Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,760
Amini usiamini CUF ni mshindi wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika 2015 ,kiasi kilichobakia ni kama mwaka na nusu kuanzia kampeni za Uchaguzi ambazo kuna baadhi ya vyama vimeshaanza tokea sasa ikiwemo CCM.
WaTanzania walio wengi wameonesha hisia za hali ya juu kukipa Chama cha CUF ushindi mkuu ambao watabiri wa mambo wanasema haujawahi kutokea.Chama Cha CUF ambacho kwa sasa kimetulia kama hakipo lakini uhakika nilioupata ni kuwa mambo yao yalikuwa yanafanyika ndani ya handaki ,na hatua waliyofikia itawashangaza adui CCM na walokole wengine .
CUF itatinga kwenye uchaguzi mkuu pale tu tume ya uchaguzi itakapobadilishwa na kuwa huru yenye kushirikisha asasi nyengine na kukubalika na asilimia kubwa ya washiriki wa Uchaguzi (vyama vyote vya siasa).Vinginevyo haitoshiriki uchaguzi na hapo ndipo itakapojulikana kama embe ni tunda.
CUF bado inahazina ya wapiga kura wengi kuliko chama kingine chochote kile ,huo ndio ukweli ,tuachane na longolongo za mitandaoni ambazo hazina mshiko. Pia mingi ya mikutano ambayo baadhi ya vyama vimekuwa vinajidai ni kuonyesha nguvu zake kwa wingi wa wananchi wanaohudhuria,vyama hivyo utavikuta vina mipasho mingi tu ,habari ambazo zinakuwa vivutio kwa wahudhuriaji na sio kuwa wao ni wanachama au wanaimani na hicho chama ,habari ambazo hazina tofauti na za magazetini zile zenye vichwa vya habari vinavyovutia wanunuzi,kumbuka tu anae nunua gazet huwa hana share na gazeti wala si memba wa gazeti hilo ,ndio sawa na wahudhuria katika mikutano ya vyama.
CUF ni Chama ngangari hapa Tz ,hilo wengi wenu mnalielewa ni Chama ambacho kinayaweza mapambano ya kisiasa na kimeonyesha nguvu zake na kuitaarifu Dunia ya kuwa kama wakiamua basi wanaweza ,mnakumbuka walichokifanya Zanzibar (Unguja na pia Pemba ,waulizeni polisi watawapa habari na zaidi kilichowapata hao polisi kule Pemba.Ni kuyakataa yanayofanywa na Tume ya Uchaguzi, Hayo ni moja yaliyofanyiwa tathmini kwa upande wa Tanganyika na imeonyesha wazi yanaweza kufanyika tena yakashinda yale ya Zanzibar ,
Yanayofanywa na vyama vingine kwa hivi sasa yote yanatizamwa na kuratibiwa vizuri sana bila ya kuacha kuyafanyia kazi na huko ndiko kulikowapa ushujaa CUF kuwa bado wanachama wao wapo hai na siku filimbi ikipulizwa basi wote wataitikia wito na kuelekeza majeshi katika njia ya ushindi mkuu.
Na kwa wale wanaobeza basi wajue wameshakosea kwani ushindi uko huku ,na hili wanasema ni basi la mwisho ,dandia upande wowote ue utafika kule unakotaka kupelekwa.