Ufunguzi wa mkutano wa kumbukumbu ya maisha ya Maalim Seif Sharif Hamad

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,747
885
UFUNGUZI WA MKUTANO WA KUMBUKUMBU YA MAISHA YA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD.

- "Nimesimama mikutano mingi kuongea na mingine ya kimataifa. Lakini sijaona ugumu kama naouona katika mkutano huu"

- "Enzi za uhai wake, Maalim Seif alikuwa ni makutano ya watu, alikuwa ni kiongozi wa watu na alitokana na watu na watu walimshiba. Na huyo ndiyo Maalim Seif na watu kukutana leo kumkumbuka siyo jambo la ajabu"

- "Pamoja na kwamba Maalim Seif alifanya kazi ya ualimu hata kuitwa maalim, umaalim wake ni wa kipekee kutokana na kuwa hakuwa tu mwalimu wa wanafunzi bali pia alikuwa ni mwalimu wa watu"

- "Maalim Seif alikuwa na uthibiti wa msimamo wake na alikuwa na utayari wa maridhiano hata pale unapotokea msigano. Na amefanya kazi hii ndani ya chama chake na katika vyama vingine"

- "Tunaomfahamu Maalim Seif hata wakati akiwa CCM, enzi za chama kimoja alipokuwa na jambo alisimama na kuongea, na msimamo huo huo aliuendeleza hata alipohama na kuanzisha Chama cha Wananchi (CUF)"

- "Maalim Seif Sharif Hamad alituheshimu na tulimuheshimu, hata alipotupinga hakuwa mwenye kutukana bali alitupinga kwa hoja"

- "Utayari wa Maalim Seif Sharif Hamad wa kuangalia maslahi mapana ya Taifa ndiyo ulifanya hata maridhiano yakapatikana na kufanya CCM na ACT Wazalendo kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa"

- "Hatuwezi kuizungumzia amani ya Zanzibar bila kumtaja Maalim Seif Sharif Hamad, Maalim Seif alikuwa ni daraja la amani na alitanguliza maslahi ya taifa mbele"

- "Kama kuna somo Maalim Seif Sharif Hamad alilotuachia kwetu wanasiasa, ni kuwa tayari na kuwa na masimamo wa kutafuta maridhiano kwa wale ambao unakuwa na tofauti nao"

- "Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa na mchango mkubwa wa mageuzi ya kisiasa na kiuchumi Zanzibar, alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa mstari wa mbele kupigania kurejeshwa mfumo wa vyama vingi kuanzia mwaka 1989 hadi 1992"

- "Siku za mwisho za uhai wa Maalim Seif alihubiri ujumbe wa maridhiano na umoja wa kitaifa kokote alipopita, tutakumbuka alifunga safari yeye na Rais @DrHmwinyi kwenda kumuona Rais Hayati John Magufuli ambapo alisema utulivu na amani ya nchi ndio jambo la muhimu"

- "Ni mtindo mzuri kuenzi waasisi wetu walioleta mchango mkubwa kwa Taifa letu. Ni jambo zuri. Na njia pekee ya kumuenzi Maalim Seif ni kuenzi Umoja na Mshikamano uliopo"

IMG-20211105-WA0034.jpg


IMG-20211105-WA0032.jpg


IMG-20211105-WA0030.jpg


IMG-20211105-WA0031.jpg


IMG-20211105-WA0006.jpg


IMG-20211105-WA0007.jpg


IMG-20211105-WA0016.jpg


IMG-20211105-WA0019.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom