CUF wafuta maandamano yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF wafuta maandamano yao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee wa Rula, Jun 11, 2011.

 1. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wana JF Prof. Ibrahimu Lipumba ametangaza kuwa kesho hakutakuwa na maandamo ya chama kama ilivyotangazwa na Julius Mtatiro baada ya kuombwa na waziri mkuu Mizengo Pinda. Hivyo amewataka wanachama na mashabiki kutojitokeza kesho kwenye maandamano na wale ambao hawatakuwa na taarifa ya kufuta maandamano basi wasibugudhiwe bali waalimishe.
  Source TBCI 20:00 Taarifa ya Habari.
   
 2. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hii ndio shida ya CCM B kutaka kupinga serikali wakati na yenyewe ni sehemu ya serikali. Nilikuwa najiuliza hivi lini alipewa talaka? Au alikuwa hajanunuliwa kanga kwa muda mrefu kwa hiyo alikuwa anatingisha kiberiti?
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu ati ya ugeni wa kitaifa wa Mama Clinton. Na kweli ni ugeni wa kitaifa kwaa kuwa nimeona Red carpet nikashangaa. Mimi Nadhani mkuu wa nchi ndio anakanyaga red carpet kumbe hata waziri wa mambo ya nje.

  Kuhusu hao ambao hawatapata taarifa nadhani Mwenyekiti wao anataka kuwaponza kwa kuwa Tanzania hatuna jeshi la polisi la kuelimisha tuna jeshi la kupiga!! Watapigwa!!
   
 4. KIMBURU

  KIMBURU JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kesho ilikuwa siku nzuri kuandamana coz Bi. Clinton yupo hapa. Wangekuwa CDM nadhan wangeitumia vema hii chance kama walivyowalk out bungeni. CUF hawako serious coz kama lengo ni kupinga uonevu wasingesubiri kunegociate na CCM ambaye ndiye muonezi mkuu.
   
 5. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kumbe pinda yupo, hazuii mauaji anazuia maandamano! Kama cuf walimaanisha wangetangaza kuyafanya next weekend, au labda clinton atakuwepo bado!
   
 6. ADAM MILLINGA

  ADAM MILLINGA Senior Member

  #6
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wameniboa sana
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Mwenyekiti Taifa wa chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba
  ----
  Mwenyekiti Taifa wa chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba ametangaza kufuta maandamano yaliyopangwa na chama hicho kufanyika kesho..Profesa Lipumba Amesema uamuzi huo umekuja baada ya kuombwa na Mhe Waziri Mkuu, Mizengo Pinda!Hivyo kesho hakutakuwa na maandamano hayo tena hadi siku yatakapotangazwa tena.

  CUF ilitangaza kufanya maandamano makubwa kesho kuanzia saa 3:00 asubuhi kutoka Ubungo hadi Manzese Bakheresa, lengo likiwa kupinga mauji yanayofanywa na polisi dhidi ya raia nchini. ​
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Naona Sheif S Hamad kazuia
   
 9. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wanamuugopa clinton kuliko Mungu, kwamba ni aibu kwa taifa kwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa marekani kuona watanzania wakiandamana kuiambia serikali yao iache kuua raia ambao wameiweka madarakani kwa tofauti zinazosababishwa na uwekezaji usiojali haki za msingi za wananchi wake. Hilary anaweza asione akiwa Tanzania lakini amesikia akiwa Marekani. Hata hivyo Mungu ameona na tayari ameisha fanya hukumu, kwani katika maagizo yake amekataza kuua, kwake hatuwezi kufanya unafiki kwani anatuona mpaka rohoni.
   
 10. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,613
  Trophy Points: 280
  Mi naona poa.pangeni j2 ijayo.
   
 11. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #11
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Cuf hamna lolote,
   
 12. M

  MPG JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CUF ni vibaraka wa CCM kwahiyo sishangai wao kumwabudu mgeni wa ccm HILARY CLITTON
   
 13. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wameona hakuna atakayetokea,labda ingekuwa ijumaa baada ya swala,j2 thubutu!
   
 14. m

  menny terry Senior Member

  #14
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  CUF ISHA ISHA.ET MAANDAMANO WAPI! Propesa li pumba hana chochote zaidi ya pumba kichwani mwake.
   
 15. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,700
  Trophy Points: 280
  Dah! mkuu umenichekesha sana! Sasa swala ya ijumaa na maandamano vina uhusiano gani?
   
 16. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Prof Lipumba bado atabaki kuwa lulu nchi hii kutokana na michango yake katika mambo mbali mbali mf. jinsi alivyoichambua bajeti iliyosomwa majuzi. Kasoro kubwa iliyomkumba ni nuru ya chama chake imeanza kufifia.
   
 17. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MarkoMAANDAMANO yaliyokuwa yafanywe jana na Wanachama wa CUF, yaliahirishwa baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwaomba wasitishe kama walivyoambiwa na Jeshi la Polisi kutokana na ugeni wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton.

