CUF wamtaka Jintao Z'Bar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF wamtaka Jintao Z'Bar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpita Njia, Feb 16, 2009.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Februari 16, 2009

  “Serikali ya Muungano ina dhamira gani kwa Zanzibar”


  Wapendwa Wanahabari,

  Wakati Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Hu Jintao, akimaliza ziara yake ya siku tatu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sisi Chama cha Wananchi (CUF), kwa niaba ya Watanzania wanaopendelea Muungano udumu katika misingi ya uadilifu na usawa, tumesikitishwa na kuondoka kwa Rais huyo bila ya kwenda Zanzibar.

  Ambapo tukio hili linaweza kuonekana la kawaida tu katika macho yasiyoona mbali, katika duru za kisiasa na kidiplomasia ni pigo kubwa kwa dhamira ya Muungano wa dola mbili za Tanganyika na Zanzibar na dalili kwamba ile khofu waliyokuwanayo Wazanzibari kwa siku nyingi sana, sasa inazidi kuwa kweli. Khofu hiyo ni kwamba Serikali ya Muungano haina dhamira njema kwa hadhi na heshima ya Zanzibar katika uso wa dunia na kwamba inafanya kila lililo ndani ya uwezo wake ili Zanzibar iendelee kusahaulika duniani.

  Wapendwa Wanahabari,

  Itakumbukwa kwamba uhusiano baina ya Zanzibar na China ni mkubwa na wa muda mrefu zaidi kutokana na historia ya kudai uhuru na Mapinduzi ya 1964. China ilikuwa katika nchi za mwanzo mwanzo kuyatambua Mapinduzi ya Zanzibar kabla ya hata baadhi ya majirani wa Zanzibar hawajafanya hivyo, na pia kufunguwa ubalozi wake Zanzibar. Tangu wakati huo, serikali za China na Zanzibar zimekuwa na uhusiano na ushirikiano wa karibu sana. Kwa hivyo, ni jambo la kusikitisha, kushangaza na kutia khofu kwamba Rais wa Jamhuri hiyo anakuja nchini Tanzania, lakini hapangiwi kwenda Zanzibar, ambako kuna mizizi mirefu ya kimahusiano baina ya nchi hizo.

  Wapendwa Wanahabari,

  Huu ni mfano mmoja tu kati ya mifano ya hivi karibuni – hasa tangu kuingia madarakani kwa Rais Jakaya Kikwete – inayoonesha khitilafu katika dhamira ya Muungano panapohusika uwanja wa diplomasia na siasa na kimataifa. Mwaka jana alikuja nchini Rais wa Jamhuri ya Watu wa Komoro, Mhe. Mohammed Sambi, lakini naye pia hakupangiwa kwenda Zanzibar. Rais George Bush pia wa Marekani alikuja Tanzania na kukaa zaidi ya siku nne lakini pia hakupelekwa Zanzibar. Mahusiano baina ya Komoro na Zanzibar ni makubwa na ya karne nyingi na mahusiano kati ya Zanzibar na Marekani yanarudi nyuma tangu mwaka 1833 kwa kufunguliwa ubalozi rasmi wa Marekani mjini Zanzibar. Si stahiki hata kidogo ukweli huu kupuuziwa kwa makusudi katika uwanja wa siasa za kimataifa na kidiplomasia.

  Wapendwa Wanahabari,

  Sisi, CUF, tunasimamia imani kwamba Muungano huu ni baina ya dola mbili huru na zilizokasimu sehemu ya madaraka yake kwa serikali moja kuu, lakini wakati huo huo zikibakia na utambulisho wake ambao lazima utambuliwe na uheshimiwe. Kwa hivyo, tunachukulia vitendo kama hivi kama jitihada za makusudi za ‘kuifanya’ jumuiya ya kimataifa isahau uwepo na hadhi ya Zanzibar. Tunatarajia wapangaji wa protokali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watazifanya ziara zijazo za wakuu wa nchi na au za wale wa taasisi ya kimataifa kuzingatia ukweli huo.


