Mkuu Ngekewa nimejaribu kusoma hapo juu, nimeshindwa kuelewa. Nilidhani mada iliyopo hapa ni kwanini Hu Jintao hakwenda Zanzibar na Wazanzibar wanaona sio fair. Sasa hili la mafisadi linahusika vipi ndugu yangu?
Mkuu mwenzangu kama utafatilia quote utaona kuwa mtu amegeneralize kuwa Wazanzibari wanapenda kulialia akimaanisha kuwa wao wanalalamika. Sasa nikujuvye kuwa hao Wazenji wanalalamika kwasababu kuna mambo yanayowakera na kila yakirejewa basi hawatoacha kulalamika kama sisi huku Mrima tunavyokerwa na ufisadi na kila mara hatuachi kulalamika nao na ndio maana nikasema kudai haki mtu hachoki na kama huku Bara kunavyochukuliwa hatuwa zidi ya ufisadi kwa kilio chetu cha kila siku pengine huku kulialia kwao kutawafanya muwape haki zao. usipofahamu nipo.