CUF-Uislam, CHADEMA - Ukristo, CCM - Mixture+UFISADI, Mungu epusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF-Uislam, CHADEMA - Ukristo, CCM - Mixture+UFISADI, Mungu epusha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mkimbizi, Aug 20, 2010.

 1. Mkimbizi

  Mkimbizi JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona kama kitu hiki kinakuja na kinaniumiza sana moyo wangu maana hatuwezi kuendelea kamwe. Kuna watu wanaleta siasa hizi sa dini(mmeona na gazeti fulani lilivyosema leo),,,,,,

  Kwa minajili hii CCM haitatoka kamwe!!! Na wataongoza maana misikitini wanasema CUF, makanisani(ukweli sijasikia wakipigia debe chochote) lakini kuna upepo wa CHADEMA sasa tutafika kweli..,,,

  Tuungane jamani, usipende CUF eti sababu ni Muislam au CHADEMA sababu mkristo. Pembenua points, ona uozo uliopo sasa na angalia mikakati ya kutoa uozo huo. Otherwise hii mijamaa itashinda tena kwa more than 70% trust me!!!!!

  Wanatugawa na tunagawanyika... STOP THIS!!!!!!
   
 2. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hayo mambo ya udini yanakuzwa zaidi na magazeti uchwara.
   
 3. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mkimbizi bwana,

  Misingi gani inatumika kusema kuwa cuf ni waislam?

  Kama ni viongozi, viongozi wa juu wa CCM wengi wao ni waislam lakini je, hiyo ni sababu ya kusema ccm ni chama cha waislam? Angalia NEC na CC ya ccm uone mgawanyo wa dini (yes ninajua dini zao maana wao wenyewe wanaziweka wazi). Je CCM pia ni chama cha waislam?
   
 4. Nungunungu

  Nungunungu JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2010
  Joined: Feb 13, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umesema ukweli ambao wengi wanaogopa kuusema. Kwa anaesikia wanachotamka waislam wengi mitaani na wakristo maofisi mengi atajua muelekeo ni huo ulioutaja. Hii sio siri tena.
   
 5. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2010
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Huu ni ushabiki CUF ina support ya waislam wengi kwasababu inasapoti Zanzibar ambako 90% ya watu ni waislam.

  Chadema haina dini labda kwasababu Dr Slaa allikuwa padre lakini sijaona ukristo wowote Chadema. Chama cha Chadema kwa mawazo yangu kinaendeshwa kama biashara, ambayo si kitu kibaya kwa upande fulani kwani Tanzania kama unatatarika huwezi kuongoza kitu, chama kinachokuwa kinatakiwa kiendeshwe kibiashara ili kiweze kudumu. Miaka inayokuja CUF itabadilika kwasababu ya serikali ya mseto lakini Chadema naona kama itakuwa imara zaidi.

  CCM inatakiwa kubadilika na kitu cha kwanza ni kutafuta wagombea ambao ni watu wa results na sio wanasiasa wa kupiga midomo tu. Watu wengi wenye akili Tanzania hawako kwenye siasa.
   
 6. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nungunungu bana, ana uwezo wa kuongoea na waislam mitaani na wakristo maofisini!
   
 7. P

  Paul S.S Verified User

  #7
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  mkuu hiyo kitu ipo sana tu hasa magazeti uchwara
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Aug 20, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwafrika mkuu wangu msitake kubisha tu kwa sababu nyie hamna imani ya kuwepo kwa vitu hivi lakini jueni kwa ukakika kwamba wWatanzania wengi na hasa wanachama wa vyama hivi hivi Wanaamini hivyo. Ukweli ni Upi (ingawa unauma na hatupendi kuukubali)

  1. Hesabu kubwa ya wanachama wa CUF (over 80%) wanaamini Chadema ni chama cha Wakristu(wao wenyewe asilimia kubwa 80% ni Waislaam.) na hawajifichi.
  2. Hesabu kubwa ya wanachama wa Chadema (over 80%) wanaamini CUF ni chama cha Waislaam (wao wenyewe asilimia kubwa ...% ni WaKristu) na hawajifichi.
  3. WanaCCM wao ni mchanganyiko ktk imani zao wapo wanaoamini CUF na Chadema ni vyama kidini na wapo wengi tu wasioamini hivyo kwa sababu members wengi wa CCM ni hawafuati dini zaidi ya chama..Ni wakristu au Waislaam lakini chama kimesimama mbele na imani zao za dini nyuma - They need Jesus!

