CUF kuiteka Zanzibar kwa maandamano

CUF kuiteka Zanzibar kwa maandamano

Yaani wewe hamu yako machafuko tu mbona kuna vitu vingi vya kufikiria zaidi ya huo ujinga ulokukaa kichwani, sasa naamini mjinga akielimika mwerevu huwa matatani. jiongeze lofa wee
Wewe ndio mpuuzi, unadhani hao wakianza kupigwa watasimama tuu? Lazima katika harakati hizo watu wanaweza kuumia au hata kufa. Sasa mie ndio nimepeleka machafuko hayo huko Zanzibar? Watu wenye akili wakiwa wanajadili mambo ya msingi wewe nenda kacheze na wenzio hayakufai haya kwa vile huelewi.
Ndio tatizo la watoto wadogo kama nyie ambao hawajui repercussions za nini kinaendelea upande wa pili wa muungano.
 
.....znz ni nchi ya kimapinduzi hawataitoa kwa makaratasi kamwe!!
what are they mean?......mtihani/
 
hayo maandamano hayana tija yoyote zaidi ya kuleta vurugu...kama wana hamu ya kuandamana waandamanie majumbani mwao...
Maandamano yenye tija ni Yale ya kuja na mabango ya Ubaguzi yanayokana ukweli kuwa hakuna MTU asiyeitwa chotara Zanzibar Yale yanapata kibali
 
Uhuru wa Kuandamana bila kibali? hawa nao wapigwe tu. Nchi bila taratibu si nchi tena, itabaki kuwa genge la wahuni
Mbona kibali kinatolewa ka chama kimoja vyama vingine hapana?
 
Uhuru wa Kuandamana bila kibali? hawa nao wapigwe tu. Nchi bila taratibu si nchi tena, itabaki kuwa genge la wahuni
Hivi wapinzani tu ndio wasiofuata utaratibu?Hivi jecha alifuata utaratibu alipofuta matokeo ya uchaguzi? Au double standards! Nchi yetu haifuati utaratibu tunaenda tuuuu!
 
VIJANA wa Chama cha Wananchi kupitia jumuiya yao (JUVI-CUF) wameweka msimamo kuwa ‘iwe iwavyo’ watafanya maandamano kesho visiwani humo kwa kuwa ni haki yao kufanya hivyo licha ya Jeshi la Polisi kupinga.

Maandamano hayo yametangazwa ikiwa ni siku chache baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kutangaza tarehe 20 Machi mwaka huu kuwa siku ya kurudia uchaguzi visiwani humo.
Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi mkuu visiwani humo uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana kwa madai ya kuwepo kwa kasoro mbalimbali jambo ambalo lilipingwa na CUF, taasisi za kiraia na baadhi ya makada wa CCM.
JUVI-CUF wamepanga kufanya maandamano makubwa visiwani humo kwa lengo la kupinga dhuluma hiyo licha ya Jeshi la Polisi kuyagomea.
Wameeleza kuwa maandamano hayo watayafanya ili kuieleza dunia kwamba,
Zanzibar haki inaminywa na kwamba, maandamano hayo yatakakuwa ujumbe mahsusi kwa wapenda demokrasia duniani.
Vijana hao wamesema kuwa, hawawezi kuona haki yao inapokwa na serikali kwa maslahi ya CCM na kwamba, maandamano hayo yatafanyika visiwani humo kama ilivyopangwa.
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa JUVI-CUF, Abeid Ali amesema kuwa, wananchi wa visiwa hivyo hawatokoma kudai haki yao mpaka pale itakaposimama.
Mkurugenzi huyo ameeleza kwamba, wana imani kuwa si risasi wala mizinga ambayo inaweza kusimamisha haki visiwani humo na kwamba, watapigania haki hata kama wengine watauawa.
Kiongozi huyo amekumbushia mauaji yaliyofanywa na Serikali ya Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa baada ya Uchaguzi Mkuu 2000 na kwamba, wananchi hawajaingia woga wala kurudi nyuma kudai haki yao.
“Sisi ni raia wakizanzibari, tuna uhuru wa kuandamana kwani CCM waliachiwa kuandamana na ulinzi wakapewa, na sisi tuna haki ya kufanya maandamano,” amesema Ali.
Amesema kuwa, maandamano hayo yatafanyika kuanzia Mtendeni kwenda Mnazimmoja na kumalizikia kwenye viwanja vya Maisara.
 
Uhuru wa Kuandamana bila kibali? hawa nao wapigwe tu. Nchi bila taratibu si nchi tena, itabaki kuwa genge la wahuni
Sheria ipi inasema kuandamana ni lazima upate kibali?
Hiyo sheria ameitunga nani?
Kama kipo kifungu, kinukuu.
Kibali?
Hii kitu ilipata kibali? Nani alitoa kibali?

DSC_2469.jpg

Polisi walitoa ulinzi?
 
Wewe ndio mpuuzi, unadhani hao wakianza kupigwa watasimama tuu? Lazima katika harakati hizo watu wanaweza kuumia au hata kufa. Sasa mie ndio nimepeleka machafuko hayo huko Zanzibar? Watu wenye akili wakiwa wanajadili mambo ya msingi wewe nenda kacheze na wenzio hayakufai haya kwa vile huelewi.
Ndio tatizo la watoto wadogo kama nyie ambao hawajui repercussions za nini kinaendelea upande wa pili wa muungano.

Nimekusoma lakini sielewi kwanini ni lazima wapigwe? Wakilindwa waachwe waseme hayo ya moyoni shida iko wapi ?
 
Yah right .............. wenye haki ya kuandamana ni UVCCM tu ............. tena pamoja na mabango yao ya kibaguzi!!
naona vifo katika hayo maandamano,maana yakiachiwa itakua mwanza wa maandamano yasiyokoma kudai kutorudia uchaguz,yakizuiwa vijana watafanya kwa kulazimisha na dola haitakubali,kuna roho zitaacha mwili
 
so bad .............. wangefikiria mara mbili walipokubali CCM waandamane kwa niaba ya Wazanzibar wote. Yale maandamano wasingeyapa image ya chama ........ at least wangekuwa na ajenda!!
 
Kabla kibali hakijatolewa ni lazima mamlaka husika ijilidhishe na dhumuni la maandamao. si kila maandamano yana tija.
Vipi yale naandamano yaliokuwa na mabango ya ubaguzi halafu ccm ikaomba radhi polisi walijiridhisha?
 
Uhuru wa Kuandamana bila kibali? hawa nao wapigwe tu. Nchi bila taratibu si nchi tena, itabaki kuwa genge la wahuni
ikishakuwa kuandamana ni kwa kibali,je UHURU unaouzungumza wewe ni upi?
UHURU haupo(never exist) mana dhana ya UHURU imejikita tu katika muktadha wa kutogusa maslahi ya mtoa kibali,ikiwa utagusa maslahi ya mtoa kibali basi maandamano hamna na uhuru haupo.
 
Naona anko magu nae anataka kuanza kuhesabu vichwa. Maana wakiandanana watafuata ile kauli ya pinda tu...nawapigwe tu maana hakuna namna.
Si tatizo kuesabu vichwa wazibari kuuliwa wameshazoea .na ndio kinachotafutwa mbona sio tatizo magu aesabu tu vichwa
 
Nimekusoma lakini sielewi kwanini ni lazima wapigwe? Wakilindwa waachwe waseme hayo ya moyoni shida iko wapi ?
Nilikuwa namjibu yule ambaye anataka haki hiyo ya kusikilizwa watu wa Zanzibar wasipewe.
 
Back
Top Bottom