Kwanza nakupa pole kwa kusomea hiyo kazi ngumu, na inayo dharauliwa mpaka na wale wananchi failures wa kila kitu katika jamii!
Pili unatakiwa kufahamu fika hiyo CWT ni tawi la ccm! Hivyo inatumiwa na hiyo ccm miaka nenda kuwaibia walimu pesa zao kupitia 2% ya ada ya uanachama kila mwezi.
Na fedha hiyo hutumiwa na viongozi wa hiyo CWT kugawana posho kwenye vikao vyao vya kipiuzi, na kiasi kinachobakia huwasaidia ccm kwa siri nyakati za uchaguzi mkuu ili kununulia kofia, tshirt, vitenge, viremba, nk vya kuwahongea wananchi wasio na elimu ya uraia.