  Lakini kwa ujumla wa hawa na WATANZANIA wote kwa ujumla wetu, sisi sote hatuna dini ila kwa kuzaliwa.. Ni wanafiki tu wa dini hizi..A true Christian or Muslim will never look over his/her shoulder kumtafuta mchawi. Na hata siku moja muumini wa kweli hawezi kuhofia hatma yake kutokana na pato la mtu mwingine.. Huu ni Uchawi unapotumika ndani ya dini.
   
 9. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  huu ni ukweli ambao unauma sana na umesambazwa na ccm kwa manufaa yao wenyewe

  cuf na chadema wanahitaji kureform vyama vyao na kuhakikisha kuna balance ya dini na wana attract watu wa dini nyingine, the best solution ni wao kuungana
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Chama chochote mufilisi huwa kinakimbilia kwenye kuwagawa wananchi kwa misingi ya udini na ukabila. Maana wanajua kuwa kwa kutumia sera hawatashinda kwani wameisha danganya sana. CCM is behind all these controversial.

  Kama nchi itaingia kwenye vurugu za kidini na kikabila wa kulaumiwa ni CCM kwa kuanzisha propaganda ambazo ni hatari kwa Taifa letu. Sooner or later CCM will start eating itself on these issues. Huwezi kuwa na chama makini kama propagandists wake ni watu wanaofikiria katika kiwango cha kina Tambwe Hiza.
   
 11. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,485
  Likes Received: 1,216
  Trophy Points: 280
  Mambo ya divide and rule ndo yameanza
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mkandala umesema ukweli kwa sehemu kubwa kuhusu kadhia hii ya udini katika vyama lakini umeamua kutosema au waswahili wanasema umeminya ukweli kuwa sasa na CCM imeshakuwa kwenye makundi haya mawili ya kafu na chadema kwa kubeba waislamu. Jambo hili liko wazi wala tusijidanganye kuwa wao wako neutral. No si kweli hata kidogo.

  Hili wala si kificho na mtu asidanganye kwamba sisi M wamepona katika mchezo huu walioanzisha wenyewe. Linajulikana hata wakitafuta kujivua kwa hili wameshachafuka.

  Habari ndiyo hiyo.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Aug 21, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu sijui kama umenisoma vizuri..

  Mimi siamini kama CUF na Chadema ni vyama vilivyoanzishwa kwa Udini hata kidogo, isipokuwa nimegundua kwamba ni wanachama wa vyama hivi (kama desturi yetu ya kutazama wengine) ndio wanaamini kwamba chama kingine kimeegemea dini fulani.

  Wapo hapa wanachama wa Chadema na wanaonyesha wazi kabisa kwamba wanaamini kuwa CUF ni chama cha Waislaam. Deep down they're Islamophobic. Na hao wa CUF ambao wapo hapa pia wanaamini kwamba Chadema ni chama cha Wakristu hata kama lugha hizi wanagonganishwa na CCM au laa. Chuki baina ya CUF na Chadema inatokana na udini wa wanachama wake.

  Kibaya kuliko yote sijawasikia CCM wenyewe wakisema wazi kwamba CUF ni ya Waislam au Chadema ni ya Wakristu isipokuwa CCM kwa kutumia wajinga fulkani ndani ya vyama hivi wamefanikiwa kueneza hizi hisia za udini baina ya CUF na Chadema kwani hofu kubwa ya CCM ni pale CUF na Chadema watakapoweza kufikia muafaka.

  Mkuu wangu unaposema CCM kufikia Muafaka na CUF ni kwamba wamewabeba Waislaam ni hisia zako na inathibitisha hofu yangu kwamba kwatu wengi wanavitazama vyama hivi kupitia dini zaidi ya kile wanachokisimamia. Na kama CCM ingefikia Muafaka na Chadema basi nina hakika Malaria Sugu angesema CCM imefikia muafaka na Wakristu. Na kutokana na sababu hizi ndio maana haijawahi kutokea makubaliano mazuri baina ya CUF na Chadema kwa sababu kila mmoja wao anamhofia mwenzake.

  Mkuu wangu CCM imefikia muafaka na CUF kwa sababu CUF ingeshinda uchaguzi huu kirahisi sana kutokana na kauli ya Pinda na viongozi wengine wa bara kusema kwamba Zanzibar sio nchi ndani ya Muungano. kauli ile iliwatisha na kuonyesha wazi kile mwalimu alichokuwa akijaribu kukiepuka yaani kuonyesha Zanzibar imemezwa na bara. Ndipo Wazanzibar wote wakajipanga nyuma ya viongozi wao kupinga kauli ile hata kama kimadaraka wanaye rais wao, bunge lao, bendera yao na kadhalika.. Kuwakatalia tu kwamba Zanzibar is not a state tayari bara tulikwisha vunja Mkataba ulowekwa na Mwalimu na Karume mwaka 1964 kwani katiba na hata hotuba ya mwalimu ilikuwa wazi kuelezea nafasi ya Zanzibar ndani ya Muungano.

