Dodoma: RPC Muroto azuia maandamano ya Amani ya vijana wa ACT na vyama vingine vya Upinzani. Asema atakayeandamana atapigwa hadi achakae!

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amewatahadharisha waliopanga kufanya maandamano kesho Jumanne Aprili 9, 2019 akisema watakaoingia barabarani watapigwa na kuchakaa.



Kamanda Muroto amewaambia waandishi wa habari jijini Dodoma leo Jumatatu Aprili 8, 2019 kuwa zipo taarifa zina sambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa baadhi ya vyama vya upinzani ikiwepo ACT Wazalendo wamepanga kufanya maandamano kesho kushinikiza Bunge kufuta kauli yake ya kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad.

Amesema kuwa wapo wengine wamepanga kusafiri kuja Dodoma kwa ajili kufanya maandamano hayo akiwataka kuacha mara moja kwani wataambulia kupigwa na kuchakaa.

“Niwatake wale wote waliopanga kufanya maandamano kesho Aprili 9, 2019 kusitisha maandamano yao haramu, wasije kuingia barabarani maana watapigwa na kuchakaa,” amesema Muroto.

Muroto amesema kazi za Bunge zinahojiwa ndani ya Bunge na si nje ya Bunge hivyo amewataka wananchi wa Dodoma kuendelea na kazi zao kama kawaida kwani hakuna maandamano yoyote yatakayofanyika.

Hata hivyo amesema jeshi hilo limejipanga kikamilifu kukabiliana na wale wote waliopanga kufanya matukio ya uhalifu katika kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu ya Pasaka.

Amesema askari polisi wamejipanga kuingia mtaani kuwatia mbaroni watu wa aina hiyo.

Soma hapa Tangazo la vijana wa vyama vya upinzani kuandamani
My Take!
KAMANDA MROTO TII SHERIA BILA SHURUTI, TUTAANDAMANA

RPC wa Dodoma ametuzuia vijana KUITETEA KATIBA, ameagiza tusiandamane kesho April 9, 2019 Dodoma kulitaka Bunge LIFANYE KAZI na CAG.

Kamanda Mruto anasema eti Bunge halihojiwi nje, tukalihoji ndani. Sijui hii sheria ya nchi gani? Kwahiyo tungeandamana kuunga juhudi za Rais tungepaswa kwenda Ikulu ndani?

Muroto ANAVUNJA KATIBA bila soni wala haya, hii ni aibu kwa Jeshi la Polisi. Ni fedheha kwa utawala wa awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.

HII HAIKUBALIKI!

Nipo hapa Nyerere Square, Dodoma ambapo kesho Maandamano yetu ya Amani yanayoratibiwa na Ngome ya Vijana ya ACT WAZALENDO ikishirikiana na Ngome zingine za vijana wa vyama vya siasa nchini, YATAANZA na kuishia viwanja vya Bunge ambapo tunatarajia Spika Ndugai atupokee.

#IStandWithCAG

FB_IMG_1554710897537.jpeg
 
Back
Top Bottom