CWT kutoa tamko utata wa malipo ya walimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CWT kutoa tamko utata wa malipo ya walimu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sumasuma, Feb 6, 2012.

 1. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Gedius Rwiza
  CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT),kimesema kuwa Jumatatu ijayo kitatoa tamko kuhusu utata unaoendelea katika ulipaji wa madai ya walimu sehemu mbalimbali nchi.

  Hatua hiyo ya CWT imekuja baada ya walimu wengi kuilalamikia Serikali kwa kushindwa kuwalipa fedha zao kama walivyohakikiwa jambo ambalo limesababisha baadhi ya walimu kufanya mgomo, ambapo walimu 54 wa Halmashauri ya Rungwe wamefutwa katika orodha ya malipo hayo.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Rais wa CWT,Gratian Mukoba alisema kuwa kikao cha Baraza la CWT kilifanyika mwishoni mwa mwezi Januari na kwamba walikuwa wakisubiri kuendelea kukusanya taarifa za ulipaji wa fedha hizo na kwamba hadi sasa kuna malalamiko mengi kutoka halmashauri mbalimbali.

  “Ni kweli hali sio nzuri katika mchakato mzima wa ulipaji wa fedha za walimu ambazo Serikali ilikubali kuanza kuzilipa. Tunapokea malalamiko mengi na baadhi ya walimu wanafutwa katika orodha ya malipo wakati Serikali ilituma fedha hizo kulingana na uhakiki ilioufanya, lakini kuna watu wengine wanaojitokeza kuvuruga mchakato huo,”alisema Mukoba.

  Wakati hayo yakiendelea uongozi wa CWT Manispaa ya Ilala umeilalamikia Serikali kwa kuwapelekea walimu fedha pungufu ikilinganishwa na idadi ya walimu wanaotakiwa kulipwa.

  Katibu wa CWT, Manispaa ya Ilala James Manyama alisema kuwa shule za msingi zilitakiwa kupata Sh 193 milioni lakini wamepelekewa Sh120 milioni ambazo ni za likizo kwa walimu ni 836.

  Alisema kuwa kwa upande wa shule za Sekondari Sh61 milioni zimefikishwa kwao badala ya Sh131 jambo alilosema linawapa mtihani mgumu.

  :lol:
   
 2. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Walimu tumewachoka na kulialia kwenu,si mgome au mnataka nani awagomee?
   
 3. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Waache waendelee kuwa legelege wadhani kuna atakaewatetea
   
 4. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,983
  Likes Received: 23,687
  Trophy Points: 280
  Yani hakuna watu wanaoniboa kama walimu..... Wao wameshikilia mpini na Serikali imeshikilia makali lakini bado wanalialia tu badala ya kuichanachana seikali ya nchi ya kitu kidogo.
   
 5. t

  taranda Member

  #5
  Feb 6, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu rais wa walimu ovyo sana. Ni majuzi kawasemea mbovu madaktari na mgomo wao. Kumbe nae ni mhanga wa malimbikizo ya madai. Wakae kimya ishu ya madaktari imalizike kwanza. Badala ya kuwasapoti madaktari yeye kaanza kutafuta umaarufu wa siasa. Ovyo kabisa huyu jamaa
   
 6. n

  nyangasese Senior Member

  #6
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sioni sababu ya serikali kutowalipa walimu madai yao kwa muda muafaka.mbona wabunge hawana malimbikizo,au serikali inafanya hivyo ili walimu wapige kelele ili ionekane walim wanalipwa.mbona wabunge wanaongezewa posho kimya kimya.ktk hotuba ya mwaka mpya rais aliagiza kusiwepo na malimbikizo kwa watumishi lakini leo mwanza walimu wana miaka 3 bila kurekebishiwa mishahara cwt wamekaa kimya
   
 7. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,134
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Babu I salute youuu
   
 8. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Hivi hao nao wanajihesabia wana akili kichwani hao. Yaani wakichoka kushika chaki ndo wanakumbuka madai yao. Waende zao huko, acha wanaume wadai chao, tumewachoka walimu. Hawana maana yoyote ktk nchi hii, na wenyewe wanalijua hilo ndo maana wakitishwa kidogo wananywea
   
 9. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  tatizo lao wanatumia masaburi ktk kuwaza na kutenda
   
 10. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  hiv wewe bado unaendelea kumuamini ****** kwa yale anayosema, kalaga bhaho
   
 11. M

  Mnyaturu Member

  #11
  Feb 6, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nawaheshmu sana walimu.leo tunategemea tamko la ukweli ambalo litakuwa na manufaa kwa wanauma wote.kwanini tuendelee kuteseka wakati haki yetu.lazima serikali tuijambishe jambishe.
   
Loading...