  In all, matatizo ya CCM hayatakwisha ktk uchaguzi huu, nina hakika watajaribu ku downpaly the all issue ili CUF wasipate kushika madaraka ya juu Zanzibar...Nina hakika cheo ambacho Seif ataambulia ni makamu wa rais wa Zanzibar na kama mjuavyo makamu wa rais hana kazi zaidi ya kusubiri kifo cha Shein..CCM watakamata kiti cha rais na Waziri mkuu madudu mengine yote watawaachia CUF wagombanie makoko ya pilau la CCM.

  Hii ni Ramadhan kareem, mtu kama Dr. Slaa anatakiwa kutumia muda wake mwingi kujumuika na waislaam ktk ibada hii kwani haikuanzwa na Waislaam au Muhammad (S.A.W). Kama sikosei Mtume Muhammad alipata (wahi) sura ya kwanza ya dini (chapter) hii akiwa katika mfungo wa Ramadhan, hivyo inaonyesha wazi kwamba mfungo wa Ramadhan uilikuwepo kabla yake.
   
 14. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #14
  Aug 21, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Ndugu zangu Watanzania

  Nawaombeni tujihadhari na siasa hizi uchwara za kutugawa. Waliodai kwamba CUF ni chama cha Waislam ni CCM. Na waliodai kwamba CHADEMA ni chama cha Wakristo ni CCM pia!

  Mimi si mwana CCM, CHADEMA wala CUF, ila ni Mtanzania halisi ninayeipenda nchi yangu!

  Siasa za aina hii zinaitwa "divide and rule", yaani, "wagawe uwatawale". CCM inajua kwamba Watanzania wakiungana kwenye chama kimoja HAWATATAWALIKA. Kwa hiyo, kila chama cha upinzani kinachojitokeza kuwa mahiri kinapigiwa zengwe ili kionekane kina kasoro.

  CUF hawana udini, wala CHADEMA hawana udini. Kwenye kila chama kuna takriban idadi sawia ya viongozi ambao ni wa dini za kikristo na kiislam. Kama mtakubali kuendelea kuamini kwamba CUF ni chama cha Waislam, na CHADEMA ni chama cha Wakristo, basi ninyi ni WAPUMBAVU kupita kiasi, kwani mnashindwa kufanya utafiti kubaini ukweli wa mambo halisi!

  Watanzania tuache uvivu wa kufikiria. Sio kila kitu kinachoandikwa kwenye magazeti, au kutangazwa kwenye redio na luninga ni cha kweli! Kama mwandishi wa habari najua jinsi wanasiasa wanavyocheza na vyombo vya habari kama silaha yao kuu ya kuwagawa wananchi!

  Mwaka huu, kama wewe ni CUF, CHADEMA, NCCR-Mageuzi, TLP, UDP au chama chochote kile kingine cha upinzani, mpigie kura mgombea yeyote wa upinzani, si lazima awe wa chama chako! Lakini kama wewe ni wa CCM, kumbuka, nchi hii ni yetu wote, kwa hiyo kama mgombea wako ni FISADI, usimchague, mchague yule anayefaa, hata kama si wa chama chako!

  Tanzania ni yetu wote, SI MALI YA CCM!

  ./Mwana wa Haki
   
 15. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Hizi "talking points" ndio zinaanza kujitokeza. Ni wazi CCM wameamua "talking point" yao kubwa ni kusema CUF cha Waislamu, CHADEMA cha Wakristu, na CCM ni cha wote. Logic gani hiyo? Yaani Wakristu wachague CHADEMA , Waislamu wachague CUF na hao WOTE watakaobaki kuchagua CCM wako wapi?

  Jakaya Kiwete na Gharib Bilal wanaweza kuitazama CUF wakasema ile ina Waislamu wengi kwa hivyo ni mbaya. Wakaitazama CHADEMA wakasema ile ina Wakristo wengi kwa hivyo ni mbaya. Ila Watanzania wa kawaida Wakristu na Waislamu wanaishi kwa ushirikiano na upendo karibu kuliko nchi nyingine yoyote duniani. Kunapotokea msiba au harusi mtaani wote wanashiriki kama ndugu, bila kujali dini. Kuwagawa kidini si rahisi.

