CUF: Vikwazo vya Marekani na Uingereza dhidi ya Tanzania

CUF Habari

Verified Member
Dec 12, 2019
239
250
TAARIFA KWA UMMA

MISIMAMO YA MAREKANI NA UINGEREZA DHIDI YA WATANZANIA KUKANYAGA ARDHI ZA MATAIFA HAYO:

CUF- Chama Cha Wananchi kimepokea Matamko ya Mataifa makubwa ya Marekani na Uingereza kwa namna tofauti.
Wakati Marekani ikipiga Marufuku Maafisa walioshiriki kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa 2020 kukanyaga ardhi ya Taifa hilo, Uingereza imetangaza zuio kwa wasafiri wote wanaotaka au waliopita Tanzania kukanyaga ardhi ya Taifa hilo kutokana na Tishio la Maambukizi Makubwa ya CORONA.

1. MSIMAMO WA MAREKANI DHIDI YA MAAFISA WALIOVURUGA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2020:
CUF- Chama Cha Wananchi kwenye Tamko lake kwa Umma la Novemba 2, 2020 kilieleza bayana matendo ya makusudi ya kuhujumu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 na kupelekea Matokeo yaliyotangazwa na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kukosa Uhalali. Kiujumla Chama kiliyapinga Matokeo ya Uchaguzi Mkuu huo kwa ngazi zote, kwa kuwa Uchaguzi huo haukuwa Huru na wa Haki.

Watanzania wenyewe walioshiriki kwenye Uchaguzi huo waliuponda Uchaguzi huo kutokana na kugubikwa na mambo mengi tena ya aibu kwa Taifa, yaliyolenga kupoka haki ya Wananchi ya Kuwachagua Viongozi wawatakao.

CUF- Chama Cha Wananchi pamoja na kuunga mkono msimamo wa yeyote anayepinga Matendo ya Kubaka Demokrasia na kukiuka Haki za Binadamu, kinatoa wito kwa Serikali kutofumbia macho tatizo hili la msingi na badala yake ichukue hatua za msingi za Kuunda Tume huru ya Uchaguzi na kuruhusu Utamaduni wa kuheshimu Maamuzi ya wapiga kura.

2. MSIMAMO WA UINGEREZA DHIDI YA WASAFIRI KUTOKA TANZANIA:
Pamoja na kuunga mkono msimamo wa Serikali wa kuwaruhusu Watanzania waendelee na harakati za Uzalishaji mali na Shughuli za Kimaisha , CUF-Chama Cha Wananchi mara kadhaa kimetoa wito kwa Serikali juu ya Umuhimu wa kuweka Utaratibu wa kupima ili kutambua uhalisia kuhusu hali ya Maambukizi ya CORONA.

Taarifa zisizo rasmi ni kuwa Maambukizi ya CORONA yanaongezeka nchini. Kwa kuwa hatupimi, hajui ukweli Wala ukubwa wa tatizo. Kimelea hatari zaidi Cha Corona Cha Mutated Corona Virus Cha Afrika Kusini huenda pia kimeshaingia Tanzania.

Wito wetu ni kwamba tujiunge na Taratibu za Shirika la Afya Duniani (WHO) za kupima na kufanya Maandalizi ya Chanjo dhidi CORONA tutakayoipata kupitia Africa CDC na Taasisi ya Kimataifa ya COVAX inayosimamia ugawaji wa chanjo kwa nchi maskini.

Kuna hatari ya Tanzania kutengwa katika usafiri wa Kimataifa endapo hatutafuata taratibu za Kisayansi za kupima na kuzuia Maambukizi ya CORONA.

HAKI NA FURAHA KWA WOTE!

