CUF wapeleka barua Ikulu ya kuonana na Rais

Kwel chadema ni chama makin,,ona wanaiga kila kona...sioni watu wa kujenga hoja hapo cuf.....
 
yamekuwa haya tena? wanataka wakamwone wakati wao lao moja? hivi kafu si ni ccm B?
 
Ni janja ya watu wa UWT kutaka kuwaaminisha watu kuwa si mapendekezo ya CDM tu yaliyokatakiwa bali hata CUF. Ni mbinu ya kitoto sana kama wanayoitumia UVCCM kutaka nao kuandamana kila CDM au BAVICHA wakitaka kuandamana ili wote wakataliwe halafu UVCCM kuwacheka pembeni.
CCM na CUF ni kama yule mwanamke muovu aliyemwambia nabii Selemani kugawane mtoto lakini yule mwenye mtoto akasema ikiwa ni hivyo basi mpe tu mwenzangu kuliko kugawana. Ndipo nabii Selemani akajua yupi aliye mzazi, na ndipo wananchi watakapojua yupi ana uchungu na katiba ya ukweli.
 
Mkuu CUF nacho ni chama cha siasa kama CDM nao wana haki ya kuonana na Mkuu wa Nchi kama walivyofanya CHADEMA. TLP, UPDP, DP, UDP, Demokrasia Makini, NCCR Mageuzi, n.k nao wana haki ya kuandika barua na kutaka kuonana na Mkuu wa nchi kama ilivyofanya CHADEMA. Na hata CCM pia inaweza kutaka kuonana na Mkuu wa Nchi huko Ikulu ili kueleza yaliyo moyoni kwa kuwa nacho ni Chama cha siasa. Kuonana na Rais Ikulu si haki ya chama kimoja tu!

Wanaenda kufanya nini huko? wenzao wameambulia juice tu. Au ndo mkakati bei nafuu walioona unaweza kupunguza safari za nje za JK? akitoka caf nafikiri ataenda mzee wa TLP. Lakini mzuka wa kupanda ndege mzee ukimpanda nafikiri atawaacha sebleni wakikodoa macho.
 
cuf mnatakiwa kuwa wapole ili ndoa yenu Idumu,nyie ndoa na iheshimiwe,wapembeni hatutaki kusikia chokochoko na huyo kidume chako,we ushaolewa so kuwa mpole.:A S 465:
 
Wanaenda kufanya nini huko? wenzao wameambulia juice tu. Au ndo mkakati bei nafuu walioona unaweza kupunguza safari za nje za JK? akitoka caf nafikiri ataenda mzee wa TLP. Lakini mzuka wa kupanda ndege mzee ukimpanda nafikiri atawaacha sebleni wakikodoa macho.


Mkuu hujui kwamba ikulu ni patamu kila mtu anapataka. Hukuona Makamanda walivyofika na kuchekelea kisha wakaondoka na makubaliano mawili tu baada ya kunywa chai na kahawa kwa siku mbili mfululizo ndani ya jumba jeupe!
 
Chama cha wananchi cuf kimemwandikia barua rais kuomba kukutana nae kutoa maoni kuhusu muswada na mchakato wa katiba mpya. Hiyo ndio taarifa iliyopatikana jioni hii ikulu

nao CUF na CCM wamezidi kudesa kila kitu kutoka chadema, sijui hawana planners kwenye chama.
 
Jamani msitake kuandika vitu ili kufurahisha baraza.. CUF wapeleke maombi ya kuzungumzia muswada wakati imeshakua sheria? mbona CUF walishawakilisha maombi yao toka mwaka jana baada ya uchaguzi! hizi habari ni uongo na hazina mshiko isipokuwa nawapeni hongera na tujifurahishe na ktk picha..

Hapa Pinda anaonekana kisha kolea na mzee wa kushoto pembeni anamcheki jinsi ulabu unavyompeleka na Bilal hana mbavu..
2+(2).jpg
 
chadema wanafanya yale yale waliokuwa wanalilia kwamba ccm wanataka kuhodhi mchakato wa katiba mpya, sasa na wao wanasema CUF wasionane na Rais kwa kuwa watakuwa wanawageza chadema
 
Tangu bungeni Chadema na CUF wanatokea milango tofauti vivyo hivyo hawawezi kuingia lango la Ikulu pamoja.
 
inauma kuona mme kaingia chumbani na mtu mwingine ambaye ni mpinzani wako...lazima ufuatilie ujue kinachooendelea nini.
 
CUF wameunga mkono muswada tena kwa kelele na sasa muswada umesainiwa na rais hivyo kuwa sheria. Sasa CUF wanaenda kuonana na rais kwa lipi? Walichokita kimefanyika wanataka nini tena? Na kama CHADEMA hawakuomba kuonana na rais CUF walikuwa na mpango gani? walipanga kuonana na rais? Kwa nini hiki chama (CUF) kimeamua kuwa dalali wa ugomvi?
 
Chama kisichoendeshwa na wasomi ni tatizo tu,si juz tu bungeni waliupitisha tena kwa mbwembwe au wanatak wakanywe juice ikulu?au wanadhan CDM wanataka kuwaharibia ndoa yao.
 
chadema walitoa tamko kwamba hawataki kuongozana na vyama vingine kwenda Ikulu kwa sababu eti wao walituma barua lakini pia vyama vingine vilishiriki kupitisha muswada ikiwemo CUF sasa CUF wanakwenda kivyao tunasema wasienda huu ni unafiki. kama chadema wangekaribisha vyama vingine kwenda Ikulu tungesema CUF wanafiki. tuwaache waende kivyao vyao
 
Mie sioni shida japokuwa ni janja ya UWT but KAFU ni watu kwa mujibu wa Katiba lakini Chama chao hakipo kwenye watu waacheni waende
 
tatizo letu tuna haraka CUF hawajasema wanakwenda kuongelea katiba wamesema tu wameandika barua kwenda kumuona Rais kwa nini bado hatujui. hakuna anayejua kinachowapeleka kwa nini tunawahukumu? pengine agenda yao ni tofauti na ile chadema nani anajua hilo?
 
Back
Top Bottom