Kuna mambo yananitatiza kwenye hii CV
Moja.... Kuteuliwa kwenye viti maalum and then naibu waziri ( hii haiji labda kama alipewa huo uviti maalum ili aweze kupewa ulaji wa unaibu waziri, na kama hii ni kweli ina maana kuna mkono wa mtu hapo! Haiwezekani rais from no where aanze mteua mtu kwenye viti maalum na kumweka kwenye unaibu waziri kama hamfahamu, hapa ina maana rais anafahamiana na huyu na ndio maana inakuwa ngumu kuchukua maamuzi dhidi yake.
Ukiangalia vizuri kwenye elimu yake toka 1985 mpaka 1991, yeye alikuwa anafululiza kwenda kusoma tu tena nje ya nchi! Je alikuwa anajilipia au alikuwa analipiwa na serikali? Haiingii akilini mtu aunganishe degree baada ya degree pasipo hata kuja kupractice alichosomea mwanzo( nina imani tukichimba zaidi hapa tutaona kuna walakini kwenye huku kusoma huku).