Chadema sasa ni shubiri kali kwa CCM na CUF... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema sasa ni shubiri kali kwa CCM na CUF...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Feb 3, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  Kishindo cha CHADEMA chawavuruga CUF, CCM
  • Mtatiro wa CUF aivurumishia shutuma nzito

  na Waandishi wetu


  [​IMG] MAFANIKIO ya kisiasa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yanaonekana kuzidi kuwa kero kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), Tanzania Daima limebaini.
  Hali hiyo ilizidi kujidhihirisha jana, baada ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro kuendelea kutoa matamshi yenye mwelekeo wa chuki na husuda dhidi ya CHADEMA yaliyomfikisha hatua ya kujikuta akitumia lugha isiyo na staha inayofanana na hadhi ya chama hicho cha upinzani chenye nguvu kubwa Tanzania Visiwani.
  Mtatiro ambaye tangu aingie katika kiringe cha siasa za kitaifa amekuwa akifanya juu chini kupambana na CHADEMA na viongozi wake kwa namna ile ile inavyofanywa na viongozi wengine wa chama hicho, jana alieleza kusikitishwa na hatua ya CHADEMA kuamua kuunda kambi yao ya upinzani bungeni pasipo kushirikiana na wapinzani wengine.
  Mtatiro ambaye katika Uchaguzi Mkuu uliopita aligombea ubunge wa Ubungo kwa tiketi ya CUF akikataa katakata ushawishi wa vijana waliokuwa wakimtaka amwachie John Mnyika wa CHADEMA, aliibuka na kuwashambulia wapinzani wenzake hao akiwapa sifa na majina mabaya.
  Mtatiro na CUF wanaonekana kukerwa na tamko la CHADEMA lililotolewa juzi na Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa aliyetangaza rasmi kuunda upinzani unaojitegemea bungeni.
  Akitoa tamko lililosheheni kauli za jazba, propaganda, maneno ya mitaani na matusi, Mtatiro aliishambulia CHADEMA na viongozi wake akisema lengo lao la kukataa kushirikiana na CUF ni kutaka chama hicho kife.
  “Viongozi wa CHADEMA na chama chao ndio watakaokufa na kuiacha CUF ikiimarika…CHADEMA ‘ni chama popo, ndumilakuwili na wajinga,” alisema Mtatiro ambaye alikwenda mbele na kuwafananisha viongozi wa chama hicho cha upinzani na Padri aliyekiuka kiapo na kukimbilia kula raha na wachumba.
  Wakati akiishambulia CHADEMA, Mtatiro alisema chama chake kitaendelea kushirikiana na CCM Zanzibar kwani kilichotokea Zanzibar ndiyo matakwa halisi ya wananchi wa visiwa hivyo na kamwe hakitawalamba miguu na CHADEMA ili kushirikiana nao.
  “CUF tunaamini CHADEMA wamewadharau Wazanzibari, wanawaona hawana maana, wanadharau maamuzi yao, wanaona hawawezi kufikiri na kujiamulia mambo yao wenyewe, hilo hatunalo shaka,” alisema Mtatiro.
  Akiendelea kuishambulia CHADEMA alisema chama hicho kiliusaliti ushirikiano wa vyama vya upinzani katika chaguzi ndogo za Tarime, Tunduru, Busanda, Mbeya Vijijini na hatimaye kusababisha uvunjike, akidai kuwa mara zote kilitaka kisimamishe wagombea wake hata katika maeneo ambako kilikuwa hakina nguvu.
  Huku akionekana kuwa naye aligombea ubunge Ubungo ilhali akijua CHADEMA na Mnyika walikuwa wamejizatiti, Mtatiro alitoa maelezo ambayo yalionekana yakiwa na mwelekeo wa wazi wa kujikanganya.
  Kumbukumbu zinaonyesha kuwa, chanzo cha kuvunjika kwa ushirikiano huo wa upinzani, ni hatua ya Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kutoa kauli zilizoonyesha kuunga kwao mkono tuhuma za kubuni dhidi ya viongozi hao wa CHADEMA kwamba walikuwa na mkono wao katika kifo cha aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Chacha Wangwe.
  Maudhui na aina ya lugha ya matusi iliyotumiwa na CUF katika tamko hilo kwa kiasi fulani vilionekana kufanana na mashambulizi yaliyofanywa na Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) hivi karibuni dhidi ya CHADEMA na Dk. Slaa ambaye wamekuwa wakimwita ‘mwendawazimu’ bila kufafanua.
  Katika hatua nyingine inayoashiria kuzidi kuungwa mkono kwa CHADEMA na viongozi wake, jana Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alikuwa kivutio katika sherehe ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambayo rais Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi.
  Mbowe alikuwa kivutio wakati akiinuka kwenye kiti alichokaa kuelekea kwenye ngazi za Mahakama Kuu kupiga picha na viongozi mbalimbali wa serikali na mahakama ambao ni watumishi wa mahakama, mawakili na wananchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo.
  Watumishi wa mahakama pamoja na wananchi hao walisikika wakimshangilia kwa sauti ya juu “Mbowe Mbowe, Mbowe” na kiongozi huyo kulazimika kuwapungia mkono na kutabasamu.
  Akitoa hotuba yake katika sherehe hizo, Rais Kikwete aliutaka mhimili wa mahakama kushirikiana na vyombo vya habari kutoa elimu kwa umma kuhusu utendaji kazi na muundo wa mahakama ukoje kwani kwa kufanya hivyo kutamuondolea adha anayoipata hivi sasa ya wananchi kufika Ikulu na kumtaka atengue hukumu mbalimbali wakilalamika kutotendewa haki.
  “Wananchi wamekuwa wakijazana pale ofisini wakitaka nitengue hukumu zilizokwishatolewa na mahakama na mimi nimekuwa nikiwaambia sina mamlaka ya kufanya hivyo… wananchi hao wamekuwa wakinijibu kama siwezi kufanya hivyo watamchagua rais anayeweza kufanya hivyo na kwamba ndiyo maana wanataka katiba mpya…lakini yote hii inasababishwa na umma kuwa na uelewa finyu wa sheria na muundo wa mahakama,” alisema Kikwete na kusababisha watu kuangua vicheko.
  Wakati huo huo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga juzi alilazimika kutumia salamu za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kuwashawishi wanafunzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya (MIST) waweze kumsikiliza.
  Kitwanga alilazimika kukikubali japo kwa muda Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kutokana na hatua ya wanafunzi wa chuo hicho kuguna kila alipoitaja ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi wakati akizungumza nao kuhusu inavyotekeleza sera ya elimu.
  Waziri huyo alilazimika kuwasalimia wanafunzi hao akisema “CHADEMA hoyee!!, na ukumbi mzima ulizizima kwa mayowe na vifijo vya wanafunzi waliopaza sauti zao wakimjibu “Oyeeee” huku kila mmoja akimpungia alama ya vema kwa kuonyesha vidole viwili.
  Kitendo cha Waziri Kitwanga kutumia jina la CHADEMA katika kibwagizo hicho kilitokana na hatua ya wanafunzi hao kuguna pale alipoanza kujibu maswali yao kwa kusema “katika Ilani ya ya CCM…..” bila kumalizia kusema alishtushwa na miguno.  [​IMG]