  Imetolewa na  Salim Bimani,

  Naibu Mkurugenzi,

  Haki za Binaadamu na Mahusiano ya Umma,

  The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi)

  Party Headquarters

  P.O. Box 3637

  Zanzibar
  Tanzania Tel: +255 777 414 112/414 100

  cufhabari@yahoo.com

  Weblog: Haki na Umma

  Website: Kuhusu CUF
   
 2. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2009
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,603
  Likes Received: 6,770
  Trophy Points: 280
  Kama hii ndo CUF, basi hawana sera, na Kura yangu hawapati ng'o, labda wajirekebishe na waachane na mambo ya kipuuzi. Huu ni ujinga mtupu.
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni sawa kabisa huyo mchina alikuwa afike Zanzibar kama sehemu ya Kuu ya Muungano wa Tanzania bila ya Zanzibar hakuna Muungano hivyo tunahesabu alikuja kutembea Tanzania ,halafu kisiasa ni bora kabisa kwani serikali iliyokuwepo ni lazima iwekwe kwenye matatizo kwa muda wote ,na kila siku huwa nasema hata Serikali ikifanya jambo jema basi ni lazima upande wa upinzani waweke doa japo la kubambikiza yaani unachomekea humo humo alimradi kuiweka serikali bize na hilo CUF wameanza kulitekeleza yale mambo ya kusifia Chama na serikali yake iliyopo madarakani yamepitwa na wakati ,maana tukianza kusifiana kutakuwa hakuna upinzani ,kuwepo upinzani ni kuikanyaga na kuikurupusha serikali maana hata jeshini kuna taratibu za kuwakurupusha makuruti hata kama hakuna vita ,alimradi wakati upo kwenye maisha ya kambi za jeshi unatakiwa usiwe na raha mpaka unamaliza ,na ndio hivyo kwa serikali iliyopo madarakani ile kukosa la kulifanya na kulipatia utatuzi ndio maana ikawa wanaiibia serikali.eti jamani hawana la kufanya kama hawakuibia serikali wapange nini ?

  Hivyo upinzani unatakiwa usiwape walioko madarakani nafasi ya kupanga mahesabu na kukwiba lazima wakurupushwe ,muda wa wao kukwiba usiwepo kabisa ,hizi purukushani zinazokwqenda sasa hivi zinasaidia sana maana wote wahoi bin taaban hawajui ni lini wapi na saa gani litawazukia la kuwazukia.
   
 4. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Wewe Mwiba wewe! nani kakudanganyeni kuwa kuna Tanganyika na Zanzibar. Nchi ni moja tu, Tanzania. Usijidanganye eti Zanzibar ikiondoka hakuna Muungano, ni sawa na kusema eti ukucha ukiondoka basi mwili haupo, ukucha ndio cha kwenda kuozea mbali na kuuacha mwaili kama kawa.

  Kama nyie mnajitambua kama nchi basi muwe mnawalika hao na kuwapangia safari zao kuanzia makunduchi na kuishia sijui kibanda maiti!

  Mie sioni hata kinachodaiwa na wanzibar! kwanini msiachiwe tu mkaenda zenu? tumewabeba hadi sasa naona inatosha, kuwalipia kuanzia mishahara kumipatieni ajira zikiwepo za nafasi 50 za wabunge, shule n.k wakati siye kwenu hatuji. Mie nimechoka!
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Visiwani kwanza punguzeni kulia lia kama mtoto mdogo ktk kila jambo!

  Nilidhani sasa mlishakuwa watoto wakubwa!

  Kumbe bado!
   
 6. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Naomba kufahamishwa. Hivi Tanzania kuna dola mbili (Zanzibar na Muungano)? Mimi siku zote nilidhani tuna dola moja katika serikali mbili.

