na kusuluhisha ugomvi huo na amewatoa wazazi wake kule walikokuwa wanaishi na kuwapa nyumba aliyoijenga yeye mwenyewe na amewaanzishia biashara ambayo walisema wanaimudu
Amewapeleka shule wadogo zake na mmoja anamalizia masomo yake kwenye chuo kimoja hapa nchini na ndie alienipa ushuhuda huu
Kwa kifupi dada huyu amefanikiwa kuyabadili maisha ya nyumbani kwao pamoja na kunyimwa nafasi ya kufanya hivyo!
Haya ndio maisha yetu!!!!!!!!
Inasikitisha sana!!!!!