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  Tamko la Chadema laichanganya kambi ndogo ya upinzani bungeni Send to a friend Wednesday, 02 February 2011 20:56 0diggsdigg

  Fidelis Butahe
  TAMKO lililotolewa na Chadema kuwa hakiwezi kushirikiana na vyama vingine vya upinzani bungeni kwa sababu, vimeungana na CUF ambayo ‘imefunga ndoa' na CCM na kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, inaonekana kuvitesa vyama hivyo.

  Katibu Mkuu Chadema, Dk Willibrod Slaa, hivi karibuni alikaririwa akisema Kamati Kuu ya Chadema, imeona chama hicho hakiwezi kuwa na ushirikiano wenye tija na vyama hivyo bungeni, na kumwagiza kiongozi wa kambi ya upinzani kuunda baraza kivuli la mawaziri la wabunge wa Chadema pekee.

  "Kamati Kuu imeendelea kuzingatia umuhimu wa vyama vya siasa kushirikiana katika kuimarisha nguvu ya upinzani nchini.

  Hata hivyo, Kamati Kuu imezingatia kuwa, CUF na CCM wamejiunga kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na kwa kuwa, sheria inayoruhusu uwepo wa vyama vya siasa inahusu pande zote za Muungano, inaamini CCM na CUF ni wamoja hata Bara," alisema Dk Slaa.

  Jana Mwenyekiti wa Umoja wa vyama hivyo ambavyo vipo nje ya kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed na Katibu wake, David Kafulila, walikuwa wazungumzie suala hilo, lakini ilitolea taarifa kuwa mkutano huo uliahirishwa hadi leo.

  Pamoja na kutolewa kwa taarifa hiyo, Makamu mwenyekiti wa umoja huo, Khalifa Suleiman Khalifa, alijikuta akitolea ufafanuzi msimamo wao baada ya kubanwa na waandishi wa habari na kusema tamko hilo haliwezi kuwalazimisha Chadema.

  Khalifa, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Gando (CUF), alisema Chadema wana haki ya kuunda kambi yao bila kuvishirikisha vyama vingine.

  "Nawashangaa sana Chadema wanaposema kuwa hivi sasa CUF na CCM lao moja, vyama hivi viliamua kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kumaliza siasa ya mvutano visiwani Zanzibar, hoja wanayoitoa sidhani kama inawatendea haki Watanzania," alisema Khalifa na kuongeza:

  "Chadema wanatakiwa kutambua kuwa, kilichopo Zanzibar ni serikali ya umoja wa kitaifa sio serikali ya mseto, kama hawataki sawa…sisi hatuko rasmi kama wao. Tutaendelea kuwawakilisha wananchi kwa kuwa ndio kazi ya mbunge.
  "
  Akitolea ufafanuzi habari zilizoenea kwamba wamewasilisha kwa spika maombi ya kutaka kubadilishwa kwa kanuni za bunge ili kuondoa neno ‘kambi rasmi bungeni' ili nao watambuliwe, alisema suala hilo ni gumu kupatiwa ufumbuzi.

  "Ili chama kiweze kuunda kambi hii, lazima kiwe na wabunge zaidi ya 45, yaani asilimia 12 ya wabunge wake wote, Chadema wamefikisha hilo, sisi tumepeleka hoja tu ila hatujapeleka pendekezo. Kanuni zinatakiwa kutizamwa upya ili kukidhi haja," alisema Khalifa.

  Khalifa aliungwa mkono na Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Mohammed Habib Mnyaa, ambaye alifafanua kwamba CUF ilikubali kuwa kitu kimoja na vyama vingine wakati kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni alipotokea kwenye chama hicho.


  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]

  Comments
  0 #4 steven 2011-02-03 08:03 Hii iko hivi hapa kuna uroho wa madaraka kwani lazma uwe kwenye kambi rasmi ya upinzani ndio ufanye kazi? Jamani tunakuwa walevi wa madaraka huyu Hamad Rashid na kafulia hawana staha za uongozi kwanza hawatufai hata kidogo chadema hakuna kurudi nyuma kuna kundi kubwa la watu lina waangalia nje huku likisubiri ukakamavu wenu kisiasa kuanza kumsikiliza uyo hamad na kafulila ni ukosefu wa akili hakuna kuweka mtu hapo cuf ni ccm na nccr hakuna mtu anayeweza kuongoza hata mmoja bora mrema kuliko wote hao
  Quote

  0 #3 elibariki yerald 2011-02-03 07:42 cuf ni wasaliti na waroho wa madaraka umoja wa kitaifa zanzibar siyo sababu ya chadema kuwa kataa cuf bali ni usaliti na unafiki wao wa muda mrefu na vitina dhidi ya chadema
  Quote

  0 #2 elibariki yerald 2011-02-03 07:40 utalisiti wa cuf hawajaanza leo kwa CHADEMA historia itawahukumu tukianza kuwasimulia hapa waanzani aCUF ni ndumilakuwili na watafutajia wa madaraka, CHADEMA songeni mbele
  Quote

  +2 #1 Isaya olomi 2011-02-03 06:16 Hapa CUF mmelikoroga na lazima mlinywe, itaingiaje akilini mnajiita wapinzani huku ni sehemu ya serikali iliyo madarakani? Chadema wapo makini kupita maelezo.Hata hivyo wabunge wote bila kujali ni kutoka chama gani nadhani wanachotakiwa kufanya bungeni sio kushabikia kila hoja sababu tu inakibeba chama chao, bali ni kuangalia manufaa ya hoja kitaifa, hivyo sioni haja ya kubabaika sana kutaka ku kijoin chadema.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  CUF: Hatuwezi kuwalamba miguu Chadema Wednesday, 02 February 2011 20:51

  Hussein Issa na Elizabeth Ernest
  CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema hakiwezi kuwalamba miguu viongozi wa Chadema, ili wakubali kushirikiana nao.

  Kauli hiyo, inafuatia baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kunukuliwa na vyombo vya habari juzi akisema hawawezi kushirikiana na vyama vingine vya upinzani bungeni kwa kuwa vyama hivyo vimeungana na CUF ambayo 'imefunga ndoa' na CCM na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

  Dk Slaa alisema Kamati Kuu ya Chadema imeona kuwa chama hicho, hakiwezi kuwa na ushirikiano wenye tija na vyama hivyo bungeni.

  Kutokana na hali hiyo, alimuagiza kiongozi wa kambi ya upinzani kuunda baraza kivuli la mawaziri kwa kuwahusisha wabunge wa Chadema pekee. Lakini jana, Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Julius Mtatiro alisema mbele ya wanahabari kuwa, chama chake hakiwezi kuilamba miguu Chadema ili ishirikiane nayo kwa kuwa haina faida yoyote kwa CUF.

