CUF vipi katibu mkuu anakuwa mwenyekiti?

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Najua mtasema mbona hata CCM katibu mkuu ndiye mwenyekiti wa sekretarieti. Lakini ile inapaswa kuwa kamati ya utekelezaji wa maamuzi na kama CUF wanavyoiita kamati ya utendaji. Ina maana yupo anayeamua (labda kamati kuu au baraza) na kamati inasimamia utendaji. Lakini hili la sasa la kuwashughulikia waasi naona katibu mkuu kawa mwenyekiti kamili.

Kisha mna makatibu wasaidizi wawili, mmoja anasikika sana Tanganyika na Zanzibar na mwingine amekaa kimya tu akimwacha huyu wa huku abwabwaje. Hata minutes za vikao anazimwaga JF bila wasiwasi. Sasa huyu ndiye katibu mwa mwenyekiti maalim? Kuna nchi duniani zina rais wa heshima asiye na meno kama ilivyo kule Israel, ujerumani na India. Ndio nafasi ya Lipumba CUF?
 
Kazi ipo kama mwana JF ana katiba ya CuF aiweke jamvini tupate kuidodosa na kujua zaidi!!labda wako sawa kutokana na katiba yao...ambayo waliibadilisha hao hao wa 2 ambao leo wanagombana....wakiwa kizuizini kwa muda mrefu sana!!!
 
Yaani CUF ni kama Popo, hawaeleweki, chama kina makamu mwenyekiti, sasa anafanya kazi gani?.
Hapa ndipo tunapojua kuwa CUF ni Maalim, kazi kwelikweli, sasa ambu fikiria hao ndio unawakabidhi nchi sijui itakuwaje?.
 
Waache wafu wazikane wenyewe!!.........
kama wasipoelewana shura ya Maimamu itaingilia kati kusuruhisha.
 
CUF ni maalim hilo mbona liko wazi, Yule Mnyamwezi amewekwa tu hana meno kama m/kiti.
 
Kazi ipo kama mwana JF ana katiba ya CuF aiweke jamvini tupate kuidodosa na kujua zaidi!!labda wako sawa kutokana na katiba yao...ambayo waliibadilisha hao hao wa 2 ambao leo wanagombana....wakiwa kizuizini kwa muda mrefu sana!!!

Kama wako sawa kwa mujibu wa katiba yao, basi wana katiba mbovu kuliko katiba mbovu zaidi. Huwezi kuwa mtendaji kisha ukawa mtoa maamuzi na tena ukaja kujitathmini umetendaje na si ajabu hata auditing ukajifanyia wewe mwenyewe na kujipa clean reports. CUF acheni hizo!
 
cuf ni shaban mloo na kapalala...........plus......hamadi rashid....maalim seif aliopolewa tuu ila sasa kaja kuiteka nchi ya wenyewe. yaani ni kama vile ccm ya nyerere ilivyokujatekwa na wakuja Rostam.!
 
Katibu wa CUF ndie alieasisi chama, so kwa hapa zinadumu fikra za katibu, sio za mwenyekiti tena!!!!!!!
 
Nafurahi kuna wana CUF wanawaza kama nilivyothibitisha

A: MADAI YA MABADILIKO YA KATIBA

1. Uwepo wa Makamu mwenyekiti bara

2. Mwenyekiti Taifa na Makamu wake wawili waingie kwenye Kamati Tendaji Taifa
 
Kama wako sawa kwa mujibu wa katiba yao, basi wana katiba mbovu kuliko katiba mbovu zaidi. Huwezi kuwa mtendaji kisha ukawa mtoa maamuzi na tena ukaja kujitathmini umetendaje na si ajabu hata auditing ukajifanyia wewe mwenyewe na kujipa clean reports. CUF acheni hizo!

msiwe mnaropoka muwe hata mnasikiliza habari kikao cha kumzika hamad kiliongozwa na makamu mwenyeki mhe .Hamisi Machano nitakuwa na washangaa sana mnaongea vitu msivyo vijua
 
Back
Top Bottom