CUF Ndani ya Bukoba Leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF Ndani ya Bukoba Leo

Discussion in 'Jamii Photos' started by Kaa la Moto, Jul 22, 2009.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wakuu leo CUF wametinga Bukoba mjini katika kampeni yao ya "Zinduka".
  Leo jioni Kiongozi wao Lipumba atakuwa akihutubia kwenye viwanja maarufu vya Uhuru.
  Naona wamepita msafara wao muda mfupi tu uliopita ukiwa mdogo sana kiasi ambacho haijazoeleka hapa ukilinganisha na nyakati zilizopita walipokuwa wakitikisa mji kwa maandamano makubwa.
  Ngoja tuisubiri hiyo jioni tuone watakuwa na yapi!


  IMGP8115 i.jpg
  Msafara wa kafu Leo.

  PICT9133 i.jpg
  Msafara wa kafu kwa mara ya mwisho siku zilizopita.

  Picha zingine unaweza kuangalia thread zilizopita!
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wana mageuzi kazi tunayo, ila wakati mwingine inawezekana kutoa taswira ya kitu kwa jinsi utakavyo. Unaweza chagua pa kupiga picha ili kutoa kile unachokitaka na si ukweli uliojiri.
   
 3. K

  Konaball JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,767
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Mwaka huu tutasikia mengi na kuyaona mengi mwisho wake CCM itazidi kutawala na kutugandamiza daima
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Siku zote nimekuwa nikitoa picha za haya matukio kama zilivyo. Na mara zote kwenye haya sipendi kuwa biased maana kama kuna mtu ana picha tofauti anaweza kuweka zilizo sahihi na hii itakuwa aibu kwangu.
  So, hii ndio taswira sahihi. Sina haja ya kuleta taswira ya uongo. Itakuwa kwa hasara yetu wenyewe. Haya ufanywa na sisi maf.....
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  hizo ndio siasa. Vita ya panzi furaha ya.......................
  Lakini nadhani kwa siasa za huko Bukoba ninavyozijua, kafu wana kazi ngumu kurudisha waumini wao upya. Shida udini. CUF=CCM=UDINI
   
 6. L

  Lukundo Member

  #6
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tukubaliane tu kuwa,Cuf wamepoteza mwelekeo, hasa pale wanapofanya kameni za matusi dhidi ya chadema, wanakuwa kama wanajichimbia kisima. MMEONA, mzee mtei alivyomjibu Lipumba katika gazeti la Raia mwema. kazi wanayo.
   
 7. K

  Kenge (Eng) JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2009
  Joined: Dec 7, 2006
  Messages: 502
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  [COLOR="Black"]Nimebahatika kuwa Bukoba takribani wiki mbili sasa na huo msafara nimeuona. Hapa Bukoba hawa watu hawana chama ila wana watu wao. Kila aendako wanaye, ukweli CUF hapa Bukoba wamefulia, huyu Bwana mkubwa Lipumba angesubiri hili wimbi lipite lakini kama amependa kupima upepo sawa.
  bahati mbaya sitapata nafasi ya kuhudhuria mkutano wake.[/COLOR]
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nimekuwa kwenye mkutano kwa muda mfupi sana. nimesikia mambo kidogo tu.
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Unfortunately sikuwahi sana kufika mkutanoni maana nilikuwa safari kwenda Bukoba na nimefika nimechelewa sana.
  Nimekuta Mh Duni keshamaliza kuhutubia, na mbunge wa viti maalum Mh. Saverina nilikuta kamaliza kuhutubia na nilikuta Mh. Lipumba akihutubia na ku address suala la mahakama ya kadhi.
  Alitoa historia na akajaribu kueleza jinsi ambavyo haina shida maana nchi nyingi wameiruhusu na haijawaletea tatizo lolote.
  Alijaribu kulaumu chama rafiki yao sisi maf..... kwamba waliweka jabo hili katika ilani yao ya chama na sasa wanawapiga danadana waislamu na kuleta mtafaruku.
  Niligundua kuwa yeye ni supporter wa hii kitu inaitwa MYK. Hakuwa na la maana upande huo.
  Akarukia suala la umaskini na kushindwa kuiendeleza nchi kwa awamu ya kwanza ya Kikwete huku akidai kwamba katika awamu hii amekuwa ni mtu wa kusafiri kwenda ulaya kila siku bila kujali wananchi wake wanashida kiasi gani.
  Akatahadharisha wananchi kuwa kama wakimpa awamu nyingine Kikwete basi wajue atahamia nje moja kwa moja na hayo wanayoita maisha bora hawatoyaona.
  Akasema anashangaa kuona kwa miaka hii mitano nchi imejenga barabara za lami chini ya kilometa 50 tu.
  Hapo ndio ukawa mwisho.
  Niliododosa nikaambiwa kuwa yalizungumzwa mambo yale yale ya ufisadi, rada n.k.
  Mwisho alizungumzia uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi wa kumi akiwataka wananchi wasiache kujiandikisha kwenye daftari la kupigia kura mitaani, na wasisahau kulinda kura zao hadi mwisho.
  Alitahadhalisha kuwa ni upuuzi kwenda kulalamika baada ya uchaguzi kwa sijui nani na nani wakati mna hakika mmeibiwa kura.
  Aliwahimiza wananchi kwamba kama mtu atachezea kura zenu mshughulikieni pale pale kituoni. Hamna haja ya kwenda kweingine maana hakuna atakayewasikiliza na kuwasaidia.
  Hapakuwa na neno lolote kuhusu mbunge aliyehama katika chama chao kuzungumzwa.
  Hata hivyo watu walikuwa wengi ingawa si kama kawaida ya mikutano ya zamani.
  Baada ya mkutano niliwasikiliza watu wengi wakizungumza hili na lile, lakini ninaweza kumaliza kwa kusema kuwa hali ya kafu hapa Bukoba haitabaki kama kawaida. Sidhani kama ziara hii imeleta mabadiliko yaliyokusudiwa.
  Wanaweza kusema lolote lakini huu ndio ukweli ambao wana kafu itabidi wabaki nao. Wakibisha wangoje majibu yaja.
  Hapa ni picha kidogo nilizopata:
  IMG_1311 i.jpg

  IMG_1312 i.jpg

  IMG_1313 i.jpg

  IMG_1315 i.jpg

  IMG_1316 i.jpg

  PICT0002 i.jpg

  PICT0003 i.jpg

  PICT0005 i.jpg

  PICT0006 i.jpg

  PICT0008 i.jpg
   
 10. K

  Konaball JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,767
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Hii ndio siasa za watanzania nakumbuka enzi ya NCCR Mageuzi walipopotea wakaibuka CUF na wameanza kupotea wanaibika CHADEMA, OMBI kwa watanzania wenzangu tusiwe na SIASA za kushabikia chama kama SIMBA na YANGA, sisi tunachotakiwa kuwakataa wanaiharibu nchi yetu,
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Na si rahisi kukataa bila kupitia vyama vya siasa sijui kama unaelewa hili? au kwa makusudi unajaribu kulifumbia macho?
   
 12. m

  malimi katoro JF-Expert Member

  #12
  Dec 6, 2015
  Joined: Mar 31, 2015
  Messages: 341
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Kesha sepa
   
Loading...