Elections 2010 CUF waiponda Chadema Live Mlimani TV

Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
284
Viongozi wa CUFwako live Mlimani tv. Moja kati ya mambo mazito waliyosema dhidi ya Chadema ni
1. Chadema kwenda kujaribu kumshawishi Hamad Rashid Hamad kujiunga na Chadema ili apewe ugombea mwenza wa Urais.
2. Chadema hawakujiandaa kugombea Urais, kwani hata Dr. Slaa hakujua kwamba anahitajika kugombea Urais. Yeye alikuwa tayari anajiandaa kugombea ubunge Karatu
 
viongozi wa CUFwako live mlimani tv. Moja kati ya mambo mazito waliyosema dhidi ya Chadema ni 1. Chadema kwenda kujaribu kumshawishi Hamad Rashid Hamad kujiunga na Chadema ili apewe ugombea mwenza wa Urais. 2. Chadema hawakujiandaa kugombea Urais, kwani hata Dr. Slaa hakujua kwamba anahitajika kugombea Urais. Yeye alikuwa tayari anajiandaa kugombea ubunge karatu

Who Knows, Labda ilikuwa ni Strategy. Na hata hivyo sijaona kuna kuponda hapo labda kama wewe unataka kuwaponda CHADEMA.
 
Hivi huyu Lipumba amegombea Urais mara ngapi vile? Na katika mara zote hizo mbona hakuwahi kuzikonga nyoyo za Watanzania na kuvuta umati wa watu kila alipopita kama inavyotokea kwa Rais wetu mtarajiwa Dr Slaa? Hana jipya huyu! Mpigie kura Dr Slaa na mbunge/diwani wa chadema.
 
Ingelikuwa Invisible hajasema tusiandike PUMBA basi leo hii ningeliandika.

Ila kwa sababu hiyo, ngoja nijizuie.

Kichwa cha habari na habari yenyewe haziendani.
 
hakijazungumzwa kitu hicho wewe, wewe ndio unayezungumza, Prof. is out of that
 
mawazo yangu tu; hivi ingekuwa hakuna CCM na CHADAMU wangekuwa wanaongozanchi hii, kungekuwa na upinzani kweli? kuna kila ushahidi CHADAMU ni chama kisicho himili usindani wa kisiasa wala hakina uvumilivu kwa wanaopinga mawazo yao, sijui demokrasia ya kweli ina maana gani kwa wenzetu?
 
Sikonge ungekuwa unaangalia hicho kipindi nafikiri ungeelewa huko kuponda. Mimi nimeandika issue iliyozua lugha za kashfa na kebehi dhidi ya Chadema. Au ulitaka niandike hayo maneno ya kashfa waliyoyazungumza? Wengine ni wastaarabu hatuandiki matusi hata kama yamesemwa na mtu mwingine!
 
sijatazama tv mlimani lakini katika kipindi chake cha mahojiano itv prof amesema yeye kama atalinganishwa na slaa basi slaa ni kichuguu na yeye ni mlima kilimanjaro. nadhani anachokisema ni kweli kutokana na uwezo wake wa kuchanganua mambo bila uzushi ama kupika data ili kujidanganya mwenyewe na wananchi udhaifu alionao Slaa
 
hakijazungumzwa kitu hicho wewe, wewe ndio unayezungumza, Prof. is out of that
Mkuu hayo yamesemwa kwenye kipindi kilichorushwa live na mlimani tv, kimeisha saa 4 kamili usiku wa leo. Cuf iliwakilishwa na viongozi waandamizi 3!
 
Hiki ni kipindi cha kampeni jamani, unatakiwa uangalie mapungufu ya mwenzio na uyafanye ndio mtaji wako, sasa unachotaka kusikia nisifa tu za chadema? hiyo sio siasa ya vyama vingi.
 
sijatazama tv mlimani lakini katika kipindi chake cha mahojiano itv prof amesema yeye kama atalinganishwa na slaa basi slaa ni kichuguu na yeye ni mlima kilimanjaro. nadhani anachokisema ni kweli kutokana na uwezo wake wa kuchanganua mambo bila uzushi ama kupika data ili kujidanganya mwenyewe na wananchi udhaifu alionao Slaa

Kama Lipumba kasema hayo, hakika inaleta logic kwa yeye kugombea uraisi mara ya nne sasa with declining prospensity.

Hakika wasomi wetu wanaonekana kuwa not only useless, but more accurately burden to the nation.
 
