CUF yasifu utendaji wa TAKUKURU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF yasifu utendaji wa TAKUKURU

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Jul 24, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeipongeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), kwa kuonyesha utendaji na uwepo wao hasa katika kufuatilia mchakato mzima wa uchaguzi kwa kuanzia kura za maoni zinazoendelea nchini na kuwakamata baadhi ya wagombea wakiwashawishi wachaguliwe kwa rushwa.

  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Naibu Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano wa CUF, Ashura Mustapha, ilieleza viongozi wengi wamekuwa wakijipatia nafasi mbalimbali za uongozi kwa njia isiyo halali, jambo linalosababisha utendaji wao kutokuwa makini kwa kuangalia masilahi yao zaidi na kutaka kurudisha viwango vya pesa walizotumia wakati wa mchakato wa kuchaguliwa.

  "Kama TAKUKURU itafanya kazi hii kwa uadilifu na uaminifu wa hali ya juu, itakuwa msaidizi mkubwa kwa Watanzania wengi ambao wamekuwa wakishawishiwa kuuza haki zao za kimsingi za kuchagua viongozi wenye uchungu na wenye moyo wa kuleta maendeleo kwa wanaowachagua na kwa masilahi ya nchi," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

  Aidha, chama hicho kimeitaka TAKUKURU ili kuhakikisha haki inatendeka, ifanye kazi bila kubagua chama wala wagombea na ijikite zaidi katika kufanikisha uchaguzi ulio huru na wa haki, ili kila mgombea achaguliwe kutokana na utendaji wake, uwezo na sifa ya kuwa kiongozi bora.

  Pamoja na hayo, chama hicho kimewaomba Watanzania wote watoe ushirikiano kwa kuwafichua hadharani wagombea wote wanaotaka uongozi kwa masilahi binafsi kwa kuwapa rushwa.

  Chanzo: Tanzania Daima


  My take:

  Hivi kweli Takukuru wako serious katika harakati hizi za kukimbizana na makada wa CCM, au wanafanya usanii tu – kwa njia ya kutumwagia vumbi? Mwisho wa siku hatutaona chochote kitakachotokea – hakuna atakayeenda jela -- na kwa hili niko tayari kupigwa risasi.

  Profesa wa CUF anawapongeza bure tu wasanii hawa. Kwanza haoni jinsi wanayofanya usanii kuhusu kukamatwa kwa wakwapuaji mabilioni katika Kagoda – au na hilo Profesa anawapongeza Takukuru?

  Tusisahau kwamba Profesa alikuwa mmoja wa viongozi wa vyama (the other was Augustine Mrema) waliomponda Mengi alipowataja mafisadi papa.
   
 2. telele

  telele Member

  #2
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo unawashauri wafanyaje sasa? come up with a solution or advice man! siyo kila siku kulaumu laumu tuu jamani.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wawe serious on more serious things that affect serious crimes committed by serious top cadres in the CCM government. Kama nilivyotaja wamekwepa kuwabana wezi wa Kagoda kwani Takukuru hawana ubavu wa kutimiza hilo -- wanakimbilia kukimbizana na sisimizi wa CCM, kitu ambacho narudia kusema ni kutumwagia vumbi la macho.

  Mimi na wapiganaji wengine humu ndani tutaendelea kulaumu jinsi nchi inavyoliwa na wajanja wachache huku Takukuru wako busy ku-chase red herrings (bad luck if you are ignorant of this phrase).

  Kipindi hiki cha mwaka wa uchaguzi ndiyo wajanja hupanga na kuliibia taifa mabilioni, wizi ambao utagundulika baada ya serikali kuapishwa. Nina hakika Takukuru hata hawafikirii kuangalia possibility hii -- wao na wagombea wa CCM tu!.
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Jul 24, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Jamani katika historia ya nchi hii mawaziri wamewahi kushtakiwa? Juzi tu kesi ya TTCL/TUCTA imefunguliwa dhidi ya watumishi waliokwapua TSh zaidi ya 4bn/- huku mambo ya Rada, Meremeta, EPA, nk yakiendelea kuchunguzwa!
  Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!
   
 5. T

  Taso JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Hiyo ndio pongezi?
   
 6. Jumboplate

  Jumboplate Senior Member

  #6
  Jul 26, 2010
  Joined: Jul 29, 2008
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
   
Loading...