PostGE2025 CUF yapinga Tume ya uchunguzi aliyoiteua Rais Samia, yadai kukosa uhuru na uaminifu

PostGE2025 CUF yapinga Tume ya uchunguzi aliyoiteua Rais Samia, yadai kukosa uhuru na uaminifu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
THE CIVIC UNITED FRONT (CUF- Chama Cha Wananchi)

MSIMAMO WA CUF JUU YA TUME YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA DKT SAMIA SULUHU HASSAN:

CUF- Chama Cha Wananchi kulikuwa Chama na Taasisi ya kwanza nchini kutoka hadharani na kutoa wito kwa Jumuiya za Kimataifa na za Kikanda kushiniza kufanyika kwa uchunguzi huru wa mauaji, uvunjaji wa haki za binadamu, uharibifu wa mali na uhalifu wa uchaguzi. Wito huo ni moja miongoni mwa mengi yaliyobebwa na TAMKO la Chama lililotolewa na Mwenyekiti wa Chama Taifa Prof. Ibrahim Haruna Lipumba Novemba 5, 2025.

Matarajio ya CUF- Chama Cha Wananchi ni kushuhudia kuundwa kwa Chombo huru kitakachojumuisha Wawakilishi kutokaTaasisi za Kimataifa zinazohusika na Haki za Binadamu na Utawala Bora, Asasi za Kiraia zilizo huru na Majaji wenye rekodi ya kuaminika ambao wanaweza kusimamia haki bila kujichagulia upande.

Tumeshuhudia Uteuzi uliofanywa na Dkt Samia Suluhu Hassan wa Wajumbe wa kilichoitwa "Tume huru ya Kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025". Kwa kiwango kikubwa wajumbe wa Tume hiyo ni watanzania waliokuwa wateule wa Rais katika awamu mbalimbali, miongoni mwao wakiwa ni wanachama wa CCM. Kwa kuzingatia ukweli huo, Tume iliyoundwa inakosa sifa ya kuaminika kufanya Uchunguzi huru wenye matokeo ya kuaminika na makundi yote yaliyoathirika kwa namna tofauti.

CUF- Chama Cha Wananchi kinatahadharisha kwamba suala la kuwa na Tume huru ya Uchunguzi lisichukuliwe kwa uzito mwepesi na wala mzaha usipewe nafasi. Watu wengi wamepoteza maisha, watu wengi wamepoteza ndugu zao, uharibifu mkubwa wa mali za Umma na za binafsi umetokea na Uchaguzi umevurugwa na kupelekea matokeo kukosa uhalali na kuaminika. Tume inayopaswa kuchunguza matukio haya inapaswa kuwa huru na kuaminika ndani na nje ya nchi, kama kweli tuna lengo la kuliponya Taifa.

HAKI SAWA KWA WOTE!


Eng. Mohamed Ngulangwa
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF- Chama Cha Wananchi
Novemba 19, 2025

Pia Soma: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025
 
Na nyinyi ni wanafiki tu. Wakati wa huo uchaguzi feki, mlishirikiana nao na kuwapongeza kwa ushindi wao feki wa kupika matokeo! Halafu leo mnajifanya eti kutoa tamko! Pumbavu zenu.
 
Kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni. Hasira na chuki za wengine kwa maneno yasiyo na staha ni jambo la ajabu na kituko.
 
Back
Top Bottom