Eng. Mohamed Ngulangwa
Mkurugenzi wa Habari,Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF- Chama Cha Wananchi
Januari 23, 2021
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
11,063
2,000
Hiyo miradi haitaisha Leo wala kesho anajisumbua tu. Aheshimu uhai wa Watanzania Mungu atafanya la sivyo anapiteza nguvu zake bure ....asipoangalia Mungu anamfunza adabu ataumwa yeye soon .....acha adharau afya walio wengi sababu ya miradi yao .....tembo mweupe
 
  • Love
Reactions: BAK

Mtuflani Official

JF-Expert Member
Dec 31, 2019
1,062
2,000
IMG_8512.JPG
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,230
2,000
Zuio litakuwa na athari kwa Profesa lipumba ambaye ni mshauri wa uchumi wa bunge la congress la marekani
 
Rusende

Member
Jul 27, 2016
88
125
TAARIFA KWA UMMA MISIMAMO YA MAREKANI NA UINGEREZA DHIDI YA WATANZANIA KUKANYAGA ARDHI ZA MATAIFA HAYO: CUF- Chama Cha Wananchi kimepokea Matamko ya Mataifa makubwa ya Marekani na Uingereza kwa namna tofauti. Wakati Marekani ikipiga Marufuku Maafisa walioshiriki kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa 2020 kukanyaga ardhi ya Taifa hilo, Uingereza imetangaza zuio kwa wasafiri wote wanaotaka au waliopita Tanzania kukanyaga ardhi ya Taifa hilo kutokana na Tishio la Maambukizi Makubwa ya CORONA. 1.MSIMAMO WA MAREKANI DHIDI YA MAAFISA WALIOVURUGA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2020: CUF- Chama Cha Wananchi kwenye Tamko lake kwa Umma la Novemba 2, 2020 kilieleza bayana matendo ya makusudi ya kuhujumu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 na kupelekea Matokeo yaliyotangazwa na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kukosa Uhalali. Kiujumla Chama kiliyapinga Matokeo ya Uchaguzi Mkuu huo kwa ngazi zote, kwa kuwa Uchaguzi huo haukuwa Huru na wa Haki. Watanzania wenyewe walioshiriki kwenye Uchaguzi huo waliuponda Uchaguzi huo kutokana na kugubikwa na mambo mengi tena ya aibu kwa Taifa, yaliyolenga kupoka haki ya Wananchi ya Kuwachagua Viongozi wawatakao. CUF- Chama Cha Wananchi pamoja na kuunga mkono msimamo wa yeyote anayepinga Matendo ya Kubaka Demokrasia na kukiuka Haki za Binadamu, kinatoa wito kwa Serikali kutofumbia macho tatizo hili la msingi na badala yake ichukue hatua za msingi za Kuunda Tume huru ya Uchaguzi na kuruhusu Utamaduni wa kuheshimu Maamuzi ya wapiga kura. 2. MSIMAMO WA UINGEREZA DHIDI YA WASAFIRI KUTOKA TANZANIA: Pamoja na kuunga mkono msimamo wa Serikali wa kuwaruhusu Watanzania waendelee na harakati za Uzalishaji mali na Shughuli za Kimaisha , CUF-Chama Cha Wananchi mara kadhaa kimetoa wito kwa Serikali juu ya Umuhimu wa kuweka Utaratibu wa kupima ili kutambua uhalisia kuhusu hali ya Maambukizi ya CORONA. Taarifa zisizo rasmi ni kuwa Maambukizi ya CORONA yanaongezeka nchini. Kwa kuwa hatupimi, hajui ukweli Wala ukubwa wa tatizo. Kimelea hatari zaidi Cha Corona Cha Mutated Corona Virus Cha Afrika Kusini huenda pia kimeshaingia Tanzania. Wito wetu ni kwamba tujiunge na Taratibu za Shirika la Afya Duniani ( WHO) za kupima na kufanya Maandalizi ya Chanjo dhidi CORONA tutakayoipata kupitia Africa CDC na Taasisi ya Kimataifa ya COVAX inayosimamia ugawaji wa chanjo kwa nchi maskini. Kuna hatari ya Tanzania kutengwa katika usafiri wa Kimataifa endapo hatutafuata taratibu za Kisayansi za kupima na kuzuia Maambukizi ya CORONA. HAKI NA FURAHA KWA WOTE! Eng. Mohamed Ngulangwa Mkurugenzi wa Habari,Uenezi na Mahusiano na Umma CUF- Chama Cha Wananchi Januari 23, 2021
 