  Cliton ambaye aliwasili nchini juzi kwa ziara ya siku tatu, jana alitembelea mitambo ya kuzalisha Umeme ya Symbion iliyopo Ubungo Dar es Salaam ambapo ndipo maandamano ya CUF yalitakiwa kuanzia na kumalizikia Manzese Bakhresa.
  Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro aliliambia gazeti hili jana kuwa waliahirisha maandamano hayo kutokana na ombi la Waziri Pinda kupitia Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba ambalo alimtaka asitishe maandamano kutokana na ugeni uliopo.

  Mtatiro alisema jana kwamba Profesa Lipumba alipokea barua kutoka kwa Pinda iliyoitaka CUF kusitisha maandamano hayo kwa sababu maeneo yalipotakiwa kuanzia ni moja ya sehemu ambazo mgeni huyo angetembelea.

  Alisema Pinda aliwataka kusitisha maandamano hayo kwa sababu za kiusalama kwa kiongozi huyo wa Marekani.“Busara za uongozi wa Waziri Mkuu zilitumika, wakatuambia kuwa maeneo ambayo tungefanyia maandamano hayo ndiko msafara wa kiongozi huyo ungepita kwa hiyo viongozi waandamizi wa CUF tulikaa pamoja na kukubaliana tuyaahirishe,”alisema na kuongeza kuwa;“Pinda alitushauri na kutueleza kuwa kama sisi tungekuwa ndiyo viongozi wa nchi halafu kuna ujio wa kiongozi mkubwa kama huyo anayekuja akakuta maandamano ingekuwaje?

  Tulimuelewa na ndio maana tumeahirisha.”Hata hivyo Mtatiro alilishutumu Jeshi la Polisi kutokuwa wawazi kwa kudai kuwa walikataa maandamano hayo kwa sababu za kiusalama bila kueleza kuwa Clinton atafanya ziara katika maeneo ambayo yatakuwapo maandamano.

  “Baada ya ufafanuzi huo wa barua ya Waziri Pinda tulikaa kikao na viongozi waandamizi wa chama tukajadili na kuona ni vema tukaahirisha ili hata msafara wa Clinton ukipata tatizo tusilaumiwe,” alisema Mtatiro.

  Pia alisema baada ya kuondoka kwa kiongozi huyo wa Marekani, CUF itakaa kikao na viongozi waandamizi wa chama hicho ili kupanga siku ambayo watafanya maandamano. Juni 6 mwaka huu, CUF ilitangaza kufanya maandamano makubwa ambayo yangefanyika jana kuanzia Ubungo hadi Bakhresa Mazense kwa lengo la kupinga mauaji yanayofanywa na polisi dhidi ya raia nchini.
  Lakini kulikuwa na mvutano mkubwa baina yao na polisi ambao waliwataka CUF kutofanya maandamano lakini walisisitiza kuendelea na msimamo wao wakidai kuwa Clinton si kiongozi wao, bali ni Mmarekani hivyo hawezi kuzuia maandamano hayo yanayodai haki za Watanzania.
  Akitolea mfano Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu (UDHR) la mwaka 1945 linatoa haki ya kuandamana ikiwa watu au chama kinataka kuonyesha hisia zake kwa jamii na kwamba Tanzania ni mjumbe wa umoja huo na imeridhia.
  “Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 ambayo tayari ina viraka zaidi ya 14 inatoa haki kwa raia wa Tanzania, vikundi au taasisi kutoa mawazo au hisia zao na hii iko kifungu ch 1 ibara ya 20,”alisema.

  Aidha Mtatiro alisema kifungu cha 43(3) kinaeleza kuwa Ofisa wa Polisi hawezi kukataza maandamano chini ya kifungu cha 43 (2), isipokuwa iwapo atajiridhisha kuwa mkusanyiko huo utasababisha uvunjifu wa amani au utaathiri usalama wa nchi.
  Alisema maandamano yatakayofanywa na CUF yatakuwa ya amani na kwamba hayatakuwa na silaha za moto isipokuwa watabeba mabango na kufikisha ujumbe walioukusudia kwa wananchi.“Kwa mantiki hiyo kukataza maandamano bila polisi kusema yatavuruga vipi amani ni uzembe wa dhahiri na kamwe chama hakiwezi kusitisha maandamano kwa kutekeleza uzembe,”alisema.
   
 18. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  aaahg,.................. mbona hapo ndipo palikuwa pazuri sasa na ujumbe wao ungeifikia marekani na dunia nzima instantly???...................... hawa cuf nao vipi??.................. they had knowingly given up a golden chance!!.................
   
 19. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  dah! Hawa cuf wajinga sana, yaani wanapewa sound wanakubali kiulaini kama shori.
   
 20. Joste

  Joste Senior Member

  #20
  Jun 13, 2011
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa CUF walipaswa kuliona hilo mapema kabla ya kuombwa na Pinda. Imagine kama tukiwapa dola itakuwaje.... vululu vululu mpaka basi
   
Loading...