CUF na Operesheni "Zinduka"

Mwiba,
Pamoja na kuheshimu kila mtu hapa JF, nilikwisha kusema, tusiendekeze hisia na majungu. Kama kuna mtu anafikiri Mzee Mtei aliiba, ashushe hapa. Tuna mambo muhimu zaidi ya kujadili kuliko hisia. Halindwi mtu, hata kama angelikuwa nani katika masuala ya ufisadi, lakini tusifanye JF kama mahali pa mjadala bila lengo, we need to do justice to this nation. Yeyote mwenye facts, aje clearly ili tujadili vema hoja, kuliko "unfounded" allegations.
 
Mkuu Slaa
Mwiba ana mission ya kuendeleza mawazo ya wale wazee wa vibandiko hana hoja tuendelee na mjadala na umeweka wazi aje na facts na aweke hapa kama hana apishe tuendelee na mapambano .
 
Mwiba,
Thanks once again. Sina sababu ya kubishana nayo. i) Hoja ya Ukabila ndani ya Chadema ni wimbo usio na mshiko, labda ubaki nayo wewe na kundi lako la mashabiki. 2) Hoja ya Mashamba na Risasi, kama unayosema ni kweli makosa ya kijanai au ya madai kwa mujibu wa Sheria za nchi, siyo mambo ya ushabiki. Inaelekea uko tayari kudaka chochote, hata kama huna facts. Hearsay, ndiyo inayoua nchi. I hope we and pray we are more serious katika serious issues and argue issues with facts, rather than emotions and propagandist approach. Nchi hii inahitaji watu serious kuitoa kutoka kwenye lindi la matatizo na siyo kwa njia hii. JF may may contribute to this cause if utilized optimally.
 
Mhesh Slaa; kwanza pole sana na majukumu ya kila siku; pili huyu Mwiba achana nae huyo hana hoja zaidi ya propaganda kama ulivyosema; na bahati mbaya muda wote anazifanyia ktk keyboard tu mpaka mimacho inamtoka wakati wenzake wanaenda on the battle ground; so they will not yield anything than wasting his time; one with no fact has no right to say.

Nina neno Mkuu;

Chadema ni chama chawa WaTZ wote; na sasa kiwezeshwe kimkakati kuwa cha umma zaidi na kweli; kwa kuongeza kasi ya uhamasishaji ktk maeneo lengwa; yaani sasa zichorwe ramani za kitafiti; kujua ni sehemu gani tunaenda kuna nini na tutapata nini; then kila mahala palipo lengwa patoe majibu kusudio ( nahisi umenielewa MH). I meana ukisema tunaenda Busanda kuchukua serikali za mitaa; biharamulo; mbeya mjini/vijijini; bukoba; karatu; mara yote nk; then mnajua kweli mnaenda kuchukua viti hivyo; msiumize kichwa kupeleka resource nyingi sana sehemu ambazo hamna mategemeo; utaratibu huo ulimwezesha Obama kushinda vema; sio lazima ushinde nchi nzima; i la ushinde sehemu kubwa ya TZ; sehemu zenye ushawishi michango watu watatoa ili kukiwezesha chama kusonga mbele hilo ninalo hakika so itafanikiwa maana najua resource za vyama pinzani kwa kweli hazitoshi na imekuwa hivyo kwa makusudi ya watawala;

Asante;
 
naomba muongozo wenu wana JF wenzangu
1)ni jinsi gani naweza kuwa Premium Members?
2)nilikuwa nataka kusoma pale kwenye MAMBO YA KIKUBWA ila kuna warning kwamba ni lazima nitume maombi kupitia PM to invisible sasa wakuu sijui hata pakutumia hayo maombi naomba muongozo wenu.
asanten sana am a new member.
 
Malunde Malundi,
Ushauri umepokelewa kwa mikono miwili. Kwa kuwa sitapenda kumwaga hadharani, nadhani utafuatilia utekelezaji kadiri muda unavyoenda....Nakushukuru sana.
 
Malunde Malundi,
Ushauri umepokelewa kwa mikono miwili. Kwa kuwa sitapenda kumwaga hadharani, nadhani utafuatilia utekelezaji kadiri muda unavyoenda....Nakushukuru sana.
 
Inawezekana labda tunatofautiana kimawazo ,pengine target yangu ipo mbali sana na inakuwa vigumu kuweza kuiona kwa vile inakuwa imejificha.

SIna elimu kubwa sana ya kuweza kuchunguza mtu,au kumfuatilia mtu,kwanza wakati huo sina ,isipokuwa huwa nadondoa dondoa humu humu na mengine kwenye magazeti na mengine kupitia redio.Na hivyo ninakuwa na dondoo ndogo ndogo ambazo kwazo huwa nazikumbukia tu.Na hata kuthibitisha kuwa jambo fulani limetokea kwa kudhihirika kwa mwenyewe aidha katika utetezi au anapohojiwa na kugusiwa yanayomuhusu.

