CV ya Dr Slaa From Certificate to PhD

Status
Not open for further replies.
Nyie wasomi wa wapi? Kama mtu ka skip ni kichwaaa! Mark mwandosya from bsc eng mpaka phd! Mnadiscuss vise versa!
 
Reactions: FJM

Haya maneno ni yako CV ya Slaa sio ya kwanza mie kuileta acha watu wajadili kuna members wapya wanaitaji kujua sio wote wana miaka mingi humu JF.
 
Nyie wasomi wa wapi? Kama mtu ka skip ni kichwaaa! Mark mwandosya from bsc eng mpaka phd! Mnadiscuss vise versa!
 
Haya maneno ni yako CV ya Slaa sio ya kwanza mie kuileta acha watu wajadili kuna members wapya wanaitaji kujua sio wote wana miaka mingi humu JF.


Soma post No 19.
 
Huelewi kimya! Mtu akiwa na akili zisizo za kawaida anaskip! Ukifanya thesis unaweza kuruka! Kama aliruka ni extraordin
 

Na wewe ni padre?
 
Huelewi kimya! Mtu akiwa na akili zisizo za kawaida anaskip! Ukifanya thesis unaweza kuruka! Kama aliruka ni extraordin
 
Unless kama kichwa kimejaa matapishi, lakini thread unayoleta hapa ipo majukwaani kwa miaka sasa. Shughulisha ubongo wako, sio kumtumikia mume bila kufanya hata vetting ya analokutuma.

Huyu jamaa ni mpuuzi sana anashindwa mdiscus fake Dr....analeta upuuzi wa kutumiwa na napi.....na waweza kuta ni mbumbumbu sana kajichokea mithri ya mgonjwa wa kwashiokohor......uwakala mwingine ni hatari sana....
 
Halafu kuna wazembe humu wanamwita Dr wakweli, sasa hiyo phd ameipataje wakati hata degree hana? Halafu mbona povu linawatoka kuhusu hii topic? CV za watu kibao zimemwagwa humu JF na mkazipoindea.
 
Halafu kuna wazembe humu wanamwita Dr wakweli, sasa hiyo phd ameipataje wakati hata degree hana? Halafu mbona povu linawatoka kuhusu hii topic? CV za watu kibao zimemwagwa humu JF na mkazipoindea.

Soma post No 9. halafu unganisha na link iliyopo.
 
Huyu jamaa ni mpuuzi sana anashindwa mdiscus fake Dr....analeta upuuzi wa kutumiwa na napi.....na waweza kuta ni mbumbumbu sana kajichokea mithri ya mgonjwa wa kwashiokohor......uwakala mwingine ni hatari sana....

Maneno mengi yanakutoka bure mie sina kitu ni masikini wakutupwa mnywa kahawa tu.
 


Kafungue kesi mahakamani wewe ni CCM utasikilizwa kwa kuwa ni Watanzania wengine wana jiuliza juu ya PhD za Nchimbi, Matayo , na mawiri kibao lakini serikali kimyaaaa
 
Huyo ndio rais wangu.. Makame na Kiravu walituwekea mtu dhaifu!

By the way... unatujazia server huu uzi upo mara nyingi sana humu
 
CV ya vick kamata? naona sasa mmeamua kuingia hadi jikoni . Laizma watoto wa baba wawe wakali
 
CV ya vick kamata? naona sasa mmeamua kuingia hadi jikoni . Laizma watoto wa baba wawe wakali

Siasa ngumu ndugu yangu na gharama za 'ueshimiwa' ni kubwa. kadhia tupu. Sasa tumeshambiwa hata mwaka wa kuzaliwa ni wrong.

NB: Umejaribu kutafuta hizo publications zake? Ningetaka sana kusoma hiyo ya microfinance kwa wanawake lakini nimefanya search sioni chochote!!!.
 
Ritz,

Kwa muda mwingi nimekuwa nikipuuzia post zako kwa sababu wewe mwenyewe umefanya iwe hivyo.

Hata hii nilitaka kupuuzia lakini nimeona nikushauri njia ambayo niliwahi kuitumia. Njia yenyewe ni hii.

Mimi ni mkatoliki. Ninapenda sana kujua mambo ya kanisa langu. Lakini kwa sababu sijawahi kupita Seminary nikadhani kufahamu mambo ya Kanisa langu ingekuwa rahisi kwa sababu mimi ni msomi na ninaelewa mengi.

Nilikwama. Kanisa Katoliki ukiliparamia ovyoovyo unaweza kuishia kuaibika kama inavyokutokea sasa. Labda uniulize ni kwa nini hapa duniani taasisi nyingi zikiwemo nchi kubwa zinaumbuka zinapolivamia Kanisa Katoliki kutaka kushindana nalo kwa hoja yoyote?

Jibu ni kwamba Kanisa katoliki ni taasisi pekee hapa duniani yenye umri mrefu kuliko taasisi yoyote. Hadi sasa ina umri wa miaka 2012.

Hivyo, usidhani kuna swali utalileta halafu Kanisa Katoliki likose majibu. Unaweza kukutana na mkatoliki ukakosa majibu lakini tatizo likawa ni huyo mkatoliki na si lenyewe kama Kanisa.

Ni kweli unaweza kuleta jambo humu JF na ukakuta wote wameshindwa kukujibu na wengine wakaishia kukutukana au kukukejeli. Mimi hao pia nawaonea huruma kwani ukweli ni kwamba majibu yako utashangaa kuona kwamba yalishatolewa miaka 500 iliyopita na wewe unarudia swali leo!

Mimi nilivyoona hivyo, nilicukua kama miaka mitatu najisomea tu mambo ya Kanisa langu. Ritz, nakujibu kiurafiki, kulielewa Kanisa Katoliki unahitajia uvumilivu wa hali ya juu kama umedhamiria kusoma mambo yake.

Mfano wa aibu mnazopata ni mwaka 2009 ambapo Waraka wa Kanisa ulitoka. Watanzania mlishangaa kana kwamba ni mara ya kwanza wakati waraka wa kwanza duniani ulitoka mwaka 1891 ukiitwa Rerum Novarum uliotolewa na Pope Leo XIII. Watanzania mkaaibika duniani kote kwamba ni washamba hawajui nyaraka za Kanisa Katoliki. Tena wakaaibika watu mashuhuri kama Kingunge!



Ona sasa topic unayoileta ya kuuliza Phd ya Dr. Wilbord Slaa. Ni wazi kwamba huelewei kwamba Kanisa Katoliki ndilo mama wa Sheria hapa duniani lakini kubwa zaidi Kanisa Katoliki ndilo mama wa mifumo ya elimu hapa duniani.

Ujerumani iliacha mwaka 1886 kukaguliwa sylabus na majesuit ambao ni mapadri wa Kanisa Katoliki ambao hapa nchini wanaendesha shule maarufu yaani Nyakahoja ya Mwanza na Loyola ya D'Salaam, St. Ignatius ya Dodoma na wamefungua Sekondari hapohapo Dodoma.

Uingereza nayo ilianza shule zake mapema kabla ya Ujerumani na ikafuata mfumo wake.

Lakini kote huko Kanisa likaendelea na mfumo wake mmja uitwao Licentiate au Licenciatura. Nenda kwenye website yoyote halafu soma kwa makini neno Licentiate ndipo utakuta mfumo waliosoma Dr. Slaa na wenzake wengi umejikita humo.

Hebu soma mfumo wa elimu wa nchi zifuatazo yaani Germany, Argentina, France, Australia, Canada, Belgium, Brazil, Bolivia, Costa Rica. Huko kuna vyuo wanafuata mfumo huu wa Licentiate. Huko kukuta mtu kamaliza Diploma halafu anapata Phd ndiyo maisha ya huko.

Sisi hapa Tanzania tuliamua kufuata mtindo wa Uingereza na hasa Oxford. Uingereza waliamua kubuni upya kabisa mfumo wa elimu.

Hivyo, Ritz na wenzako, unpouliza swali kama hili ni wazi kuwa inabidi ujikite maeneo ambayo ni wazi na wao upeo wao ni mdogo. Ungekuwa thread yako umeiandika kwa kiingereza na tukakutana kwenye anga za international threads na tunajadili mataifa mbalimbali ungeumbuka umbuko ambalo hutalisahau, kwani ni wazi wapo ambao wangeuliza umetoka nchi gani huelewi system hiyo ya Eductaion.

Mimi hata leo nikilichukia Kanisa Katoliki na nikaingia katika timu ya watu wanaolichambua kwa kuumbua mambo yake, basi ningekutana na nyinyi kisha nikawapa semina kwamba tubadili mbinu maana hizo mbinu zenu mtaishia kuumbuka tu.

Kawaulize waarabu ambao waliwahi kupiga kelele kuhusu Vatican kupewa ubalozi kwenye nchi kadhaa lakini jinsi wlivyozidisha kelele na wakikaa meza moja na Vatican wanajikuta na wao wanaishi kushawishika kufungua balozi nyingi kama Iran na kwingineko.

Waulize Russia ambako walikejeli sana Ubalozi huo na mwisho nao wakajikuta wanaufungua kwao. Wamarekani tangu mwaka 1871 walikataa ubalozi huo, wakajikuta mwaka 1994 wanaufunguwa kule Washington.

Leo wewe umeuliza swali kuhusu Phd. ya Dr. Slaa. Si mara ya kwanza unauliza hivi. NImesema ukisoma kuhusu Licentiate education system utajikuta umefunguka usichikijua na utashukuru Mungu kwamba unatumia ID ya jina la Ritz na hivyo aibu ya ushamba hutaipata maana hatukujui.

Soma tu utaelewa, document zipo tele. Ni kichwa chako tu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…