  Sijui kama Pres. Hu alikuwa na lolote la kutembelea Zanzibar. Nijuavyo, Marais wa nchi zilizochangamka, hawawezi kwenda mahali ili kufurahisha baadhi ya watu. Nadhani hufanya hivyo kwa kuzingatia umuhimu wa ziara hizo. Vile vile, sina uhakika kama kuliko=uwa na mwaliko maalumu kutoka kwa Rais wa Zanzibar kwa marais hao watatu ambao CUF wanalaumu kutofika kwao Zanzibar.
   
 7. epigenetics

  epigenetics JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2009
  Joined: May 25, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Je, Serikali ya Tanzania ina tamko gani kupanga ratiba ya ugeni wa kiongozi wa kimataifa? Rais wa China anakuja na schedule yake, na sidhani ya kwamba raisi wa nchi yetu anaweza kumpangia rais wa China ni sehemu gani za nchi afanye ziara. Kama hamna projects zenye umuhimu kwao hawatatembelea sehemu hiyo ya nchi.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Feb 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Recta,
  Mkuu kifupi tumejifunga wenyewe.. Tanzania ina ma RAIS wawili hivyo figure out! ukianza na hapo tu utaona makosa mengi sana ambayo bara tunajaribu kuyajengea hoja...
   
 9. k

  kananyayo Member

  #9
  Feb 16, 2009
  Joined: Dec 15, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani Makamu wa Rais ambaye maalum kutoka Visiwani hakuwepo kati ya viongozi waliomlaki na kuzungumza na Rais huyo wa China. Haya mambo hayaendi kwa nusu-kwa nusu yakheee
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ndio hapo maana mwili bila ya ukucha kutakuwa na kasoro na huwezi kuita mwili ,umewahi kusikia mbuzi kasoro mkia ,ina maana si mbuzi huyo bali angekuwa na mkia ndio angekuwa mbuzi. Ndio hivyo hivyo bila ya Zanzibar hakuna Tanzania. Yaani tutawaita Tanzania kasoro Zanzibar ndio maana yake.

  Yaani japo watu hawautaki muungano bado mnang'ang'ania wezi wakubwa,karibu chaka lenu litafyekwa.
   
 11. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Halafu eti mnasema CUF ni chama muwafalka kushika madaraka. Mnaona utumbo huo. Bimani ana hoja za katika vijiwe vya kahawa na vigogo vya karata. Kwa kweli hiyo ni aibu kwa CUF.
   
 12. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,497
  Trophy Points: 280
  Hivi jamani hawa CUF wanaoperate vipi?

  On one side, wana CUF wanalalamika kuwa Hu JIn nTao hajaenda Zanzibar

  On the other side, Mwenyekiti wao Profesa Lipumba anaonekana ikulu akipeana mikono na HU Jin Tao kwenye hafla ya kitaifa

  Hikichama kinaendeshwaje? nacho kina mamlaka mbili?

  [​IMG]

  Picha kwa hisani kubwa kabisa ya MICHUZI blog
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Feb 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kaizer,
  Mkuu sasa nawe unapotosha hoja.. Hapa kinachozungumzwa ni JinTao kutembelea Zanzibar sio swala la CCM wala CUF isipokuwa walio raise hoja ni CUF..
  Kama issue ya Chadema na swala la EPA inawezekana kabisa kuna watu wanachama wa Chadema wanafanya kazi BoT..
  Wakitaka wao kumkaribisha Jin tao mtawambia ni swala la Muungano...wakati Tanzania ina ma RAIS wawili sasa nambieni kwa nini Zanzibar sio nchi!.
   
 14. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,497
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mkandara,

  heshima mbele mkuu labd ahujanifahamu vizzuri hoja yangu,

  Ninachomaanisha hapo ni kuwa iweje,, chama kitoe tamko 'kali' kulaani kitendo cha serikali kutompeleka Hu Jin Tao huko zenji, lakini nikadhani pia wangesusia na mwaliko waliopewa wa kushiriki kwenye hafla ikulu kama picha inavomwonyesha Prof Lipumba akiwa ikulu na JK na Hu jin Tao.

  je, Lipumba alijua kuhusu hili tamko? mbona kama linapingana na what they do in practice?

  plus, kuna wakati pia marais/viongozi wanakuja wanaextend hadi Zanzibar na wanakaa na rais ikulu, lakini haina maana kila rais anayekuja basi afike zanzibar, nadhani inategemea pia anaenda kule kufanya nini kimaslahi ya taifa kama tanzania mkuu au sio?

