Cyberbullying

Cyberbullying

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
9,296
Reaction score
7,688
Habari za saa hizi waungwana.

Tuanze na kama title ya uzi huu inavyowakilisha.Cyberbullying ni nini?Kama tunavyojua kuna wambea,wasengenyaji,wazushi na wanafiki kwenye kila jamii.

Cyberbullying ni uzushi wa kwenye internet kupitia kwenye mitandao.Uzushi huo unaweza kuwa wa aina tofauti,unaweza kuwa kama mtu anakufatilia maisha yako na kuzusha vitu visivyo na ukweli au hata vyenye ukweli lakini aongeze pilipili na chumvi ili apate attention.

Kwenye cyber bullying kuna victim na kuna bully.Bully/mzushi ni mtu ambaye kwa lugha ya rahisi anayependa "ATTENTION", au tumuite "ATTENTION SEEKER"mtu huyo anakuwa na character ya kutokujiamini,kuwa na low-self esteem na mpweke.

Anakuwa mpweke kiasi cha kwamba anaona njia pekee ya yeye kuonekana ni kuzusha vitu visivyo na ukweli.Ni mtu ambae muda wote anataka aonekane na yeye yumo anavuma na hajachacha.

Mtu huyo huyo hajali maslahi ya athari atazozipata victim,kwasababu kwake yeye akipata attention ni furaha,anaona furaha watu wakifanya masikhara.

Bully ni mtu ambae anakuwa anafikiri na kufatilia sana maisha ya wengine baadala ya kutumia muda wake kufikiri vitu vyenye maendeleo na manufaa kwenye maisha yake.Nimeshashuhudia kesi tofauti ambazo watu wamekuwa bullyed mpaka kupelekea kifo,ni kitu kinachosikitisha mno.

Wanasema njia pekee ya kuepuka kuwa bullyed ni kuwa na nguvu za kukabiliana na mzushi na kumueleza kuwa hutovumilia upuuzi wake tena.Lakini swali linakuja tutazuia vipi cyberbullying wakati hali hio inatokea kwenye mitando na kuna uwezekano mkubwa humfahamu muhusika.Naelewa kuna wahanga wengi walopitia cyberbullying au hata bullying katika jamii tunazoishi.

Je mlichukua hatua gani hali hiyo ilipowakuta?Kuna kitu ambacho ulikifanya ungekifanya tofauti?Unadhani ni jukumu la nani kuhakikisha hali hio haitokei tena?Wahusika wa mitandao?Je kama umewajulisha kuhusu hali hio na hawakuchukua hatua zozote utakuwa na imani nao na mtandao wanaowakilisha?

Karibuni mtoe michango yenu.
Gorgeousmimi
 
Kuna wengine wana stress za maisha, unawaonea huruma unawasamehe tuu..
Huko mitaani maisha yashawapiga vibao basi wanahaha kusaka umaarufu wa kwenye mitandao....

Mara nyingi huwa ni watu ambao jamii haiwapi attention either ni wabaya kwa muonekano au wanatabia mbaya nk...so huwa hawajiamini hivyo likes za kwenye mitandao ndo zinawafariji.

Dawa yao ni kuwadharau kama walivyodharauliwa huko walikotoka, ukiwafuatilia ndo unakuwa umewapa attention wanayotaka....!
 
Perspicacious!
 
Hakuna cyber bullying Tz. Mtu anaekua bullied online can always pull him/herself out. Kama ni picha za utupu kuachiwa online they shouldn't have taken them in the first place. Mambo mengine ni utoto na skendo zingine za kijinga ambazo wanaoanzisha na victims wote wanataka attention.

Punguzeni uzungu tuna matatizo mengi ya kushughulikia kabla ya kudiscuss cyber bullying. Tena, sijaona na hakuna cyber bullying Tz so far
 
Kweli hakuna kitu kama hicho tanzania.
 