Rusende

Member
Jul 27, 2016
88
125
TAARIFA KWA UMMA

MISIMAMO YA MAREKANI NA UINGEREZA DHIDI YA WATANZANIA KUKANYAGA ARDHI ZA MATAIFA HAYO:

CUF- Chama Cha Wananchi kimepokea Matamko ya Mataifa makubwa ya Marekani na Uingereza kwa namna tofauti.
Wakati Marekani ikipiga Marufuku Maafisa walioshiriki kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa 2020 kukanyaga ardhi ya Taifa hilo, Uingereza imetangaza zuio kwa wasafiri wote wanaotaka au waliopita Tanzania kukanyaga ardhi ya Taifa hilo kutokana na Tishio la Maambukizi Makubwa ya CORONA.

1.MSIMAMO WA MAREKANI DHIDI YA MAAFISA WALIOVURUGA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2020:

CUF- Chama Cha Wananchi kwenye Tamko lake kwa Umma la Novemba 2, 2020 kilieleza bayana matendo ya makusudi ya kuhujumu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 na kupelekea Matokeo yaliyotangazwa na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kukosa Uhalali. Kiujumla Chama kiliyapinga Matokeo ya Uchaguzi Mkuu huo kwa ngazi zote, kwa kuwa Uchaguzi huo haukuwa Huru na wa Haki.

Watanzania wenyewe walioshiriki kwenye Uchaguzi huo waliuponda Uchaguzi huo kutokana na kugubikwa na mambo mengi tena ya aibu kwa Taifa, yaliyolenga kupoka haki ya Wananchi ya Kuwachagua Viongozi wawatakao.

CUF- Chama Cha Wananchi pamoja na kuunga mkono msimamo wa yeyote anayepinga Matendo ya Kubaka Demokrasia na kukiuka Haki za Binadamu, kinatoa wito kwa Serikali kutofumbia macho tatizo hili la msingi na badala yake ichukue hatua za msingi za Kuunda Tume huru ya Uchaguzi na kuruhusu Utamaduni wa kuheshimu Maamuzi ya wapiga kura.

2. MSIMAMO WA UINGEREZA DHIDI YA WASAFIRI KUTOKA TANZANIA:

Pamoja na kuunga mkono msimamo wa Serikali wa kuwaruhusu Watanzania waendelee na harakati za Uzalishaji mali na Shughuli za Kimaisha , CUF-Chama Cha Wananchi mara kadhaa kimetoa wito kwa Serikali juu ya Umuhimu wa kuweka Utaratibu wa kupima ili kutambua uhalisia kuhusu hali ya Maambukizi ya CORONA.

Taarifa zisizo rasmi ni kuwa Maambukizi ya CORONA yanaongezeka nchini. Kwa kuwa hatupimi, hajui ukweli Wala ukubwa wa tatizo. Kimelea hatari zaidi Cha Corona Cha Mutated Corona Virus Cha Afrika Kusini huenda pia kimeshaingia Tanzania.

Wito wetu ni kwamba tujiunge na Taratibu za Shirika la Afya Duniani ( WHO) za kupima na kufanya Maandalizi ya Chanjo dhidi CORONA tutakayoipata kupitia Africa CDC na Taasisi ya Kimataifa ya COVAX inayosimamia ugawaji wa chanjo kwa nchi maskini.

Kuna hatari ya Tanzania kutengwa katika usafiri wa Kimataifa endapo hatutafuata taratibu za Kisayansi za kupima na kuzuia Maambukizi ya CORONA.

HAKI NA FURAHA KWA WOTE!Eng. Mohamed Ngulangwa
Mkurugenzi wa Habari,Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF- Chama Cha Wananchi
Januari 23, 2021
Asante kwa kutukumbusha kuwa bado mpo!!
 
Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
2,411

Cuf hata hamwaminiki tena mama chaka baada ya yale ya kukubali kuivuruga na kuiuwa cud tuliyoifahamu,kupitia ofisi ya buguruni na msajili,chochote msemacho tunajuwa mnatumiwa na wale wanaohujumu democrasia ya kweli.Hivyo ni bora hata msituletee habari zenu uchwara.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom