CUF nao wamshukia Nnauye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF nao wamshukia Nnauye

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 16, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2]16 AUGUST 2012[/h]Na Grace Ndossa

  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimedai kushangazwa na kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye kwa vyombo vya habari kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeingia mikataba ya kifisadi na wafadhili wa nje ili kupora rasilimali za nchi.

  Taarifa iliyotolewa Dar es Salaama jana na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Bw. Abdul Kambaya, alisema Bw. Nnauye hakupaswa kuishtaki CHADEMA kwa wananchi bali kupitia Serikali yao walipaswa kuzuia fedha hizo na kuwataja wafadhili hao.

  “CUF kimeshangazwa na kauli hii ambayo imetolewa na msemaji wa CCM, ambacho ndio chama kinachoongoza nchi, tulitarajia Bw. Nnauye angewataja hao wafadhili wa CHADEMA ambao dhamira yao ni kupora rasilimali za nchi,” alisema Bw. Kambaya.

  Aliongeza kuwa, chama hicho kinaamini CCM na CHADEMA ni watoto wa familia moja ambapo wafadhili wao ndani na nje ya nchi pia wa aina moja.

  “Kama CHADEMA imeingia mikataba ya kupewa mabilioni ili baadae wataposhika madaraka waweze kulipa mabilioni hayo kupitia rasilimali za nchi basi watakuwa wanaendeleza utaratibu wa CCM kuingia mikataba mibovu isiyo na tija kwa Watanzania,” alisema.

  Alisema CUF inaamini kuwa, tatizo lililopo nchini ni mifumo mibovu inayoendesha Serikali, nchi, kukithiri kwa wizi, matumizi mabaya ya fedha za umma na ukiukwaji wa haki za binaadamu.

  Bw. Kambaya alisema, sababu ya Watanzania wengi kuwa maskini wa kutupwa, ukosefu wa huduma bora kwa jamii, kudumaa kwa maendeleo ya nchi na ukosefu wa ajira ni matokeo ya muda mrefu yanayosababishwa na mfumo mbovu uliopo.

  Alisema njia sahihi ya kulinda rasilimali zilizopo na zinazoendelea kugunduliwa nchini Serikali ya Umoja wa Kitafa ambayo itashirikisha vyama vyote vyenye wabunge.

  Aliongeza kuwa, kwa kuzingatia utaratibu huo hakuna chama ambacho kitakuwa na maamuzi yake katika matumizi ya rasilimali na Maliasili za nchi.

  “Sisi tunataka Watanzania waelewe kuwa, mazingira yanaonesha CHADEMA kimeizidi kete chama tawala kwa kuwa na wafadhili wa nje ndio maana CCM Inapiga kelele,” alisema.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Poor Nape Nnauye... Hakuna wa CCM yoyote wa kumuunga Mkono? wanamtelekeza ...

  Sasa ajiangalie... ajisome... ajue kuwa uropokaji hana backup... katibu mkuu wake ndio huyo bubu...

  Yule Mropokaji Mwingine naona anaogopa inasemekana atamwaga Unga kwenye CC - Mwingulu Mchemba.
   
 3. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  sasa hawa nao si ndio wamesusia sensa?
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mpaka mke wao kawashitukia...duuuuh
   
 5. M

  MTK JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  "Sisi tunataka Watanzania waelewe kuwa, mazingira yanaonesha CHADEMA kimeizidi kete chama tawala kwa kuwa na wafadhili wa nje ndio maana CCM Inapiga kelele na kuweweseka," alisema.

  Well spoken!
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nape alisema mwenyewe au aliagizwa?
   
 7. KML

  KML JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 863
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ukiona adi mke wako anakushukia basi ujue we umefeli...
  POOR CCM
   
 8. r

  ray jay JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 60
  Hivi hiki chama bado kipo?au ndo kinataka kupata umaarufu kupitia mgongo wa nape...
   
 9. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  nape ni ubao wa shabaha kila mtu anajilengea tuu
   
 10. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Kauli ya nape ni ya kulaaniwa na chama chochote cha siasa hata hao ccm inatakiwa wampinge ,vinginevyo athibitishe kauli,Nape aliwehuka baada ya kuona michango imekuwa mingi
   
 11. D

  Dabudee Senior Member

  #11
  Aug 16, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hata akibaki peke yake CCM haiwezi kufa
   
 12. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nape anajifanya anajua kuongea kumbe hajui asemalo
   
 13. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Ahaa! Kumbe CUF nao wapo eeh! Maaana niliwasahau kidogo hasa katika mijadala inayoligusa Taifa kwa sasa! Siwasikii. Ni CCM Vs CAHDEMA tu!
  CHADEMA msijali, CUF tunamtumia kuzigawa kura za CCM.
   
 14. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,454
  Trophy Points: 280
  **** propaganda by Nape has yield all the barrage of abuse from every corner.

  Still, ccm will come with an even worse propaganda in the vain hope of covering Nape's face. Where is Makamba Snr?
   
 15. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #15
  Aug 16, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani muda umefika wa kumpuuza Nape Nnauye. Anaropoka mno.
   
 16. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Wafadhiri wa nje wanaingia mikataba na cha UPINZANI kupora rasilimali za Tanzania?

  Am I missing something?

  Au Nape anataka kuwaaminisha kwamba 2015, CCM ndiyo itakuwa chama cha upinzani, ndiyo maana wafadhiri wa nje they don't give them a damn shit.

  Hongera Nape kwa kukubali kushindwa, at least umeonesha kukomaa kisiasa
   
 17. Man 4 M4C

  Man 4 M4C JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 737
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kijana hana jipya yeye ni gamba ndani ya magamba''A dog having teeth will never to its master''
   
 18. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #18
  Aug 16, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Nape ni janga kwa vijana kama jinsi ccm ilivyokuwa janga kwa watanzania.
   
 19. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #19
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,728
  Likes Received: 12,797
  Trophy Points: 280
  Hawawezi kumuunga mkono mropokaji

   
 20. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #20
  Aug 16, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,170
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Mukama aliwahi kusema "chadema wameingiza magaidi kutoka libya, afghanistan na somalia" kilikuwa kipindi cha uchaguzi wa Igunga, like a father like a son!
   
Loading...