Mpita Njia
Platinum Member
- Mar 3, 2008
- 6,999
- 1,189
Ni sawa kabisa huyo mchina alikuwa afike Zanzibar kama sehemu ya Kuu ya Muungano wa Tanzania bila ya Zanzibar hakuna Muungano
Mkuu kifupi tumejifunga wenyewe.. Tanzania ina ma RAIS wawili hivyo figure out! ukianza na hapo tu utaona makosa mengi sana ambayo bara tunajaribu kuyajengea hoja...Naomba kufahamishwa. Hivi Tanzania kuna dola mbili (Zanzibar na Muungano)? Mimi siku zote nilidhani tuna dola moja katika serikali mbili.
Wewe Mwiba wewe! nani kakudanganyeni kuwa kuna Tanganyika na Zanzibar. Nchi ni moja tu, Tanzania. Usijidanganye eti Zanzibar ikiondoka hakuna Muungano, ni sawa na kusema eti ukucha ukiondoka basi mwili haupo, ukucha ndio cha kwenda kuozea mbali na kuuacha mwaili kama kawa.
Kama nyie mnajitambua kama nchi basi muwe mnawalika hao na kuwapangia safari zao kuanzia makunduchi na kuishia sijui kibanda maiti!!
Kaizer,
Mkuu sasa nawe unapotosha hoja.. Hapa kinachozungumzwa ni JinTao kutembelea Zanzibar sio swala la CCM wala CUF isipokuwa walio raise hoja ni CUF..
Kama issue ya Chadema na swala la EPA inawezekana kabisa kuna watu wanachama wa Chadema wanafanya kazi BoT..
Wakitaka wao kumkaribisha Jin tao mtawambia ni swala la Muungano...wakati Tanzania ina ma RAIS wawili sasa nambieni kwa nini Zanzibar sio nchi!.
Kama hii ndo CUF, basi hawana sera, na Kura yangu hawapati ng'o, labda wajirekebishe na waachane na mambo ya kipuuzi. Huu ni ujinga mtupu.
Halafu eti mnasema CUF ni chama muwafalka kushika madaraka. Mnaona utumbo huo. Bimani ana hoja za katika vijiwe vya kahawa na vigogo vya karata. Kwa kweli hiyo ni aibu kwa CUF.
Wewe Mwiba wewe! nani kakudanganyeni kuwa kuna Tanganyika na Zanzibar. Nchi ni moja tu, Tanzania. Usijidanganye eti Zanzibar ikiondoka hakuna Muungano, ni sawa na kusema eti ukucha ukiondoka basi mwili haupo, ukucha ndio cha kwenda kuozea mbali na kuuacha mwaili kama kawa.
Kama nyie mnajitambua kama nchi basi muwe mnawalika hao na kuwapangia safari zao kuanzia makunduchi na kuishia sijui kibanda maiti!
Mie sioni hata kinachodaiwa na wanzibar! kwanini msiachiwe tu mkaenda zenu? tumewabeba hadi sasa naona inatosha, kuwalipia kuanzia mishahara kumipatieni ajira zikiwepo za nafasi 50 za wabunge, shule n.k wakati siye kwenu hatuji. Mie nimechoka!
Visiwani kwanza punguzeni kulia lia kama mtoto mdogo ktk kila jambo!
Nilidhani sasa mlishakuwa watoto wakubwa!
Kumbe bado!
Naomba kufahamishwa. Hivi Tanzania kuna dola mbili (Zanzibar na Muungano)? Mimi siku zote nilidhani tuna dola moja katika serikali mbili.
Sijui kama Pres. Hu alikuwa na lolote la kutembelea Zanzibar. Nijuavyo, Marais wa nchi zilizochangamka, hawawezi kwenda mahali ili kufurahisha baadhi ya watu. Nadhani hufanya hivyo kwa kuzingatia umuhimu wa ziara hizo. Vile vile, sina uhakika kama kuliko=uwa na mwaliko maalumu kutoka kwa Rais wa Zanzibar kwa marais hao watatu ambao CUF wanalaumu kutofika kwao Zanzibar.