CWT chama cha matumizi kuliko uwekezaji

The golden

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
1,381
2,553
Nimewahi kuwashauri CWT kipindi kile nikiwa mwanachama wao kuwa kwa kuwa wanachama wake wengi( walimu) wana uchumi duni kutokana na maslahi duni wanayopata kutoka kwa mwajiri wao. Chama kijikite zaidi katika uwekezaji badala ya matumizi.

Hili linawezekana kama CWT wataachana na matumizi yasiyo ya lazima ikiwemo ununuzi wa magari makubwa kwa makatibu wa mikoa. Jambo la pili ni kupunguza muundo wa uongozi wa chama kwa lengo la kubana matumizi kwa kupunguza vikao vinavyotumia fedha nyingi.

Naomba kutoa mfano wa structure ya chama ngazi tu ya wilaya. Kwenye level ya wilaya kuna muundo ufuatao
1. Sekretarieti, inayoundwa na Mwenyekiti, katibu na mhazini
2. Kamati ya uendeshaji
3. Kamati tendaji
4. Mkutano mkuu
5. Kuna vitengo vya; wanawake, walemavu na vijana.

Structure yote hii inatumia michango ya wanachama kujiendesha. Ukiangalia kwa makini majukumu yanayofanywa kwa mfano na kamati uendeshaji yangeweza kufanywa na kamati tendaji ili kupunguza matumizi.

Unapokuwa masikini jitahidi kupunguza matumizi. Peleka pesa yako kidogo kwenye uwekezaji ili ujikomboe.
 
CCM ilishaFELI kabisa kiutawala.

Sasa hivi mbinu wanayotumia ni KULA na kila mwenye USHAWISHI.

Hakuna kundi lolote LA Kijamii ambalo CCM haina Mkono.

Na kwasababu CCM haiwezi kuwapa pesa vyama vya wafanyakazi, imewaruhus KUKATA MISHAHARA ya WATUMISHI Zig zag ili wasipige kelele.

Kwahiyo kazi kubwa ya hiyo MICHANGO ni KULA tu.
 
CCM ilishaFELI kabisa kiutawala.

Sasa hivi mbinu wanayotumia ni KULA na kila mwenye USHAWISHI.

Hakuna kundi lolote LA Kijamii ambalo CCM haina Mkono.

Na kwasababu CCM haiwezi kuwapa pesa vyama vya wafanyakazi, imewaruhus KUKATA MISHAHARA ya WATUMISHI Zig zag ili wasipige kelele.

Kwahiyo kazi kubwa ya hiyo MICHANGO ni KULA tu.
Seen
 
Viongozi mmeona comments za wanachama wenu? Zifanyieni kazi nasi.
IMG_20220226_114247.jpg
 
Back
Top Bottom