Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Profesa Anna Tibaijuka kiasi cha Tzs milioni 80

Kazi ipo walahi!!

Ulimi ni kiungo kidogo lakini balaa lake si la kitoto!
JamiiForums-829252439.jpg
 
MMa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, ilimuamuru Musiba kulipa Sh. milioni 80 kwa Prof. Tibaijuka baada ya kuridhika kwamba alikashfiwa na kudhalilishwa na mshitakiwa kupitia gazeti lake la Tanzanite. Nakala ya hukumu hiyo ilitolewa Julai 16, 2021
Mama anahasira sana na yule alitangulia mbele.
 
Huyu kijana Cyprian nilijua haya yatampata tu. Alipindukia mipaka ktk uanaharakati wake. Alidanganywa.
Kimsingi, alikuwa ktk lengo la kuingia kwenye system ya Serikali ili atoke kimaisha. Aligombea hadi ubunge, akapigwa chini. Alitakiwa kushtuka pale pale.
Anyway, mambo mengi aliyokuwa aliyasema ilikuwa ni kweli. Lakini, dunia na Nchi hii ni ya kuwa muwazi na mkweli kiasi hicho? Unawagusa "bigwheels", mfano wa mama Tibaijuka, Membe, mzee Makamba's family, mzee Kinana, JK's family, kuwataja wachache tu; Nilijua lilikuwa ni suala la muda tu. Hayawi hayawi ...
Niliwahi mshauri huyu kijana hata kupitia media zake. Bila shaka aliona na Alipuuzia. Sasa namshauri tena kama huwa anapita humu JF. Waingereza hunena, ... If you cannot fight them, join them. Nina hakika, waungwana niliowataja hapo juu ni waungwana kweli kweli. Ni wazee walioshiba hekima. Ni wasomi. Ni wazazi. Hawana njaa. Wanajua njaa ndiyo ilikuwa ikimsumbua Cyprian. Ni njaa tu. Unajua hapa duniani wapo watu wenye haiba anapotafuta kitu atatumia hata njia zisizofaa hata kama anawaumiza wenzake kama Cyprian alivyokuwa akifanya; potelea mbali! Ndivyo dunia ilivyo.
Sasa, namshauri atafute wazee wenye hekima, waende "kuwaangukia" wahanga wa matendo yake. Naamini watamsamehe. Akishupaza shingo, ... Oohoo! JPM hayupo tena duniani. Aige mfano wa Nape na January. Walipoona wamelikoroga, walienda kujisalimisha kwa "Jiwe". Aliwasamehe na maisha yaliendelea. Huo ndio ubinadamu ati.
Cyprian Musiba mdogo wangu kama siyo mwanangu, jishushe, Nenda ukatubu kwa wote uliowatendea ndivyo sivyo. Uliwajeruhi na kuwaumiza sana mioyo yao nasi tulishuhudia. Kumbuka ewala hushinda utumwa. Huwezi kushindana na "vingunge" hawa ukashinda. Wakumbuke wanao, kumbuka ndugu walio nyuma yako wanakutegemea wewe. Wakumbuke watumishi uliowaajiri kwenye media unazomiliki. Ukipotezwa itakuwa pigo kubwa.
Hata hivyo, nawashauri vijana walio na tabia au haiba ya Cyprian. Chungeni sana na kuwa makini na njia mnazotumia kupata maisha. Siyo kila njia ni nzuri na salama. Naamini Cyprian alikuwa akitumiwa na wanasiasa. Wanasiasa wa Tanzania ni wa kuwaangalia kwa makini kwa jicho la tatu. Jamaa mmoja alisema, ... Mwanasiasa wa TZ akikwambia, amka kumekucha ni saa 12:00 Asubuhi, kabla ya kuamka angalia saa yako kwanza. Ni hatari! Wanakutumia kisha wanakutelekeza. Ni wajasiriaSiasa!
Naamini umenielewa. Mwenyezi Mungu akusimamie ktk hili. Amen.
Teh teh teh teh...umenifurahisha sana hasa hapo ulipomtaka Musiba akawaangukie wazee.

2880792_IMG_20210613_182943_1.jpg


2975331_IMG-20141102-WA0010_1.jpg
 
Back
Top Bottom