Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Mume wa mama ni baba. Ndugu zangu wazanzibari tulikubali hilo.Nazi haishindani na jiwe.
Heshima tulioipta kutoka nchi zilizostaarabika duniani inatosha kutuliza machungu.
Heshima hiyo ni kubwa kuliko ile yakuranda nusu uchi mitaaani kusherehekea ushindo wa kishindo.
CCM ina haki yakufurahi kutokana ushindi wa kishindo, lakini haistahiki kusheherekea kwa yale yaliodhihirika.
CCM iwache kutamka maneno ya kiwendawazimu, kama vile " tuko radhi tufe na njaa...." Kwa mzanzibari mwenye umri kama mimi hasau mateso na madhila tulioyapata katika kipindi cha 1968-1972. Kulikuwa na njaa balaa ambayo ndio ilioibuwa wimbi la wazanzibari wasomi kukimbia nchi na kupoteza nguvu kazi ambayo mpaka leo tunaililia. Ikija njaa, watunzi wa wimbo huu haitawagusa isipokuwa wazanzibari wanyonge wa CCM na CUF na wasiokuwa na chama.
CUF ina haki ya kusikitika lakini haistahiki kuropoka lugha ambazo zitakazo tafsirwa na Amiri jeshi mkuu kuwa ni "fyokofyoko" Hatuna ubavu wa kuoneshana na watu 49 milioni wenye ghadhabu ya kutaka kukimeza kisiwa cha Zanzibar na watu milioni moja na ushei wa visiwani ambao wimbo wao mkuu ni " hewala bwana". Tujihadhari kabla ya athari. Wazanzibari kindakindaki wengi ni ndugu wa damu na si wa bendera, tushikamane kuutii utawala utakao tawadhisha kesho.
Kunguru mwoga..........