CUF na Maalim Seif Wajiandae na Propaganda ya Kula Mabilioni Kunyamazishwa

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Nina wasiwasi sana juu ya mstakabali wa Cuf na Maalim kisiasa.Lazima maalim seif achukue hatua stahiki baada ya Ccm kupuuza mazungumuzo na kuwapuuza wahisani.

Endapo hatochukua hatua,Upo uwezekano wa Ccm kuibuka na propaganda juu ya seif siku za usoni.Si mnakumbuka walipoibua propaganda kuwa Lowassa kainunua CDM?Ni uimara wa Chadema ulizima hoja hiyo.La sivyo baadhi ya wafuasi walishaingia kingi.

Sasa Wakati wowote wanaweza kuibuka na kusema Maalim alinunuliwa na kuwasaliti wa Zanzibar ndio maana kawa mkimya tofauti na miaka ya nyuma alipokuwa akionyesha mapambano ya kiharakati.Siasa za harakati zina ushawishi,Totauti na za mipango.

Na kama Cuf watashindwa kukabiliana na propaganda hiyo,Inaweza kuwaletea madhara siku za usoni.Maana watu wanatofautiana kufikiri na watanzania wengi hupenda kusikia tu na si kutafakari.

Tochi yangu imeliona hili ni lazima Cuf wajiandae si la kupuuza.
 
Tatizo znz walioikataa ccm siyo seif bali wananchi ni vigumu kuwabadili wananchi uliowadhulumu haki yao ya kikatiba
Viongozi wanastahili kuja na mstakabali wa znz baada ya tukio.Wakiendelea kumsubiri mmarekani,Ukimya wao utageuzwa mtaji wa kisiasa.Watanzania wanachoteka kirahisi sana
 
uzuri wake wazanzibar wako imara sana kiakili , na kwa vile umekwisha lileta hapa basi ni kama umefumua siri za wachumia tumbo hawa akina lizaboni , usikute kumbe walikwishaandaa tayari uongo wao .
 
Viongozi wanastahili kuja na mstakabali wa znz baada ya tukio.Wakiendelea kumsubiri mmarekani,Ukimya wao utageuzwa mtaji wa kisiasa.Watanzania wanachoteka kirahisi sana
ni kweli pamoja na ukweli kwamba maalim anaaminiwa sana zanzibar na ndio maana taarifa za kimataifa zinasema waliojitokeza kupiga kura za marudio walikuwa 58,000 tu , lakini anatakiwa kutoa TAMKO LA KIKAKAMAVU ( plan B ) kuhusu hatma ya zanzibar .
 
uzuri wake wazanzibar wako imara sana kiakili , na kwa vile umekwisha lileta hapa basi ni kama umefumua siri za wachumia tumbo hawa akina lizaboni , usikute kumbe walikwishaandaa tayari uongo wao .
Kama lizaboni ni mpishi mbaya sana wa propaganda,Alipika majungu mengi juu ya lowassa lakini Vijana imara wa CDM tulimdhibiti kabla ya madhara.
 
Usafi wa Maalim hakuna katika Tanzania yote anaye mfikia.... hana Tamaa ya fedha wa shida ya kuhongwa hilo halina nafasi yeye hata nyumba hana na alikua kiongozi mkuu tu tangu Nyerere lakini.

ccm wajitayarishe kisaikologia kuwaponza wazanzibar juu ya hio njaa ilo semwa na Aboud Mohamed
 
Kama lizaboni ni mpishi mbaya sana wa propaganda,Alipika majungu mengi juu ya lowassa lakini Vijana imara wa CDM tulimdhibiti kabla ya madhara.
chadema ni habari nyingine mjomba , huyu lizaboni pamoja na kwamba analipwa zaidi kuliko wengine kama bakshishi ya kumtukana lowasa lakini kwa cdm amegonga mwamba , Bavicha kiboko !
 
chadema ni habari nyingine mjomba , huyu lizaboni pamoja na kwamba analipwa zaidi kuliko wengine kama bakshishi ya kumtukana lowasa lakini kwa cdm amegonga mwamba , Bavicha kiboko !
CHADEMA ilikuwa zamani enzi za akina Zitto na Dr Slaa! Hii ya akina Kingunge na Lowassa ni nyingine kabisa!
 
Lowassa ameiangamiza CHADEMA mkuu! Hebu mwambie Mbowe atamke neno "Ufisadi" kama ataweza!

Mwenye mamlaka ya kumshitaki fisadi lowassa ni DPP wa ccm, sasa kinachonichosha ni kuwa ccm inamwogopa lowassa kuliko wanavyoogopa ukimwi, polisi,jeshi, mahakama na usalama wa taifa vyote mnavyo sasa kinachowashibda ni nini kumshitaki lowassa japo afagie kama wakina mramba
 
Kama lizaboni ni mpishi mbaya sana wa propaganda,Alipika majungu mengi juu ya lowassa lakini Vijana imara wa CDM tulimdhibiti kabla ya madhara.

.......mpaka Lowasa akachukua nchi. !
 
Aisee wabongo bwana kwahyo thread imeuwa ya lowasa na chadema wakati inazungumzia ukimya Wa maharim
 
Back
Top Bottom