CUF na CCM Zanzibar wana ajenda ya siri

CUF na CCM Zanzibar wana ajenda ya siri

ibange

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2010
Posts
1,543
Reaction score
553
Kuna bwana mmoja wa Cuf Znz nilikuwa nazungumza nae amenifungua akili. Nilimuuliza kwanini CUF kimetungusha hivyo na je CUF ni chama cha wazanzibari tu mbona wanasema maslahi ya Znz yamelindwa kwenye mswada wa katiba wakati chama kipo hadi bara? Aliniambia Znz walichofanya ni kuitega serikali ili wao znz wapewe meno kwenye mchakato. Wakishapewa meno watashinikiza mambo yao mengi yapite. Na ni kweli znz lazima kwenye bunge waunge mkono theluthi 2 na kura ya maoni asillimia 50. Mambo ambayo watayataka walalazimisha yaingizwe na kutishia kuipinga katiba kama hayatazingatiwa ni kama yafuatayo:
(i) Kupunguza mambo ya muungano yabaki kama yalivyokuwa wakati wa muungano
(ii) Kuundwa kwa serikali tatu
(iii) Znz kuruhusiwa kujiunga na jumuiya za kimataifa kama OIC, EAC nk kama nchi
(iv) Rais wa znz kuwa makamu wa kwanza wa rais
(v) Urais wa muungano kuwa wa mzunguko nk
(vi) Wabara waingie znz kwa passport

Nadhani wabunge wa CCM waliokuwa wanashangilia bungeni hawaku foresee hayo sasa wao wameshika mpini sisi makali. Hakuna katiba bila wao kukubali na pia wana haki ya kuamua mambo ya bara yawe vipi. kwa mfano jamaa anasema watashinikiza kuwa na mahakama ya kadhi bara na kwa kuwa wanamamlaka ya kutuamulia bara tuwe na mambo gani katiba haitapita bila wao kuamua. lets wait and see
 
Habari za vijiwe vya kahawa hizo hapa si pahala pake,unamaanisha watanganyika wote hawana akili mpk wakubaliane mambo hayo??
 
Habari za vijiwe vya kahawa hizo hapa si pahala pake,unamaanisha watanganyika wote hawana akili mpk wakubaliane mambo hayo??

JF yenyewe ni "kijiwe cha keyboards!" Tuendelee kujadili! Wazanzibari wanampokonya hata JK mamlaka ya kuamua mambo bila kufuata ushauri wa mtu yeyote kwa mujibu wa Ibara ya 34 ya Katiba! This time kwa mujibu wa Sheria aliyoisaini mwenyewe juzi tr 29 Novemba, 2011, atalazimika kwanza "kushauriana" na "kukubaliana" na Rais wa Zanzibar pindi rasimu ya Katiba mpya itakapowasilishwa!
 
Kuna ubaya gani kushauriana na kukubalina na wazanzibar??
 
Rais wa Zanzibar awe makamu wa kwanza wa rais....kwa nini wakati kutakuwa na Rais wa Tanganyika? Je Rais wa Muungano akitokea ZNZ bado makamu wake atakuwa rais wa znz/
 
Crap as usual
Mkuu, I'm sorry to differ with you on this issue. This argument is very sensible. Do not regard it as minor. We mainlanders, with all our boldness, have at last been trapped in the corner. Our clever CCM MPs applauded and passed the bill unknowingly just to annoy CHADEMA MPs as if the new debated constitution does not concern them. Oh, my poor country! Do we really have a future as an independent country?
 
Hii ngoma mtaona mlivyozungukwa vibaya na JK! Tabasamu lake huwa linaficha mengi!
 
CUF si wajinga kiasi hiki.Mtu asiyeona mbali ndie hawezi kuiona nia ya wazanzibari kwenye mchakato
 
Tusuburi leo nini CUF wataongea huko Magogoni hapo ndipo tutajua ni nini lengo lao

Haya mambo kwa kizazi hiki si rahisi kihivyo
 
Wewe binafsi ungeshauri vipi?
Au sisi wote, kabla ya kusema crap au vp, tunapendelea nini?
mimi ningependelea mtu anieleweshe maana ya serikali mbili, nadhani huwa inazungumzwa sana ila sielewei,
pls kama kuna mtu anaejua ubaya wa kuwa na serikali 3, uzuri wa kuwa na serikali mbili na sio tatu anieleweshe.
ubaya wa kuwapo na tanganyika na zanzibar na kila moja iwe na uwezo wa kujiunga na vyama inavyotaka,

ila itakapo kuwa hivyo, basi mambo ya Zbar kuamua mabobo ya Bara yataisha, mambo ya bara kuamua mambo ya Zbar itaisha, vitabaki kujadiliwa mezani hadi muafaka ufikiwe, mimi sioni ubaya hapo,
 
Wewe binafsi ungeshauri vipi?
Au sisi wote, kabla ya kusema crap au vp, tunapendelea nini?
mimi ningependelea mtu anieleweshe maana ya serikali mbili, nadhani huwa inazungumzwa sana ila sielewei,
pls kama kuna mtu anaejua ubaya wa kuwa na serikali 3, uzuri wa kuwa na serikali mbili na sio tatu anieleweshe.
ubaya wa kuwapo na tanganyika na zanzibar na kila moja iwe na uwezo wa kujiunga na vyama inavyotaka,

ila itakapo kuwa hivyo, basi mambo ya Zbar kuamua mabobo ya Bara yataisha, mambo ya bara kuamua mambo ya Zbar itaisha, vitabaki kujadiliwa mezani hadi muafaka ufikiwe, mimi sioni ubaya hapo,

Huo ndio ukweli. Mtu anayeitakia mema Tanzania lazima atapendekeza kuwe na serikali tatu. Swala la gharama si la kweli kwani waziri mkuu aliyepo ndio atakuwa mkuu wa tanganyika, bunge lililopo liltakuwa bunge la bara na wawakilishi wanabaki. Tunaweza kuwa na wabunge wasiozidi mia kwa ajili ya bunge la muungano na wizara za muungano zinabaki zilivyo na zile ambazo si muungano zinakuwa za tanganyika.
 
Very likely..........
Tanganyika ni koloni la Zanzibar long time kitambo mbona!!
 
Hao wazanzibar wanajisumbua tu! hata kama wabunge wa CCM wamekalia kushabikia UCCM badala ya kuangalia Interest za watu wao,lakini mwisho wa siku sisi wananchi tutakataa ujinga huo,waache hao akina duni haji sijui wanajifanya wanaongea sana kwenye TV na kiswahili cha cha vimisemo vingi lakini wajue kuna wengine sisi zanzibar tunawaona kama illegal aliens kwenye Nchi yetu na you will go one day,mmetuchezea vya kutosha inakuwa kama tunawabebembeleza vile,kila siku kutishia serikali Ondokeni tu na nikweli mnaona JK anacheka Mnadhani hajui Njama zenu? Jidanganyeni tu siku mtaiona Mziki wake.Watu wa Tanganyika ndivyo tulivyo wakati mwingine utamuona Mtu anacheka lakini atakumaliza. CUF Iko wapi na Ngangari zake? Mmenyewa kwa maagizo ya Magogoni.

Rais kutoka visiwani hiyo msahau hata Mwinyi hakuwa Mzanzibar!wazazi wake walihamia tu huko! na alizaliwa bara Mlipigwa mchanga wa macho!
 
Thats their country and they should decide their own destiny

whats so wrong wao kuwa na aspirations zao?

Muungano ni kama ndoa, ulikuwa haupo, ukawepo na kama hakuna maslahi na mmoja naona hatendewi haki na maslahi yake hayaendi anavyotaka then unaweza kuvunjwa

Muungano sio sacrosanct au Quran ambayo haiwezi kubadilishwa

wao wana nchi yao na sisi tuendelee kufocus na nchi yenu na mafisadi wetu wanaotuongoza

get over it and move on thats life
 
Back
Top Bottom