CUF kuiteka Zanzibar kwa maandamano

CUF kuiteka Zanzibar kwa maandamano

Yaani mi nashangaa unakuta mambo yote hata watu kumi.hawafiki wamaotaka zanzibar iaribike
 
Huo uchaguzi wenyewe ni kumnyima maalim seif ushindi wakishindwa wao turudie uchaguzi
 
Naona anko magu nae anataka kuanza kuhesabu vichwa. Maana wakiandanana watafuata ile kauli ya pinda tu...nawapigwe tu maana hakuna namna.
 
Ya Burundi yanataka kuanza! Na jana tumetishiwa kwa ndege za kivita! Hakiiiiiiiiiii. Damu ikimwagika itakuwa ni ushahidi tosha kuwa CCM inangangania madaraka!
 
Uhuru wa Kuandamana bila kibali? hawa nao wapigwe tu. Nchi bila taratibu si nchi tena, itabaki kuwa genge la wahuni
Unadhani kupigwa tu ndio suluhu ya madai yao? Uhuru gani kama democracy inaminywa? Miongoni mwa elements za democracy ni free and fair election, transparent na nyinginezo nyingi. Je Z'bar kuna free and fair election? Wa Z'bar wasiposikilizwa nani atasikilizwa kwa maslahi na ustawi wa Z'bar?
 
Kabla kibali hakijatolewa ni lazima mamlaka husika ijilidhishe na dhumuni la maandamao. si kila maandamano yana tija.

Kiswahili sahihi:
ijilidhishe= ijiridhishe
dhumuni= (hii ni common mistake, hakuna 'dhumuni' katika Kiswahili. Siku zote ni 'madhumuni'. "Ma' si kiambishi cha kuonesha wingi, bali ni sehemu ya shina la neno kama vile maziwa (ya ng'ombe), makamu, maji, maslahi....nk.
 
Wako sahihi na wana haki.
sasa hao polisi kwa nini wawapige watu wanaoandamana kwa nini wasiwalinde hao wanaoandamana dhidi ya wale wanaotaka kuleta vurugu? wakiwapiga wanaoandamana hapo siitakuwa polisi ndio wameleta vurugu?
 
Kiswahili sahihi:
ijilidhishe= ijiridhishe
dhumuni= (hii ni common mistake, hakuna 'dhumuni' katika Kiswahili. Siku zote ni 'madhumuni'. "Ma' si kiambishi cha kuonesha wingi, bali ni sehemu ya shina la neno kama vile maziwa (ya ng'ombe), makamu, maji, maslahi....nk.
Nimeisoma, ahsante
 
muandamane bila kibali kutoka polic? Mnakatazwa na police walinda aman mnalazimisha? Mkipigwa mtasema ccm ndo wameamurisha au, jaribun kuheshim sheria jaman na mkiandamana bila kibali mtapigwa tu kwa sababu hamna jinc pengne mmemis virungu vya polic

Mkuu, hii siyo sahihi, shida ya vyombo vyetu vya usalama viko biased. Na siku zote hata kwenye familia mzazi usipotoa haki sawa kwa wanafamilia tegemea vitu kama hivyo. Utatoa maelekezo/ maagizo hayatatekelezwa. Mimi nadhani polisi walipaswa wawaruhusu tu wafanye maandamo, waelezee hisia zao. Police ni kuhakikisha maandano yanafanyika kwa amani bila vurugu. Kwa mtazamo wangu, Uonevu kama huu ndo huwa uanzaa vikundi vyenye misimimamo kama Al shababu, Al Qaeda, ISIS, Boko Harama n.k. Amini usiamini Machafuko yatakapo tokea zanzibar, hawa jamaa (Magaidi ) watajipenyeza tu. na huo ukanda hautokuwa salama milele.
 
Uchaguzi ulio pita Cuf walikubali kwa roho safi tu kuunda serikali ya mseto(SUK) kwa maslahi ya wazanzibar wote.
Kwani nini Ccm msifanye ustaarabu huo? Tamaa mbaya sana na Mungu awalaani wote walio husika na ufedhuli huu.
 