  "Tunapenda kuwataarifu Watanzania wote kuwa sisi (CUF), pia hatuwezi kuwalamba miguu viongozi wa Chadema kwani jitihada zetu za kuwaambia wafanye kazi na vyama vingine tayari zimegonga ukuta," alisema Mtatiro.

  Alisema mara nyingi Chadema imekuwa na historia ya kusaliti vyama vingine vya upinzani, kutokana na kuwa na uchu wa madaraka. Alisema mwaka 2002 walifikia maamuzi ya kushirikiana kwa vyama vinne vikiwemo Chadema, NCCR na TLP, lengo likiwa kuunga mkono chama chenye nguvu mahali panapofanyika uchaguzi, lakini Chadema ilikataa.

  Alisema tofauti na matarajio ya malengo yao, katika uchaguzi wa marudio Jimbo la Tunduru NCCR na TLP walijitokeza kuisaidia CUF kwa kuwa huko ilikuwa ni ngome yake, lakini Chadema walisimamisha mgombea wao na kumfanya mgombea wa CCM kushinda bila tatizo. "Chadema walijifanya mapopo, wakasaliti makubaliano yaliyowekwa na vyama vingine, wakati hata tawi hawana kule Tunduru," alisema .

  Alisema hali kama hiyo pia iliwahi kutokea katika majimbo ya Tarime, Busanda na Mbeya vijijini, ambako Chadema walikataa kutoa ushirikiano kwa vyama vingine kama walivyokubaliana na kuamua kusimamisha wagombea.

  Alisema kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Chadema ndiyo inayotakiwa kuunda kambi ya upinzani bungeni, lakini CUF iliiomba Chadema ishirikiane na vyama vingine vya upinzani ili kambi hiyo iwe imara zaidi na yenye nguvu, lakini Chadema walikataa suala hilo kwa maelezo kuwa wao hawako tayari kuungana na CUF na vyama vingine ikiwa havitashirikiana na CUF.

  "Jana Chadema wametoa kauli ya kinafiki eti wao hawawezi kushirikiana na chama kinachoongoza Dola yaani CUF, na kwamba wapo tayari kushirikiana na vyama vingine.

  " Chadema ni chama popo sana, hawajui wanachokifanya, wamelewa madaraka na kuchanganyikiwa vibaya baada ya kupata majimbo 20,"alisema Mtatiro.

  Aliifananisha Chadema kuwa ni sawa na mtu masikini sana kuamka ghafla akajikuta tajiri, hajui namna gani atatumia utajiri wake na kuanza kuwatukana majirani zake alioishi nao kwa shida na raha katika umasikini wake.

  Alisema kitendo cha Chadema kuwashambulia CUF kwamba ni sehemu ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, ni dhambi kubwa, kwani Wazanzibar walitaka kuungana na CCM.


  "Chadema wamekuwa waoga mno, wanaiogopa CUF, wanajua CUF inamtandao mkubwa na mbinu ya kujiimarisha bara na hatimaye kuongoza nchi,"alisema Mtatiro.

   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  Upinzani ni itikadi na Chadema misimamo yao haioani na ya CUF au vyama vingine vya upinzani........................vile vile CUF wanapaswa kujifunza ya kuwa kujikita katika kambi ya upinzani hakumaanishi lazima mpewe kamati za kuziongoza la hasha........................mnaweza kuiunga mkono Chadema kwa kauli zenu Bungeni na nje ya Bunge...............................................
   
 5. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndio maana siku hizi sisomi tena Tanzania Daima wanapenda kuandika udaku na biased stories! Naliweka category moja na Sani na Kiu!
   
 6. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Kweli chadema imewashika pabaya. Kila kukicha bila kuitaja hawasikii raha.
   
 7. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CHADEMA nomaaa.....hivi kuna chama lingine lolote liloweza kutesa kama chadema kinavyotesa sasa?
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,636
  Likes Received: 4,746
  Trophy Points: 280
  CUF wacheni uchangudoa wa kisiasa, nyie mmewekwa kinyumba na CCM sasa huku CDM mnataka nini? Si nyie mlikimbilia kukalia viti vya CDM wakati wanamsusia Dr wa magumashi pale bungeni na huku mkigongeana mikono na mashoga zenu CCM? Wacheni wenye dhamira ya kuleta ukombozi wafanye kile tulichowatuma, nyie bakini kuwa wa tende halua halua. Hamna haya nyie.Ama kweli changu doa hana haya.
   
 9. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,458
  Trophy Points: 280
  CUF wapinzani wao ni CHADEMA sio CCM. How pathetic!
   
Loading...