  Taliking point itakayokuwa na mshiko mwaka huu ni ya UFISADI. Dr. Slaa akiwaambai watu CCM inalea ufisadi wote watamwamini. Wala Ukristu wake hautakuwa kipimo.
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Aug 21, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwalimu, tatizo kubwa la hizi talking point ni kwamba wapo watu wengi sana wameibeba na wanaamini maneno hayo. Tena kibaya zaidi sio watu wa nje isipokuwa waliokamatwa ni wanachama wa CUF, Chadema na CCM..
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  Aug 21, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Haya hayakuanza leo na victim mkubwa ilikuwa ni CUF.

  CCM kwa kuhofia nguvu za CUF walisambaza sumu ya udini kwa upande wa Bara na Uarabu kwa kule visiwani kwa vile uislamu ungeisaidia CUF.


  Kibaya zaidi vyama vya upinzani kwa kuona nguvu ya CUF dhidi yao vilitumia karata hiyo na wala si uongo kuwa hali hii iliwasaidia CHADEMA. Watanzania waliochoka na CCM hawakuwa na jinsi bali kubaki CCM au kujiunga na CHADEMA. Hili la sasa hawakulitegemea CHADEMA kuwa litakuja kuwala nao na sasa linawala. Kanisa na watu wake wako wazi kuunga mkono CHADEMA na hivyo waislamu wanashindwa kukiamini na hivyo waende upande wao au wabaki CCM.

  CCM ni mkosefu zaidi hapa kwani Waislamu wengi wataunga mkono CUF na Wakristo wengi watakuwa CHADEMA. Hili la kukataa udini kwa vyama viwili hivi ni kuukataa ukweli.
   
 18. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #18
  Aug 21, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Tunakumbuka shuka asubuhi? Tulikuwa wapi chama kimoja kilipoinamiwa na tuhuma hizo? Binaadamu ana tabia ya kuamini iwapo atakuwa akisikia jambo kila mara. Tukivumisha CUF kuwa ni cha Waislamu sasa tukitegemea nini? Jawabu ni rahisi, Wasio waislamu wakichoka CCM wataenda CHADEMA na Waislamu wakichoka CCM wataungana na wenzao na sio wenye itikadi tofauti.
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Aug 21, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu jaribu kutazama pia upande wa pili wa sarafu hiyo hiyo.. wakati wanaCCM na Chadema wakiamini maneno ya viongozi wa CCM kuhusiana na CUF... wanachama wa CUF nao walianza kuamini kwamba CUF ni chama chao Waislaam.

  Rudia mabandiko mengi humu ya wana CUF ni kichefuchefu kitupu yaani wamekumbatia kuamini kwamba CUF na Zanzibar ya Waislaam. Yaani vyama vyote hivi vya Upinzqani vinatakiwa kuamini kwamba vyama vyao na vingine havina mahusiano na dini fulani lakini kama tutaendelea kutuhumiana basi bila shaka kwa mila na desturi za kimaskini siku zote tutamtafuta mchawi mtu mwingine na sio sisi wenyewe.
   
 20. Mkimbizi

  Mkimbizi JF-Expert Member

  #20
  Aug 21, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa huku kwetu,, mimi nilimchagua mzee wangu mmoja wa CUF sababu:-
  1. Ni mpenda maendeleo pale mtaani
  2. Kila shida ikitokea anakuwa wa kwanza kufuatilia
  3. Ni mtu wa watu

  Kilichotokea....
  Jamaa anaishi maisha ya chini, nyumba mbovu(haijaisha) na aligombea toka 2000 kwa CUF, ni muislam... Mimi nilimpigia kura kutokana na juhudi zake mtaani, mwenyekiti wa serikali za mtaa wa CCM hajawahi hata kukanyaga huku chini zaidi ya kuweka kontena ofisini kwake na kusign forms za wanachuo za mikopo!!!!

  Sababu mtaani wananifahamu vizuri, siku ya matokeo wakanitania..."Baba Abuu ameshinda bwana",, nilifurahi sana... Baadae nikaambiwa kuwa,, "Ashinde yule? na CUF yake nani ampe?" NILIHUZUNIKA SANA NIKAGUNDUA KUMBE KUNA WAPUZI WENGI SANA TUKO NAO AMBAO WANACHAGUA SURA NA DINI YA MTU SIO MATENDO!!

  Mpaka leo Baba Abuu namkubali kwamba anafaa kuwa kiongozi sababu ya moyo wake wa kupenda kutumikia, na mwenyekiti wa sasa simkubali kabisa..

  Tuache mambo haya jamani,,, Dhambi ya ubaguzi itatutafuna
   
Loading...