CUF kuiteka Zanzibar kwa maandamano

CUF kuiteka Zanzibar kwa maandamano

Hivi kikatiba polisi wanaombwa kibali au wanapewa taarifa ya maandamano yatakakopitia ili kuyaongoza au ni kutoa kibali. Inawezekana kbs kwamba tunataka kufanya mikutano au maandamano tunafanya makosa kuomba kibali na polisi wanakataa kutoa vibali kwa sababu siyo wajibu wao kikatiba. Wenzetu ccm wanafuata katiba kwa kutoa tu taarifa kama katiba inavotamka na polisi kazi yao kama katiba inatamka inawapa ulinzi baasi. Nyie mnakimbilia kuomba kibali wapi na wapi.
 
Vijana wa Chama cha Wananchi kupitia jumuiya yao (JUVI-CUF) wameweka msimamo kuwa ‘iwe iwavyo’ watafanya maandamano kesho visiwani humo kwa kuwa ni haki yao kufanya hivyo licha ya Jeshi la Polisi kupinga.

Maandamano hayo yameelezwa kuwa ni sehemu kumbukumbu ya Wazanzibari waliouawa mwaka 2000 kutokana na vurugu za kisiasa zilizotokea chini ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Maandamano hayo yametangazwa ikiwa ni siku chache baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kutangaza tarehe 20 Machi mwaka huu kuwa siku ya kurudia uchaguzi visiwani humo.

Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi mkuu visiwani humo uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana kwa madai ya kuwepo kwa kasoro mbalimbali jambo ambalo lilipingwa na CUF, taasisi za kiraia na baadhi ya makada wa CCM.

JUVI-CUF wamepanga kufanya maandamano makubwa visiwani humo kwa lengo la kupinga dhulma hiyo licha ya Jeshi la Polisi kuyagomea.

Wameeleza kuwa maandamano hayo watayafanya ili kuieleza dunia kwamba, Zanzibar haki inaminywa na kwamba, maandamano hayo yatakakuwa ujumbe mahsusi kwa wapenda demokrasia duniani.

Vijana hao wamesema kuwa, hawawezi kuona haki yao inapokwa na serikali kwa maslahi ya CCM na kwamba, maandamano hayo yatafanyike visiwani humo kama ilivyopangwa.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa JUVI-CUF, Abeid Ali amesema kuwa, wananchi wa visiwa hivyo hawatokoma kudai haki yao mpaka pale itakaposimama.

Mkurugenzi huyo ameeleza kwamba, wana imani kuwa si risasi wala mizinga ambayo inaweza kusimamisha haki visiwani humo na kwamba, watapigania haki hata kama wengine watauawa.

Kiongozi huyo amekumbushia mauaji yaliyofanya na Serikali ya Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa baada ya Uchaguzi Mkuu 2000 na kwamba, wananchi hawajaingia woga wala kurudi nyuma kudai haki yao.

“Sisi ni raia wakizanzibari, tuna uhuru wa kuandamana kwani CCM waliachiwa kuandamana na ulinzi wakapewa, na sisi tuna haki ya kufanya maandamano,” amesema Ali.

Amesema kuwa, maandamano hayo yatafanyika kuanzia Mtendeni kwenda Mnazimmoja na kumalizikia kwenye viwanja vya Maisara.

Chanzo: Mwanahalisionline
Wakiruhusiwa kuna tatizo gani, serikali iwapatie ulinzi tu.
 
Uhuru wa Kuandamana bila kibali? hawa nao wapigwe tu. Nchi bila taratibu si nchi tena, itabaki kuwa genge la wahuni
Hakuna kipengele katika sheria ya JMT kinachotaka wanaotaka kuandamana waombe kibali ama ruhusa kutoka kwa polisi au kokote kule. Wanatakiwa kutoa taarifa tu polisi ili wapatiwe ulinzi.

Kuzuwia maandamano ni advantage kwa CUF kwa vile wanataka kuuhakikishia ulimwengu kama nchi hii haina demokrasia. Tukumbuke tu kwamba hata hizo nchi nyengine zenye machafuko ya kisiasa sasa hivi zilianza kwa kuzuiliwa maandamano.
 
Uhuru wa Kuandamana bila kibali? hawa nao wapigwe tu. Nchi bila taratibu si nchi tena, itabaki kuwa genge la wahuni
vibari vya kutolewa kwa matakwa ya lumumba!
 
Aliyo
Ya Burundi yanataka kuanza! Na jana tumetishiwa kwa ndege za kivita! Hakiiiiiiiiiii. Damu ikimwagika itakuwa ni ushahidi tosha kuwa CCM inangangania madaraka!
Aliyoyataka Jecha yanaelekea kutimia.
 
Sasa kama mmeamua ole wenu mbadili maamuzi, kwakweli hatutawaelewa. Hata hivyo polisi ndo nafasi yao ya kula maujiko kwa kuwa fair. Hawa vijana ni wakupewa ulinzi stahiki maana kuna kero ambazo hata polisi zinawahusu. Maafande ebu vaeni uzalendo kwa mambo ya msingi hata mara mojamoja
 
Wangewaacha waandamane siku nzima najua kesho yake wasingeandamana tena sababu ya uchovu, kiu na njaa. Na hii pia ingekuwa ni dawa ya kupunguza mihemko au tension walizonazo
 
Aliyefuta aliepusha vurugu kwani tayari kuna mtu alikuwa amejitangaza mshindi wakati hata tume ilikuwa haijafika nusu ya matokeo iliotangaza...
Wewe ni la nne nendavkaseme adhabu ya mtu anaejitangaza .jf imevamiwa na la nne
 
Unadhani kupigwa tu ndio suluhu ya madai yao? Uhuru gani kama democracy inaminywa? Miongoni mwa elements za democracy ni free and fair election, transparent na nyinginezo nyingi. Je Z'bar kuna free and fair election? Wa Z'bar wasiposikilizwa nani atasikilizwa kwa maslahi na ustawi wa Z'bar?
gud thinker
 
Uhuru wa Kuandamana bila kibali? hawa nao wapigwe tu. Nchi bila taratibu si nchi tena, itabaki kuwa genge la wahuni
Police hawana mamlaka ya kuzuia maandamano, police wana haki ya kuyalinda maandamano, kama wamekataa, CUF watajilinda wenyewe
 
Back
Top Bottom