CUF wapeleka barua Ikulu ya kuonana na Rais

February

Member
Nov 15, 2011
90
21
Chama cha wananchi cuf kimemwandikia barua rais kuomba kukutana nae kutoa maoni kuhusu muswada na mchakato wa katiba mpya. Hiyo ndio taarifa iliyopatikana jioni hii ikulu
 
Nacho CUF kimeomba kukutana na JK kuhsu Katiba. Wamekubaliwa na maandalizi yanafanywa.

Chanzo Ch10 bulletin 7.00pm
 
Kweli cdm ndo wanaöngoza nchi,walisema tutaleta katiba mpya, ccm wakadakia!!! Wameomba kuonana na rais cuf nao wamedakia wanataka!!sasa kwann nyie cuf msiungane na cdm?shame on you
 
Chama cha wananchi cuf kimemwandikia barua rais kuomba kukutana nae kutoa maoni kuhusu muswada na mchakato wa katiba mpya. Hiyo ndio taarifa iliyopatikana jioni hii ikulu
kugeza ruksa tu!
 
Hatimae CUF nao wamefuata nyayo za chama kikuu cha upinzani Tanzani CHADEMA. Nao wanahitaji kuonana na Rais ambapo leo wamepeleka barua yao. Rais kasema ratiba ya kuonana nao ipangwe haraka iwezekanavyo.source ch10. Mia
 
CUF na wao si wapo Ikulu? Kila siku si wanaonana na raisi sasa wanataka kuonana nae kvp?
 
Sasa hawa ni fujo tu. Si waliiuafiki Muswada Bungeni? Wanataka wamwambie nini tena?
Pengine wanataka kumwambia JK asiwasikilize CDM ni wakorofi tu. nadhani ni hiyo tu!

Hapana. Hii request imezuka leo tu na hasa chimbuko lake ni CUF Zanzibar. Wanataka kumwambia JK kwamba kwanza Muungano uvunjwe.
 
chadema walitaka kunyang'anya mume wa CUF pasipo kufuata utaratibu. Utaingiaje nyumbani wa CCM bila CUF kuwepo? uliwahi kuona wapi mnamtembelea mtu halafu unasema mke wako nisimkute nyumbani kwako. Hapa Jf wanachadema ndio wanasema kuna ndoa kati ya CCM na CUF. Nini cha ajabu kama CUF wameomba kukutana na Rais
 
tuache ushabiki wa kisiasa CUF ni chama cha siasa kinachowakilisha wananchi kina haki ya kumuona Rais kama ilivyo chadema na wadau wengine wote
 
CUF wazidi kudidimia kweli! sasa hii tena nini, na hali waliuafiki muswada bungeni 100% na kuwalaani CDM? Kipi kipya wanacho tena?
 
Hii ni aibu kweli. Uamuzi wa cdm na cuf unamjenga jkbila sababu. Yani kama watoto wanamlilia vile baba. Shame
 
hoja sio ombi la CUF kuonana la Rais hoja ni nini wanakwenda kuzungumza na Rais. Kama wanakwenda kumuuliza rais kwa nini ulikutana na chadema ni kosa lakini kama wanakwenda kujenga hoja kwa ajili ya maslahi yetu wote hakuna tatizo
 
kama CUF si chama cha siasa basi kwanza kifutwe kwa msajili vinginevyo kina haki ya kwenda Ikulu
 
CUF wazidi kudidimia kweli! sasa hii tena nini, na hali waliuafiki muswada bungeni 100% na kuwalaani CDM? Kipi kipya wanacho tena?


Hata CUF kuonana na rais mnaona wivu aise mapenzi mapya matamu..

CUF wanawakilisha wananchi wanaweza kuonana na rais bila tatizo..of course wameiga
 
Hakuna tatizo cf kuonana na rais ila kwa issue ya katiba c waliiunga mkono? cf bara wawe makini na cf zanzibar. cf zanzibar wanashinikiza mambo ambayo yanaua cf bara na kupoteza umaarufu kwa tz bara. Cf ijiandae kubaki chama cha pemba.
 
Back
Top Bottom