  Hoja ya zanzibar kuwa nchi au sio nchi nadhani ishajadiliwa hapa na mkulu JK alisema kuwa kwa mambo ya nje Zanzibar SIO nchi,, sasa hili walitaka liweje wakati mgeni ni wa Tanzania na sio 'nchi' inayoitwa Zanzibar kwenye anga za kimataifa?

  I mean, CUF hoja inaweza ikawa ni hii tu? au ni tu$20 na ushee? Mimi nadhani wamhoji JK kwa nini hadi leo tunaendelea kuomba omba
   
 15. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Upi ujinga huo wa CUF kumtaka Rais wa China aende Zanzibar au huu wa wewe kutishia kutotowa kura yako?
  Kwa upande wangu sioni baya hapa hasa tukitilia maanani malumbano ya nchi au si nchi. Pengine ile kwenda Zanzibar na akapokewa kwa heshima sawa na Tanganyika ndiyo inayotaka kuondoshwa kwani hicho kilikuwa kigezo kikubwa kuwa Zanzibar ni nchi.
   
 16. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  kweli hivi Karume akikutana na Hu Dar haitoshi kama ratiba iko taiti?

  Ni lazima Hu aende Visiwani physically?

  Kaazi kweli kweli!!!
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ajabu unauza Uzanzibari wako kwa chuki ya CUF. AMka we Mzanzibari hiyo ni mikakati ya kuzidi kukushindilia. Masikini Wazanzibari wa kina Pakacha. Eti CUF si Chama ni nini mbona mnatumia muda wote kupanga njama dhidi yake?
   
 18. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Pole ndugu! Zanzibar ilikuwepo kabla ya Muungano na haikutetereka kiuchumi kama ilivyo sasa katika Muungano. Kama fikira zako kuwa Zanzibar ikiachwa kwenye Muungano itathirika chembelecho Dr Salmin YAGUJU. Kwani huu Muungano unawafanyia nini Wazanzibari wa kuwa wategemezi? Fedha mnazokusanya haziendi Zanzibar na huduma kama umeme ni biashara, sasa kipi cha kusema kuwa ukivunjika Muungano Zanzibar itaumia. Ukivunjika Nuungano wataumia viongozi wa CCM kule Zanzibar ambako mnapeleka pesa kwao ili wanganganie na kukubali muundo wa Muungano usiotowa usawa.
   
 19. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Tungeacha sisi kwanza kulialia na ufisadi. Kama kurejea kupigania haki ni utoto basi na sie ni mitoto mikubwa tunaolilia na ufisadi. Hili unalosema wewe ni sawa na mkuki kwa nguruwe. Hebu tuache kuwabana ili tuone hawatakuwa? Sisi wenyew hatukuwi na kila siku tunatafutia dawa kero za Muungano tangu wakati wa Nyerere hadi huu wa JK. Tuwpe haki ili wasilalamike.
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Pengine ungeeleweshwa kuwa Zanzibar kama dola haijawahi kutowa mualiko kwa Rais yoyote uliesikia ameenda Zanzibar. Utaratibu wa Marais kwenda Zanzibar ulikuwa ni utaratibu wa kawaida kabla ya Zanzibar kudai kuwa ni nchi kamili. Kinachofanyika sasa ni kuondowa ile dhana ya kuonekana kuwa Rais anakwenda kule na kupokewa kama nchi nyengine. Iwapo kulikuwa na utaratibu basi si vizuri kuuondowa kwa nguvu ya upande mmoja tu kwani Muungano ni ridhaa ya sehemu mbili, sasa iwapo mmoja anajichukulia madaraka ya kila uamuzi ndiko kulikotupeleka tulipo kwenye Muungano wetu.
   
Loading...