Tumejaza fomu na kuzirudisha, tutaitwa kuhojiwa na vikao, ili kupeleka majina kwenye vikao uteuzi, hapo sasa ndipo nitawajulisha tuanze kusali tukifunga na kuomba ili jina lipitishwe. Uchaguzi ni Bunge la NovemberTufunge lini? Tulisogeze mikononi mwa Bwana
Tumejaza fomu na kuzirudisha, tutaitwa kuhojiwa na vikao, ili kupeleka majina kwenye vikao uteuzi, hapo sasa ndipo nitawajulisha tuanze kusali tukifunga na kuomba ili jina lipitishwe. Uchaguzi ni Bunge la November
Sisi CCM tuko 186 tukigombea nafasi 6!.
p
Naunga mkono hoja, Wasukuma wenyewe asili na halisi ni watu poa sana, ila siku hizi kumeibuka kada mpya ya Wasukuma wa ajabu ajabu wenye tabia za ajabu ajabu tofauti kabisa na tabia za kiasili za Wasukuma asili na halisi. Hawa watu wanatuharibia sana kabila letu na kutufanya Wasukuma wote tuonekane ni watu wa ajabu ajabu!.Hakuna MTU ambaye hajakaa na wasukuma they are cool and nice people. Chunguzen hao wengine
Amen Amen, Tumtangulize Mungu kwenye hili, afungue njia.Utapita Mkuu!!!Unastahili
AMENMkuu Tate Mkuu, kwanza ni kweli kabisa kuna watu wana vipaji lukuki, yaani multi talented, ila kutokana na kutegemea fani moja tuu, vipaji vyao vingine vinakuwa havionekani, mimi ni mtangazaji wa redio, yaani radio announcer, enzi nikiwa mtangazaji wa RTD, sikufahamika sana, kwasababu nilikuwa ni mtangazaji wa External Service, idhaa ya Kiingereza, matangazo yake wali ya beamed nchi za Kusini mwa Africa kusaidia ukombozi wa nchi za Kusini mwa Africa hivyo sii wengi wananijua kama mtangazaji mzuri tuu wa redio.
Nikiwa RTD pia nilikuwa a Radio DJ, na Music DJ.
Mimi ni mtangazaji wa TV Talk Show Host wa kipindi cha Kiti Moto.
Mimi ni AV producer, yaani sio mtangazaji tuu bali pia ni mtayarishaji wa vipindi, content producer, presenter na sasa distributor.
Mimi ni journalist nikiandika for print media na electronic media
kazi hii nimeifanya kwa miaka 30 mpaka nimestaafu.
Baada ya kustaafu ndipo sasa nimejigundua kumbe nina kipaji cha uongozi ambacho kilifunikwa na utangazaji, nilikigundua nilipo beeb uchaguzi wa ubunge Kawe, japo niliambulia kura moja tuu, kutoka kwa wajumbe, kuna kitu nikajifunza, sasa kumetokea fursa nyingine ya kukipima kipaji changu cha uongozi, nime ingia in full, na kiukweli nitalisaidia sana taifa langu hili katika hilo jambo langu.
Mungu Nisaidie.
Paskali.
Mkuu guzman_ , kwanza asante kunianzishia thread, nina jambo languNdg wana JF. Wasalamu.
Hivi karibuni nimejaribu kupitia michango/thread zilizoletwa na mtajwa hapo juu.
Kwa namna ya uandishi wake na mawazo yake imenilazimu kutaka kujua Pascal Mayala ni nani hasa? Kiwango chake cha elimu? professional yake ni nini?
Mkuu Yahana Mbatizaji, johnthebaptist , amen, amen!.Tumuombee mwanaJF Pascal Mayalla apitishwe
Wote tuseme Amen!
UpdateMkuu guzman_ , kwanza asante kunianzishia thread.
Pascal Mayalla ni mwana JF mwenzenu mtu wa kawaida sana.
Kiwango changu rasmi cha elimu ni darasa la 7, ila baada ya hapo nikaanza kuungaunga mara usome hiki mara kile, nikaungaunga hadi nikawa mwandishi wa habari na mtangazaji, nikaendelea kujisomea kwa kujisomesha kwa elimu ya kuunga unga hadi kuhitimu shahada ya sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, ambapo ilinichukua miaka 15 kukabidhiwa LL.B yangu na ikanichukua miaka 5 mingine kukubaliwa kuwa wakili.
Professional yangu ni Mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea na sasa ni Wakili wa kujitegemea kwa kujitolea kutetea haki kwa watu na uwezo wa kuajiri wakili.
Niliwahi pata ajali mbaya ya Piki Piki nikadhaniwa nimekufa kumbe nilizimia tuu nikafufukia baridi la mortuary, kwa muda niliozimia madaktari wakasema nitakuwa confined to a wheelchair!, nilikuja kusimama and here I'm.
Sio tuu ni Mtanzania, bali ni Mtanzania original halisi na Mzalendo wa kweli wa taifa hili.
Asante
Mimi naandikia watu watatu humu
Ikitokea wewe ni simple mind ukakutana na mada ya great minds, utaishia chaka!. Hiki ndicho kilichokukuta wewe uliposoma bandiko hili Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze..., ukikutana na mada iliyokuzidi kimo, lazima utaishia kuingia chaka. Pole.
- Kuna mada nawaandikia wananchi wa kawaida simple minds, ambao hawahitaji kufikiri chochote, wao interest zao ni kusikia tuu chochote, hizi ni mada kuwahusu watu, naziandika kwa ajili ya simple minds ambao wao interest zao ni habari za watu.
- Mimi kama Mwandishi wa habari, kuna mada naripoti kuhusu matukio mbalimbali, Kwa ajili ya ordinary minds ambao hu discuss events, kumetokea nini wapi na ikawaje.
- Na kuna mada naziandika kwa ajili ya great minds, hizi ni mada kuhusu ideas na wasomaji they need to think. Mada hizi huziandika kwa coded ili kuelewa nazungumzia nini ni lazima kwanza uwe na uwezo to read in between the lines, pili uwe na uwezo wa kuzibaini hizo codes na uncode the codes to connect the dots.
Ila pia kiukweli nimeisaidia sana jf kuwa transforms simple minds wengi kuwa great minds. Na wewe uliposoma mwanzo bandiko hilo ulikuwa simple mind, sasa lisome tena huku unatafakari utapata kitu kingine, akisoma ikashindwa kabisa kujua nazungumzia nini, then bandiko hilo sio saizi yako.
Karibu ujaribu, ukishidwa kabisa nitakufungulia baadhi ya codes.
P.