Sasa ninaposema kuwa fulani alihusishwa na kutaka kumuua mtu (Ndivyo ilivyopokewa) kutoka upande mmoja wa aliekusudiwa kuuwawa kutokana na madai yake.
Kesho yake unakuja kusikia kuwa yule aliemlenga mtu risasi na kutaka kumuua anagombea uraisi anagombea ubunge na jinsi ya hayo ,sasa hapa ndipo linapokuja suala la uadilifu ,hii au hapa ni very sensitive issue ,na kwa wenzetu wa Marekani nadhani unakuwa dismissed tokea ndani ya chama chako ,hufai kabisa hata kama ulijitetea sijui wanatumia vipimo gani lakini nina uhakika wa hilo kuwa huwezi huwezi kabisa kugombea .maana ukipima hata kama una mambo ya kutongoza tongoza wanawake ,basi jamii wenzetu inashawishika katika kukutenga kwa kukuona hufai kuongoza.unahusikahusika na mambo fulani fulani labda ya ufisadi au rushwa yote hayo huwa yamo katika list ya kutokufanya kuwa hufai.

Sasa hapa kwetu sishangai kwa kuwa bado hatujafikia kiwango cha wenzetu katika kupashana habari,kiwango na hitimisho la habari yenyewe navyo vinakuwa na kubakia kama siri isiyokubalika au inayotakiwa isijulikane na wananchi wapiga kura. Hili ni tatizo katika kumpata kiongozi alie mwadilifu na ambae atawajibika katika kutenda haki kutokana na historia na tabia za mtu huyo anaetaka kuwa Raisi , Ukimuondoa Mwalimu Nyerere ,Ali Hassani Mwinyi waliobakia wote wana matatizo na tumeona na tunaona ni jinsi gani NCHI hii inavyoendeshwa ,yote hayo ni kutokana na kufichwa kwa mambo ambayo yanatia walakini tabia zao, Ukiangalia uchaguzi wa Marekani uliopita kampeni zilikuwa moto sana na mahojiano ya wazi kabisa yakiendeshwa katika kumbi mbali mbali ,tokea ushindani ndani ya Chama kimoja hadi kufikia ngazi ya vyama tofauti.
Masuala ambayo yakiulizwa ni mengi na ni madogo na makubwa ,kiasi ya kwamba mengine yakigusa personal life.

Leo hii hapa Tz viongozi hawana ushindani ndani ya vyama vyao ,labda tunategemea kwa siku zijazo mambo ya kugombea nafasi nyeti kama ya Urais yaanze kwa ushindani ndani ya Chama mkoa hadi mkoa kwa kumtafuta mgombea wa Uraisi wa Tz kwanza ndani ya Chama chenyewe tuachane na yale mambo ya kukutanika ndani ya ukumbi na kuchaguana ,inakuwaje inawezekana kwenda popote pale na timu nzima kwa ajili ya uchaguzi wa mbunge.

Nimetoka nje ya mada ila kinachojitokeza kwa sasa ni viongozi hawa wanaokimbilia kugombea nafasi ya Uraisi wa Tz kutumia umaarufu wao ndani ya mipaka ya Chama chao na kuwa rahisi wao kupita.

Cha ajabu kabisa ni kuwa viongozi hawa huwa wana madoa ambayo hayafai kwa mtu anaetaka kuongoza watu ,tabia zao ni mbovu ingawa wanaweza kuwa na personality nzuri ,good appearance na hata maneno yao yanaweza kuonekana ni mazuri na mepesi kuchukulika ,lakini mtiririko wa mambo yaliopita kwa nyakati tofauti ni vina ambayo vinatakiwa kupimwa katika kugombea nafasi ya uraisi vinginevyo itakuwa kunatumika ubabe tu na kujipatia madaraka yasio na faida kwa watawaliwa waliowengi.
 
Mwiba wewe ndiye meneja wa propaganda wa kafu?
Tangu asubuhi hadi usiku wa manane tunakuacha upo hapa na asubuhi twakukuta je unalala saa ngapi? na kazi za kipato kingine unafanya saa ngapi.
Au ni kwako ndiko zile pesa za kafu waliwekeza na sasa unakula kidogo kidogo na maalim seif?
 
kwa kweli ushahidi wa humu unaonesha wazi kuwa jadili ccm,cuf,TLP n,k lkn chadema usijadili.. duh! kwa kweli nimejaribu kusoma hoja zinazotolewa na kanda2,mwiba,chuma ni hoja za mantiki na nikiangalia majibu kama ya mzee slaa na mzee mtei bado sioni hoja wanazojibu kama zinakidhi majibu sahihi, na nikiangalia wachangiaji wengi hapa naona wamo tu,alimradi chadema isijadiliwe.. haya tuone... au twambieni tu kama hii JF ni ya chadema tujue..
 

Mbona hushangai kina Halisi, Invisible, Mwanakijiji? mwache ajitanue. Kwani we hujui kwamba majina mengine ni taasisi, watu wanaingia kwa shifti 24/7. Na tayari maelekezo yapo mikononi mwao. Hilo si kosa ndio maendeleo, na inatakiwa kila chombo/chama/idara wawe na watu wanaofanya kazi ya kujibu hoja na kutoa changamoto katika JF ili iendelee kuwa LIVE muda wote.
 
HALISI,
UMEENDA CHUO BABA... Nahitaji kutafuta elimu kutoka kwako
 

Kwa Invisible iliwahi jibiwa humu wako wawili. Lakini kwa Halisi na Mwanakijiji sikujua kuwa ni Taasisi basi wako kibao wamepangiana muda kuchangia ama kujibu hoja. Shukrani kwa taarifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…