CWT yaanza kusambaza ujumbe wa simu (sms) za mgomo kwa walimu nchi nzima

Ualimu ni wito jamani ni kazi ya kujitolea kama jkt,na hiyo ni motisha tu mnayopewa sio mishahara..!sasa wewe dokta kapata div1 ya pcb we umepata dv4 ya hkl alafu unataka mlipwe sawa huo utakuwa uchizi sio bure

Kweli wewe ni kilaza namba moja. Kufahamu mambo siyo kufaulu tu darasani lazima uwe na tabia ya kujifunza. Kuna walimu wenye digrii moja, mbili na Phd; je, hao nao walipata divisheni 4? Umeshindwa kutambua kuna walimu wa kada mbalimbali? Je huyo daktari aliyepata divisheni 1 au 2 ya pcb alifundishwa na mwalimu aliyepata divisheni 4 ya HGL? Unataka kutuambia mwalimu aliyesomea HGL anaweza kufundisha Physics, Chemistry na Biology(PCB)?

Ni kweli kuna walimu wa shule za msingi ambao wengi walipata divisheni 4 kidato cha nne. Lakini si wote walipata huo ufaulu. Hata waliopata divisheni 4 kidato cha si vilaza maana wamewezesha vijana wengi kufanikiwa kielimu.

Ikumbukwe kuwa hata ktk idara ya afya kuna clinical officers ambao ni vilaza; wameshindwa kutatua matatizo ya afya ya watanzania. Hali hii imesababisha watanzania kuteseka na magonjwa kila siku. Mfano babu wa Loliondo alipotangaza kikombe tulishuhudia watu wengi wakikimbia hospitali na kuelekea kwake. Hata hao vilaza ma-clinical officers na madaktari nao walikimbilia kwa babu. Kufaulu mtihani ni jambo moja na kutenda ni jambo jingine

Walimu msikatishwe tamaa na wapumbavu kama Dully. Piganieni maslahi bora ili muweze kumudu gharama za maisha. Jambo la msingi ni kujiamini. Hakuna maendeleo yoyote bila mwalimu.

Pia mtambue kuwa CWT kimevamiwa na usalama wa taifa(usalama wa CCM) na makada wa CCM. Makatibu wa wilaya na baadhi ya wenyeviti ktk ngazi mbalimbali ni makada wa CCM au wana-usalama wa CCM. Ondoeni hao watu kwanza
 
Kaza buti walimu. kama manesi ambao wengi ni darasa la saba, matabibu na madaktari wameweza kwa nini ninyi msiweze?
 
Acheni kugoma mnawaumiza watanzania maskini wao wanasomesha nje ama kwenye shule nzuri ambazo walimu wanalipwa vizuri.

Ushauri wangu kwenu Waalimu na Madaktari Gomeni kuwapa kura CCM si mmeona Zitto kabwe kima cha chini 300,000 na ushee, amkeni CCM na serikali yake ndo wanaowaumiza si watanzania Maskini!
 
Tupo hapa tulipo kwa sababu ya UDHAIFU wa Rais Kikwete, Bunge legelege na upuuzi wa CCM! - J J Mnyika - Mbunge - Ubungo.
 
Source please???- Kilimo/mifugo 959,400/= certificates holders- KLM/MFG 1,133,600/= Diploma holders- Klm/MFG 1,354,000/= Degree Holdersmimi ni mdau katika fani hii na hizi taarifa zilizowekwa hapa siyo za ukweli hata kidogo pia zinalenga kutugombanisha na familia zetu maana mama watoto amenipigia simu akinituhumu kuwa mdanganyifu kwenye income declaration MODERATOR naomba kama huyu aliyeleta uzi hatatoa source ya data hizi kama alivyoombwa apigwe BANE ya maisha hapa jukwaani - naomba kuwasilisha.

Mbona watu wa mifugo certificate wanaanzia na Tsh 228,000.=
 
Haya mambo sisiem ieyalea muda mrefu sasa yanaanza kulipuka..
kwa nini mwalimu adharaulike kiasi hiki?? kwani yeye hana haki kupokea mshahara mzuri kama watumishi wengine??
"ILA WAALIMU NAO MMEZIDI KUIENDEKEZA CCM MSHATUKANWA SANA NA VIONGOZI WA HIKI CHAMA" ila mwisho wa siku mnapozwa na hela ya sensa na uchaguzi na vifulana mnawekewa mziki mkubwa mnacheza viduku mnaenda kulala kesho msoto kama kawaida
 
Walimu wana bahati mbaya sana kwa kuwa wanachama wa cwt.cwt viongozi wake asilimia kubwa ya shughuli zao ni vikaovikao tu visivyokuwa na tija kwa walimu.mwl ukienda kwao hakuna msaada unaopata kwao.sasahivi wamesisimka na kukulupuka wanadai eti mgomo-lakini muda si mrefu utasikia wamesitisha wanafanxa mazungumzo zaidi.walimu tunahitaji kukikataa chama hiki-ni cha wachumia tumbo.
 