Kama yule mwanaharamu daktari wa IMTU, aliyenisambazia picha zangu za utupu, kwa kweli kila nikifikiria nakosa la kufanya.
Yote namuachia Mungu....ila ipo siku.
 
Kuna thread kama mbili hivi zimeanshwa hapa..si nzuri kabisa..i can't say more lkn humu kwenye mitandao kuna watu washamba sana..

Umeongea ukweli, kuna thread kama mbili nilizisoma umu niliishia kusoma nakuchoka tu. Yani mmetofautiana na mtu kitaa alafu unakuja kumwanzishia mada ni zaidi ya ushamba ila ni unyama.

Mimi siku moja namzingua member mmoja umu kimasihara tu nashangaa eh pm zina miminika napewa big up napewa mpaka taarifa nisizoomba kwa kweli nilishtuka nikaona kumbe kuna mambo sio kama tunavyoyachukulia wengine unaweza kucheza muzki usioujua.
 
Kama yule mwanaharamu daktari wa IMTU, aliyenisambazia picha zangu za utupu, kwa kweli kila nikifikiria nakosa la kufanya.
Yote namuachia Mungu....ila ipo siku.

Aaah,kweli madam B???usimwachie kirahis ivo
 
Umeongea ukweli, kuna thread kama mbili nilizisoma umu niliishia kusoma nakuchoka tu. Yani mmetofautiana na mtu kitaa alafu unakuja kumwanzishia mada ni zaidi ya ushamba ila ni unyama.

Mimi siku moja namzingua member mmoja umu kimasihara tu nashangaa eh pm zina miminika napewa big up napewa mpaka taarifa nisizoomba kwa kweli nilishtuka nikaona kumbe kuna mambo sio kama tunavyoyachukulia wengine unaweza kucheza muzki usioujua.

Humu kuna wehu....tena wengine wanaelimu zao lakin sijui inakuaje yani...mxeeeew
 
Kuna mtu tulikuja kutofautiana akawa anani bully na matusi kwenye nyuzi. Nilipokuja ku retaliate alitia akili. Hovyooo!!
 
Umeongea ukweli, kuna thread kama mbili nilizisoma umu niliishia kusoma nakuchoka tu. Yani mmetofautiana na mtu kitaa alafu unakuja kumwanzishia mada ni zaidi ya ushamba ila ni unyama.

Mimi siku moja namzingua member mmoja umu kimasihara tu nashangaa eh pm zina miminika napewa big up napewa mpaka taarifa nisizoomba kwa kweli nilishtuka nikaona kumbe kuna mambo sio kama tunavyoyachukulia wengine unaweza kucheza muzki usioujua.

Kweli, humu mtu uatakiwa kuwa makini, kuna ngoma zinapigwa chini chini, unaweza kujikuta unacheza ngoma usiyoijua...
 
Kama yule mwanaharamu daktari wa IMTU, aliyenisambazia picha zangu za utupu, kwa kweli kila nikifikiria nakosa la kufanya.
Yote namuachia Mungu....ila ipo siku.

Madame B utakua sio wa kawaida, mpaka daktari asambaze picha zako inaelekea una maumbile adimu.
 
Kwa hiyo mnataka wote tuwe na ideas sawa? Wengine wataleta utoto, masikhara, ujinga na upuuzi. Ndivyo maisha yalivyo, hata huko mitaani, kazini, misikitini na makanisani ndivyo watu walivyo..!

Mtu kwenye busara anachanganua kipi cha kuchangia na kipi sio cha kuchangia. Ajabu Ni kuwa tunalalamika lakini ikija thread ya kipuuzi sie ndio wa kwanza kuipa traffic.

Kuwa bullied mtandaoni ni kujitakia tu. Ukishea na mtu privacy zako, humjui-hakujui, akija kukugeuka unamlaumu nani. It's simple, don't share your privacy with everyone. Mnatuma picha za uchi au mnatongozana mtandaoni...unategemea mkikosana itakuwaje?
 
Back
Top Bottom