....akiba ya maneno ktk kukumbushana: " vyombo vya usalama ktk nchi zetu za ulimwengu wa tatu kiutendaji, vina mapungufu mno!....Basi na asije mwanasiasa au mfuasi yeyote wa mwanasiasa akajifanza ati kushangazwa na "viroja vya polisi fujo" kazini.........kila la kheri waandamanaji ktk unguja!
 
Vijana wataandamana, Polisi watatumika kupambana na waandamanaji wasio na hata manati, maafa yanaweza kutokea na maisha ya watu yakapotea jee nini kitafuata?
Nionavyo mimi, kwa mara ya kwanza tutashuhudia viongozi wa Kitanzania nchi inayojiita ya amani na utulivu wakipelekwa kwenye mahakama ya kimataifa ya Uhalifu dhidi ya binadamu. Chondechonde ccm acheni kuwaponza wazee wenu hawa, hivi mnaona raha gani mkija sikia wananyea debe huko Ulaya kwa kuwalazimisha wafanye mkitakacho?
Nina uhakika mzee kama Shein hata hamu na haya mambo hana tena na alipenda baada ya kukataliwa kwa kura akajipumzisha na kula pension yake kwa raha mustarehe na Mama Mwema wake. Lakini nyie wabaguzi kwa vile kikiwaka hamtakamatwa nyie basi mnaona potelea mbali. SHAURI YENU!
Yaani wewe hamu yako machafuko tu mbona kuna vitu vingi vya kufikiria zaidi ya huo ujinga ulokukaa kichwani, sasa naamini mjinga akielimika mwerevu huwa matatani. jiongeze lofa wee
 
hayo maandamano hayana tija yoyote zaidi ya kuleta vurugu...kama wana hamu ya kuandamana waandamanie majumbani mwao...
Mbona na wewe unakuwa kama JIPU UCHUNGU linalohitaji kutumbuliwa?

"Mjumbani" mwao!!??.....How? Kila mmoja awe anatoka chumba kimoja kwenda chumba kingine, au? Na sisi wenye chumba kimoja je, kona moja ya chumba hadi kona nyingine siyo!!??

Acha kujifanya jipu wewe wakati wewe ni kachunusi tu bhaaaana, alaa!!
 
Mbona na wewe unakuwa kama JIPU UCHUNGU linalohitaji kutumbuliwa?

"Mjumbani" mwao!!??.....How? Kila mmoja awe anatoka chumba kimoja kwenda chumba kingine, au? Na sisi wenye chumba kimoja je, kona moja ya chumba hadi kona nyingine siyo!!??

Acha kujifanya jipu wewe wakati wewe ni kachunusi tu bhaaaana, alaa!!
kumbe umenielewa ila unajifyatua akili...
 
Sasa kama wanaomba kibali na wananyimwa pasipo sababu wafanye nini,wakati huo huo CCM wakiomba kibali wanapewa pasi na shida!!!
FAHAMU CCM NI CHAMA TAWALA NDUGU YANGU. HAO WAKIANDAMANA BILA KIBALI WAPIGWE TU MAANA HAKUNA NAMNA NYINGINE!!
 
MiCCM walizunguuka Unguja nzima eti kusheherekea sherehe za Mapinduzi wakati sherehe izo sio za kichama na mwisho wake wakazuka na mabango ya ubaguzi,

Si polisi wala usalama waliowaita wale wabaguzi na kuwahoji nilitegemea Mheshimiwa Magufuli angelipasua lile chunusi la kipolisi kwa kutochukua sheria za kuwaita na kuwahoji ,Mheshimiwa si wakuu wa idara za TRA tu ndio wanaohitaji kuwajibishwa,kusimamishwa hata hawa wakuu wa polisi wanao onekana waziwazi wakimezea majambo mabaya ya CCM.

Haiwezekani vijana wa CCM waachiwe wafanye na kusema watakavyo wa vyama vingine mikono ya vyombo vya sheria inakuwa mirefu na kwa haraka ukichanganya na kasi kuwashughulikia ,wakuu hawa wa polisi si wa kuachiwa kwani haki za kibinadamu zinapimwa kwa utendaji wao wa kazi na kuiwakilisha Tanzania katika anga za kimataifa.

Mheshimiwa na hawa inahitaji kuchangamshwa ili waondokane na utendaji wa kazi kwa upendeleo wakati vyama vyote vina haki sawaa katika suala la kufuata sheria.
 
Back
Top Bottom