Unachosema kinawezekana kwa ni sahihi....Ila hizo ni kama hasira za CUF kuona CHADEMA wanakubalika zaidi yao, kitu ambacho CUF hawajagundua ni kuwa mbaya wao sio CHADEMA mbaya wao kama yupo basi ni CCM. Hilo la Slaa kama yeye kutokuwa tayari kugombea urais tangu mwanzo ni kweli, Slaa mwenyewe kasema mara kibao kuwa chama kilimwomba na kwa kusikiliza maoni ya wanachi, na kwa kufata ule msemo kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu yeye ndo akakubali na watanzania wameonyesha ni kweli kuwa yeye ndio kiongozi wanayemhitaji. kwa kugombea mara ya Nnne Lipumba ni kwamba sio anajikosesha kura yeye bali hata chama chake, kinakosa sbb kinaonekana hakina kiongozio mwingine zaidi ya walewale. CUF wangekazia kwenye ngome yao pemba, sasa wao wanamwachia maalim seif peke yake na Shein anapiga kambi huko kupunguza majimbo yua CUF.
Too late, no time.....si CCM si CUF kwa siku mbili hizi wataweza kubadilisha mawazo ya waTz wapenda mabadiliko
 
Ingelikuwa Invisible hajasema tusiandike PUMBA basi leo hii ningeliandika.

Ila kwa sababu hiyo, ngoja nijizuie.

Kichwa cha habari na habari yenyewe haziendani.

Sikonge,

Sema tu ukweli kwamba unaogopa kufungiwa! Tena inatakiwa ufungiwe kesho na kuachiwa Jumatano.
 
Vyama vya Upinzani Tanzania ni kama Simba na Yanga. Mwaka huu utakuwa wa Yanga kuitesa Simba, halafu itafuatia Simba nayo itamtesa Yanga.
Upinzania ndiyo hivyo hivyo, Chadema mwaka huu kina Washabiki wengi ambao hawatapiga kura siku ya uchaguzi. Halafu wakishindwa, itakuwa zamu ya CUF au TLP, na baadaye may be NCCR-Megeuzi kama kitafufuka tena.

Kumbuka tulikuwa na Mrema ambaye alikuwa NCCR-Mageuzi. Alikuwa na vishindo kama vya Mh. Slaa, lakini matokeo yake sasa hivi anaomba kazi kwa JK.

CUF haina haja ya kuiponda Chadema. CUF wakubali kwamba Nguvu za Soda mwaka huu zipo Chadema.
Any way, Chadema siyo Yanga. Yanga ni mabingwa.
 
Viongozi wa CUFwako live Mlimani tv. Moja kati ya mambo mazito waliyosema dhidi ya Chadema ni
1. Chadema kwenda kujaribu kumshawishi Hamad Rashid Hamad kujiunga na Chadema ili apewe ugombea mwenza wa Urais.
2. Chadema hawakujiandaa kugombea Urais, kwani hata Dr. Slaa hakujua kwamba anahitajika kugombea Urais. Yeye alikuwa tayari anajiandaa kugombea ubunge Karatu

Hivi jamani tuwe serious! sasa hapo kuna problem gani!?? Hebu tuelimishane sababu i can't c any problem!:bowl::bowl:
 
Hivi huyu Lipumba amegombea Urais mara ngapi vile? Na katika mara zote hizo mbona hakuwahi kuzikonga nyoyo za Watanzania na kuvuta umati wa watu kila alipopita kama inavyotokea kwa Rais wetu mtarajiwa Dr Slaa? Hana jipya huyu! Mpigie kura Dr Slaa na mbunge/diwani wa chadema.

Mkiambiwa nyinyi ni wageni kwenye upinzani, mnapandisha mizuka! Hata 2005 mlisema hayo hayo kuwa mpambano ni kati ya Kikwete na Mbowe matokeo yake Chadema waliishia kudai kuwa 2005 walikuwa wanabipu! Teh teh teh!!!
 
Hivi jamani tuwe serious! sasa hapo kuna problem gani!?? Hebu tuelimishane sababu i can't c any problem!:bowl::bowl:

Mfano katika suala la pili la Dr. Slaa kutojiandaa, viongozi wa CUF walisema kuwa baada ya Shekh Yahya kutoa utabiri wa kuwa yeyote atakaye gombea nafasi ya Urais dhidi ya JK angekufa. Wakasema Chadema waliogopa kauli hiyo na walipanga wasisimamishe mgombea kabisa. Ghafla, baada ya Prof. Lipumba kutangaza nia na baadaye kupitishwa na CUF kama mgombea urais kupitia chama hicho ndipo Chadema wakaamua kumtaja Dr.Slaa kama mgombea. Viongozi hao wakaendelea kuwasihi watanzania kwamba Chadema wame copy na ku paste ilani yao na hivyo wasiwapigie kura na kura zao zote zielekezwe kwa Prof. Lipumba. Huku kiongozi mmoja mwanamke akisema kuwa huwezi kuwa na mgombea anayetaka kuongoza nchi miezi 2 kabla ya uchaguzi hana wazo wala mpango wa kugombea urais...akaendelea kusema Dr. Slaa hajajiandaa kisaikolojia kupambana na changamoto za urais na hivyo amekurupuka.
 
Back
Top Bottom