......Dada anapolazimika kuolewa ili kaka asome!!!!!!!!!

......Dada anapolazimika kuolewa ili kaka asome!!!!!!!!!

bora huyo dada mwisho wake umekuwa mzuri maana unaweza pitia shida zote hizo na ukafa nazo.
 
Siamini kama mtu anazaa mtoto ali aje kusaidiwa naye. Ila litakuwa jambo la kichekesho kama mtoto umeneemeka na wazazi wako hali tete na wewe usiwiwe kuwasaidia...

Kumsaidia mzazi ni sawa na unapomsaidia binadamu mwingine yoyote

Kuna watu wanazaa ili waje wasaidiwe na watoto wao baadae
Nadhani umeshasikia zile kauli "huna hata mtoto ukizeeka utaishije"?
Hizi ni kauli zinazolsababisha mtu kutowajibika kwenye ujana wake
Na matokeo yake mtoto wa kiume akioa mama anaanza kupata wivu
Anakuwa anawaza vile vitenge alivyokuwa ananunuliwa sasa vitapungua na kwenda kwa mke
Hii ni aina mbaya sana ya kufikiri!
 
sina maana familia zooteee laa, nina maanisha baadhi ya familia tu. Mjombangu mwenyewe ni mfano tosha wa hili.

Haya bhana!
Mi nilitaka uelewe tu, kama familia chache ndio hutokea hayo uliyosema!!!!
 
Hivi mtu anazaa mtoto ili aje amsaidie?

Mkuu, hapa namaanisha kwa "case" kama ya hapo juu...msaada niusemao ni ule wa lazima. Let say, nyumba ya wazazi imesombwa na mafuriko na mtoto/watoto wa wazazi hao wanao uwezo wa kuwasaidia lakini wapi!!! huu ndo msaada niusemao....

Mzazi kumtunza mtoto ni lazima lakini, silazima kwa mtoto kumtunza mzazi....
 
....
Na kama dada huyu alivyotabiri baada ya taarifa kuwafikia wazazi wake walitaka arudi kwa mumewe lakini walipoambiwa kuwa watashtakiwa waliogopa na kumlaani mtoto wao huyo kwa kumuambia kuanzia siku ile sio mtoto wao tena laana based on wrong/unjust principle haina effect. i like how binti alijikaza 'kisabuni' na kuendelea na nia yake ya kusoma. righteousness will prevail :smile:

Binti hakujali

.....

Ugomvi na wazazi wake uliisha kwani binti ilibidi atafute ndugu na kusuluhisha ugomvi huo na amewatoa wazazi wake kule walikokuwa wanaishi na kuwapa nyumba aliyoijenga yeye mwenyewe na amewaanzishia biashara ambayo walisema wanaimudu
Amewapeleka shule wadogo zake na mmoja anamalizia masomo yake kwenye chuo kimoja hapa nchini na ndie alienipa ushuhuda huu

Kwa kifupi dada huyu amefanikiwa kuyabadili maisha ya nyumbani kwao pamoja na kunyimwa nafasi ya kufanya hivyo! nimefurahi binti hakuweka kinyongo na kuwasaidia afterwards. upendo > all

Haya ndio maisha yetu!!!!!!!!
Inasikitisha sana!!!!!
rreedd
 
Good story,...Siku hizi naona waja kivinginevingine,story za mafundisho zaidi
 
Kumsaidia mzazi ni sawa na unapomsaidia binadamu mwingine yoyote

Kuna watu wanazaa ili waje wasaidiwe na watoto wao baadae
Nadhani umeshasikia zile kauli "huna hata mtoto ukizeeka utaishije"?
Hizi ni kauli zinazolsababisha mtu kutowajibika kwenye ujana wake
Na matokeo yake mtoto wa kiume akioa mama anaanza kupata wivu
Anakuwa anawaza vile vitenge alivyokuwa ananunuliwa sasa vitapungua na kwenda kwa mke
Hii ni aina mbaya sana ya kufikiri!

Nakubaliana nawe kwenye mchango wako, though ninatofautiana nawe kidogo kwenye sentensi yako funguzi.

Kila binadamu anayehitaji usaidizi/msaada na asaidiwe, ila nina uhakika nikiwa na shilingi 100 sitaigawa paripassu kwa 'binadamu' wote waliochanganyika kwenye kundi moja na wazazi wangu.....
 
Umezaliwa Tanzania kweli wewe? au maisha yako umekulia mijini tu?


Tanzania halisi, na mjini nilifuata sukari......Swali dogo tu, hivi kweli mtu anazaa mtoto ili kujiandaa na wasaidizi wa hapo baadaye? Kweli? Yaani uzazi wako ni kwa ajili ya kutafuta wasaidizi? watu8 mbona unaniangusha mkuu....Kwa hiyo kama mambo yako safi huhitaji watoto? Au nao unawatafuta ili waje kukuogesha ukizeeka na hujiwezi kuoga mwenyewe?
 
Hii stori imenikitisha sana na yote yaliyompata huyo dada ni kwa sababu ya patriarchy system ambayo wakati mwingine mtoto wa kike hulazimishwa kuolewa kwa nguvu ili familia ipate mali hata kama mume ni mzee.
 
Swali dogo tu, hivi kweli mtu anazaa mtoto ili kujiandaa na wasaidizi wa hapo baadaye? Kweli?
Yaani uzazi wako ni kwa ajili ya kutafuta wasaidizi? watu8 mbona unaniangusha mkuu....Kwa hiyo kama mambo yako safi huhitaji watoto? Au nao unawatafuta ili waje kukuogesha ukizeeka na hujiwezi kuoga mwenyewe?

Kuna jambo moja labda nadhani unashindwa kulielewa, mjadala unapowekwa mezani jaribu kutanua mawazo na kufikiria nje ya boksi.
Mimi binafsi na wengineo waliojaribu kuibua hiyo hoja hawakujilenga wenyewe, bali walijaribu kuakisi vile baadhi ya wazee wenye maisha duni walivyo na mawazo ya namna hiyo.

Wapo wazee kabisa husema, "Kwa kuwa mimi nimeshindwa maisha na kuishia kwenye ufukara, basi nitalizaa watoto wengi kwani Mungu si Mzee Mkumba atanijaalia heri kupitia wao na si haba kuwa mwanangu mmoja atajakuwa mbunge".

Mwisho wa siku wingi wa watoto unakuwa kadhia, na kama ujuavyo wa mbili huwa havai moja...watoto wote pamoja na yeye hudidimia pamoja katika lindi la ufukara.
 
Back
Top Bottom