mkuu umesema kweli kabisa viongoz wa cwt ndio wanaotuangusha sisi waalim but hata wao sasa hivi tutawatoa na tutadai haki yetu hadi kieleweke

Enhe! Kumbe nawe ni mwalimu, ninyi ndo mnaosaidia ccm kufoji ushindi sasa mjibebe ccm haiwajui mpaka hapo 2015 wataikumbuka mbeleko yao.
 
serikali ilishakalili kuwa walimu ni wito sasa wanatakiwa wabadilike kwa kuonyesha vitendo kwa walimu wa kada zote la sivyo kwa kipindi hiki mgomo unanukia zaili shairi kwani walimu utajua kwamba wamegoma ktk matokeo ya wanafunzi na sio kuandamana barabarani kama tunabisha tusubiri matokeo ya darasa la saba, kdt cha nne na sita ndipo utajua walumu waligoma au la.
 
Mshahara wa mbunge umepanda hadi 10,000,000/= utaanza julai 012, ninyi endeleeni kuibeba ccm
 
Walimu vyuoni hufundishwa maadili ya kuwa watu wema mbele za watu wa rika zote...ikiwemo viongoz wao, wanafunz wao n.k, hii saikolojia ya uoga walojengewa ndo inaisaidia serikali kusambaratisha migomo yao.
 
Walimu serikali hii isiwalipe maana hawana shida kila siku ni kutishia kugoma halafu hugomi hata kama ni mimi nafahamu tabia yako ya kutokua na msimamo na unafiki sikulipi najua njaa ndiyo shida yako nakupiga ahadi na mazungumzo. Toka nasoma mpaka leo hadi nimemaliza chuo kikuu nasikia walimu wako katika mazungumzo, acha waendelee na mazungumzo. Serikali ya CCM msiwalipe walimu hawana shida ndiyo maana hawagomi!!!
 
Siwaungi mkono kwani ualimu ni wito kwa sasa,we huoni wanaosomea ualimu ni waliofeli form4&6?hilo ni chaka la vilaza,tena hyo wanayolipwa ni nying sana ingepunguzwa

F@k ur useles brain! Unataka kuniambia hao madaktari na mainjinia walifundishwa na masabury yako? Kauli yako imenikera sana...nchi zingne mwalim ni mtu mhmu sana ila tz ndo anaonekana failure! Failure mkapeleka watoto wenu mashuleni? Mngewafundisha nyumbani kwenu bs? *****!! Ashakum waungwana!
 
Viongozi wa CWT Ninyi ndo mnaowasaliti waalimu kwasababu mnajilipa mishahara mikubwa na maposho yanayotokana makato ya haohao waalimu.
HEBU TIZAMA TOFAUTI HII YA KUTISHA YA VIWANGO VYA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA WA TZ! (Ajira mpya cheti)

Mwl 244,400/= Afya 472,000/= Kilimo/mifugo 959,400/= Sheria 630,000/=


Diploma mwl 325,700/= Afya 682,000/= KLM/MFG 1,133,600/= sheria 871,500/=


degree mwl 469,200/= Afya 802,200/= Klm/MFG 1,354,000/= Sheria 1,166,000/= Je upo tayari kuvumilia kunyanyaswa hivo katika utumishi wa umma wa taifa moja lenye soko la bidhaa lililo na mfumuko wa bei wa kutisha? Ungana na Cwt kudai nyongeza ya mishahara 100%, Teaching allowance hardship allowance. Wape sms hii walimu 20 tu! Mshikamano daima.
 
Siwaungi mkono kwani ualimu ni wito kwa sasa,we huoni wanaosomea ualimu ni waliofeli form4&6?hilo ni chaka la vilaza,tena hyo wanayolipwa ni nying sana ingepunguzwa

Hapo kwenye red
Hivi wewe ulifundishwa na walimu waliopata ngapi?
 
F@k ur useles brain! Unataka kuniambia hao madaktari na mainjinia walifundishwa na masabury yako? Kauli yako imenikera sana...nchi zingne mwalim ni mtu mhmu sana ila tz ndo anaonekana failure! Failure mkapeleka watoto wenu mashuleni? Mngewafundisha nyumbani kwenu bs? *****!! Ashakum waungwana!

Hata mimi kanikera!
Ni sawa na wale wanao dharau wazazi wake kisa yeye kasoma!
Baba na mama hata waweje, wao ndio wamekufikisha hapo ulipo!
Wasomi wote wamefunzwa na hao walimu anaowadharau!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom