CUF yataka Eddy Riyami aachiliwe haraka

CUF yataka Eddy Riyami aachiliwe haraka

kapime akili ndiyo jibu sahihi kwako!
unauwezo finyu sana wa kuona mambo
Mkuu asante ntakwenda, ila kabla ya kwenda mm heb jarb nawe kujifikiria kama unapaswa kupima akili au laa? Maana cjaona hapo uhusika wa ccm,

Kwa mtazamo wangu mkuu kapime kwanza kisha njoo na majib, nami ntakwenda... ila cjapata mtu ambae anaweza kuhusianisha ccm na hlo tukio... Kapime akili mkubwa kunamahali unahisia mbaya....
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tarehe: 23 Februari, 2016

Wiki iliopita, mnamo tarehe 16 Februari, 2016, aliyekuwa mjumbe wa Timu ya Kampeni ya Chama Cha Wananchi (CUF), Ndugu Mohamed Ahmed Sultan Al-Mugheiry (maarufu kwa jina la Eddy Riyami), alipokea barua ya wito kutoka kwa Jeshi la Polisi Zanzibar ikimtaka kufika Makao Makuu ya Polisi, Ziwani, Zanzibar siku inayofuata, yaani tarehe 17 Februari, 2016, saa 2 asubuhi kwa kile kilichoelezwa kwamba “kuna mambo muhimu yanayomhusu” ambayo walitaka kuzungumza naye.

Bila ya kukosa, Eddy Riyami aliitikia wito huo na kufika Makao Makuu ya Polisi, Zanzibar na kuonana na SSP Simon S. Pasua wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID). Hata hivyo, hakuhojiwa na badala yake alipewa simu na kutakiwa azungumze na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Bw. Salum Msangi ambaye alimwambia arudi tena Jumatatu, tarehe 22 Februari, 2016.

Eddy Riyami, akiwa raia mwema, alirudi tena jana kama alivyoagizwa. Alipofika hapo alihojiwa na Polisi na baadaye mwanasheria aliyefuatana naye akatakiwa kutafuta wadhamini wawili watakaomdhamini hadi atakapoitwa tena. Wakati mwanasheria wake aliporudi na wadhamini, akaelezwa kwamba Polisi imebadili uamuzi wake na imeamua kumuweka ndani hadi leo, tarehe 23 Februari, 2016. Mwanasheria na familia yake wakatakiwa kwenda tena Makao Makuu ya Polisi hiyo leo, saa 3 asubuhi. Walipofika leo asubuhi, wakaambiwa kwamba DCI kaacha maagizo kuwa suala la Eddy Riyami liachwe kwanza na wao warudi tena saa 6 mchana.

Hadi tunapotoa taarifa hii, hakujapatikana maelezo yoyote ya msingi juu ya kinachoendelea na wala Eddy Riyami hajafikishwa Mahkamani kusomewa mashtaka yoyote.

La ajabu zaidi, ni kwamba hata mke wake alipofika kituo cha polisi cha Madema anakoshikiliwa kwa ajili ya kwenda kumuona, hakuruhusiwa kumuona.

Kutokana na mwenendo huu, Chama Cha Wananchi (CUF) kinalichukulia suala hili kwamba ni mwendelezo wa vitendo vya unyanyasaji wa kisiasa dhidi ya wapinzani wa CCM, vitendo ambavyo tunaamini vinafanywa kwa shinikizo la wanasiasa.

Itakumbukwa kwamba kwa muda mrefu tokea wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015 tumekuwa tukitoa tahadhari za kuwepo mipango ya kuwakamata viongozi wa CUF na wanaharakati wengine ili kufanikisha malengo ya kisiasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Tuna kila sababu ya kuamini kwamba hatua ya kumkamata Eddy Riyami na kumuweka ndani bila ya kumfikisha Mahkamani ni utekelezaji wa mipango hiyo. La si hivyo, ikiwa Eddy Riyami ametenda kosa basi angelishafikishwa Mahkamani ndani ya muda wa saa 24 tokea kukamatwa kama sheria inavyotaka.

Chama Cha Wananchi (CUF) kinalitaka Jeshi la Polisi kuacha kutumiwa na kutumika kisiasa kufanikisha malengo ya kisiasa ya CCM. Tunashangazwa kwamba siku zote wanaoitwa kuhojiwa, kukamatwa na kuwekwa ndani ni wanasiasa wa vyama vya upinzani na wanaharakati wengine lakini hatujawahi kushuhudia viongozi wa CCM kuitwa kuhojiwa, kukamatwa na kuwekwa ndani. CUF imetoa taarifa kadhaa kwa Jeshi la Polisi zinazohusu matamshi na vitendo vya viongozi wa CCM vyenye mwelekeo wa uhalifu lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. Hizo ni dalili za waziwazi za Polisi kutumiwa na kukubali kutumika kisiasa.

Tunalitaka Jeshi la Polisi iwapo kweli lina kesi dhidi ya Eddy Riyami basi limfikishe Mahkamani haraka ili hatua za kisheria zifuate mkondo wake. Na iwapo hawana kesi, basi wamwachie huru mara moja.

Umefika wakati wa Jeshi la Polisi kufanya kazi zake kitaalamu kama sheria na kanuni zao zinavyoagiza badala ya kuwatumikia wanasiasa wa CCM.

HAKI SAWA KWA WOTE

HAMAD MASOUD HAMAD
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO NA UMMA – CUF
fanyeni mpango hamasisheni wananchi wa zanzibar wasishiriki uchaguzi haramu...
 
Mkuu asante ntakwenda, ila kabla ya kwenda mm heb jarb nawe kujifikiria kama unapaswa kupima akili au laa? Maana cjaona hapo uhusika wa ccm,

Kwa mtazamo wangu mkuu kapime kwanza kisha njoo na majib, nami ntakwenda... ila cjapata mtu ambae anaweza kuhusianisha ccm na hlo tukio... Kapime akili mkubwa kunamahali unahisia mbaya....
yani me nvokusoma tu nikashindwa kukutofautisha na NGUCHIRO
 
Serikali ya Zanzibar waacheni CUF kwa amani...ushindi mmewapokonya jela mnawaswekea nini!?
 
Mkuu asante ntakwenda, ila kabla ya kwenda mm heb jarb nawe kujifikiria kama unapaswa kupima akili au laa? Maana cjaona hapo uhusika wa ccm,

Kwa mtazamo wangu mkuu kapime kwanza kisha njoo na majib, nami ntakwenda... ila cjapata mtu ambae anaweza kuhusianisha ccm na hlo tukio... Kapime akili mkubwa kunamahali unahisia mbaya....
Kutoona ndiyo tatizo la ubongo ulilonalo,mimi sina sababu ya kupima.kwakuwa "ratna"yangu iko safi na
 
kwanza tunashukuru kwa taarifa hui, maana wiki nzima ta Jana kulikuwa na uongo humu Eddy Kakamatwa na haijulikani alipo, Kulikuwa na Matako ya Eddy aachiwe Mara moja, kwa Maelezo yako Eddy kaingia Lockup Jana. Sasa tuelezeni sababu ya kukamatwa kwake kwa mujibu wa mahojiano
 
Hawatashiriki mkuu
itakuwa ni jambo la busara... kwanza sijaelewa ni wasimamizi gani ambao wamekubali kusimamia huo uchaguzi feki.... je kama hakuna wasimamizi utafanyikaje ? lkn kama ni kucheza mduara hiyo haina noma na wacheze tu
 
Mkuu asante ntakwenda, ila kabla ya kwenda mm heb jarb nawe kujifikiria kama unapaswa kupima akili au laa? Maana cjaona hapo uhusika wa ccm,

Kwa mtazamo wangu mkuu kapime kwanza kisha njoo na majib, nami ntakwenda... ila cjapata mtu ambae anaweza kuhusianisha ccm na hlo tukio... Kapime akili mkubwa kunamahali unahisia mbaya....

kawaida anaehitaji kwenda kupima akili huwa hajijui ...ila huyu aliekwambia ukapime akili hakukosea...
 
Inanikumbusha Stive Biko alivyokamatwa na kaburu same story...yataisha tuu hayo...
 
itakuwa ni jambo la busara... kwanza sijaelewa ni wasimamizi gani ambao wamekubali kusimamia huo uchaguzi feki.... je kama hakuna wasimamizi utafanyikaje ? lkn kama ni kucheza mduara hiyo haina noma na wacheze tu
Eu wamekata kuleta wasimamizi kwenye uchaguzi wa kichina
 
Una maansha uchaguzi ulifutwa kwa kufuata taratibu?
au ndo muhemko wa kisiasa humu JF?
Kwani Seif amepata wapi mamlaka ya kujitangaza kuwa ameshinda au amekuwa mgombea wakati huo huo mwenyekiti wa ZEC yaani Seif ni hybrid uh? kama Jecha hajafuata utaratibu nani amefuata hizo taratibu ? uchaguzi ni tarehe 20 ndugu, sidhani kama kuna other alternative zaidi ya kushiriki tu kikamilifu baada kuendekeza hisia.
 
Kwani umeambiwa wamelazimishwa ? hivi mnakaa angalau mkasoma vizuri ama kusikiliza hizi habari zinaporipotiwa? Jecha amewaambia hawajafuata taratibu na ndio maana akawambia tume inawatambua kama washiriki sasa si wafuate taratibu kesi ishe, ata kwenye upatu huwezi kuamka ukasema ati mimi najitoa kuna taratibu zake bhana kubwa..munaendekeza sana siasa za hisia kuliko uhalisia .
mnatafuta mteremko... habebwi mtu safari hii... mtajibeba wenyewe na nguchirrro zenu
 
CUF ........huku siyo kwenu ondokeni hatuwataki.Kama muna ubavu fanyeni chokochoko ndiyo mutajuwa maharagwe ni futari au mboga....Machotara ZNZ siyo kwenu.
 
mnatafuta mteremko... habebwi mtu safari hii... mtajibeba wenyewe na nguchirrro zenu
Kwani vipi umesikia kuna kiwete anataka msaada wa kubwebwa? mimi nadhani muache upofu kwanza ili muweze kudeal na fact, course hamjua nini mnataka watu nyie, mara mnajitoa mara mnakwenda mahakani mara mnataka mazungumzo mwisho mtataka kuvuliwa chup...
 
we unavojiona hapo unadhani unaweza kutembea bila kupakatwaaa?
 
Back
Top Bottom