CUF inapoisakama CHADEMA

Kama CDM hakitishi ilikuwaje kikawamwaga CUF Igunga?Unaposema kampeni makanisani mbona hukushangaa maaskofu 2005 kusema kikwete ni chaguo la Mungu?Acheni hizo ndugu,jipangeni upya manake mziki wa CDMhamuuwezi.Mmesikia CDM wanakwenda kumuona Rais na nyie mnataka.Mnakwenda kumwambia nini wakatimlibariki kila kitu kule bungeni?Acheni unafiki.
 
Mtoa mada ktk point no2 umesema cuf walikua wanafanya kampeni zawazi msikitini,pia hata cdm walifanya kampeni zawazi makanisani hasa katoliki,tena na ushahidi wa cd za picha tunao,slaa alikua analala makanisani nakufanyiwa kampeni zawazi namapadri wenzie,ukibisha cd tunazo zakampeni za cdm naslaa makanisani,usitukane mamba kabla hujavuka mto.

mkuu, ili kukata kabisa mzizi wa fitna ingekaa vizuri kama ungezianika kabisa hizo cd hapa jamvin. Kudaaadek, hapa ndo nnapo papenda mie!
 
kwavile umewaambia ukweli mtupu tena usio nashaka nakwambia hawatokujibu kwa hoja badala yake wataanza kukuporomoshea mitusi ila usijali tumeshawazoea ndio staili yao yakisiasa,siasa zao za maji taka tupu.

kweli kichaa hajijui! Kwa akili yako umeona jamaa kajibu kwa hoooja bila kutukana?
 
msitukanane wajomba kwani sisi wote ni watanzania na hii sio dalili njema katika siasa na utulivu wetu, kwa maana kama hapa JF tunanyukana namna hii, itakuwaje tukikutana live. Nani wana tolerance zaidi baina ya CUF na CDM?
 
Chama cha CUF kimeibuka kuwa mpinzani mkubwa wa CHADEMA hata katika mambo ambayo chenyewe kilikuwa kikiyaamini kilipokuwa chama kikuu cha upinzani. CUF hawajiulizi ni vipi CHADEMA imepata umaarufu wa ghafla namna hii. Kwa mtazamo wangu, umaarufu wa CHADEMA sio wa ghafla bali ulijengwa taratibu. Zifuatazo ni miongoni mwa tofauti za utaratibu ndani ya vyama hivi.
  1. Tangu kuanzishwa, CHADEMA imekuwa na wenyeviti watatu na wawili waliostaafu bado ni wanachama wenye kuheshimika ndani ya CHADEMA tofauti na CUF yenye king'ang'anizi asiyependa mabadiliko.
  2. CHADEMA kimezushiwa kuwa na udini baada ya CCM kuona nguvu yake. Hali ya CHADEMA ni tofauti na CUF ambapo mwaka 1995 mwenyekiti wake alipiga kampeni misikitini wazi wazi na katika mikutano yake utakuta ni vi-barghashia vinatawala.
  3. CHADEMA imebadilisha karata ya ugombea urais baada ya Mbowe kujaribu bila mafanikio ndipo ilipomleta Slaa aliyetokea kuwa kipenzi cha wengi tofauti na Lipumba tunayemtarajia tena 2015.
  4. Dr. Slaa wa CHADEMA amekuwa maarufu zaidi kwa staili ya yake kulipua mabomu bungeni na kuwataja mafisadi bila woga tofauti na Lipumba ambaye hajawahi kukemea ufisadi kwa besi.
  5. CHADEMA ni walifanya ujanja kwa kuiga staili ya Obama kufanya kampeni kupitia mitandao ya simu na internet na CUF walifikiri haitawasaidia kwani vijana wengi walionekana kutopenda siasa, ikala kwao.
  6. CHADEMA walitengua msemo wa nabii hakubaliki nyumbani kwa kuchukua jimbo analotoka mwenyekiti wao na katibu aliyekuwa akigombea urais, tofauti na CUF waliopoteza nyumbani kwa mwenyekiti. Hii inatokana na tofauti ya kuwekeza ambapo CUF wamewekeza zaidi visiwani huku wakiutaka urais wa muungano.
  7. Wakati CUF wanazinduka kumleta machachari Mtatiro katika siasa zao wanasahau kuwa CHADEMA waliliona hilo mapema na kuwa na vijana kama Mnyika, Zitto, Kafulila, nk
  8. Wazee wa CHADEMA hawaangalii zaidi wao wanataka nini, bali watu wanataka nini. Ndio maana mwanamuziki Sugu ambaye kwa kauli za awali za wapinzani wake walimwita mhuni, akawekwa kulikwaa jimbo. CCM nao kama CHADEMA walikuwa wakiandamana na kundi kubwa la wasanii wakiongozwa na Joseph Haule. CUF walidhani kipaza sauti pekee kinatosha.
  9. Nguvu kubwa ya kimaamuzi CCM ipo kwa mwenyekiti, CHADEMA ipo kwa baraza kuu na CUF ipo kwa katibu mkuu.
  10. CHADEMA, hata kama wanakosea; wana kawaida ya kutoa tamko pale jambo linapojitokeza. Tofauti na CUF ambao wana kawaida ya kusubiri kwanza kuona upepo unavumaje.
  11. Siasa ni kama dini ambapo muumini huvutwa na mlengo wa chama. Kimataifa, CHADEMA kimefuata mlengo wa kulia na ndio maana kinahusishwa na vyama kama conservative cha Uingereza na Republican cha Marekani, na CCM mlengo wa shoto kikihusishwa na Labor cha Uingereza na Democrats cha US. CUF kama chama, mlengo wake hauko wazi.
Ni dhahiri basi CUF wana kazi kubwa ya kurekebisha kuanzia ndani ndipo watoke uwani. Umaarufu wa CHADEMA usiwatie wivu hata wakaamua kuwapinga katika masuala yenye manufaa kwa Watanzania. Kushiriki katika serikali ya Zanzibar kusiwe chanzo cha uswahiba na serikali ya Tanzania na kuwa mpinzani wa wapinzani wenzako.

angalizo : mwanzisha sredi sio mwana CUF wala CHADEMA
Mkuu samahani sana ktk hoja hiii inaonyesha wewe ndiye mwenye kuisakama CUF.. Matusi yote haya ya nini ikiwa Chadema imefanikiwa kwa mtazamo wako.. Labda nikwambie tu moja ya kwamba CUF wana matatizo yao na inajulikana wazi kwamba chama hiki kilizushiwa Udini kaaChadema walivyozushiwa lakini wapo wanachama wengi wanaoendesha Udini ndani ya vyama hivi. Na wewe unajionyesha wazi kwamba ni Mkristu mwenye chuki na Uislaam.. Hali halijifichi na umeliweka wazi..

Pili, Chadema wamekuwa maarufu sio kwa sababu ni chama mbadala, laa hasha ni kwa sababu CCM inakufa, CCM imepoteza mwelekeo na hivyo Chadema ndio chama pekee kinachoshindilia kidole ktk madonda ya CCM. Lakini umaarufu wa NCCR au CUF kwa wananchi na mapenzi ya chama bado kabisa Chadema haijafikia mapenzi yale kwa sababu Ukimwondoa Dr.Slaa, chama kinapoteza nguvu kubwa wakati CUF na NCCR waliondoka viongozi lakini bado wananchi waliweka mapenzi yao kwa vyama. Hawa CUF na NCCR walipambana na CCM wakati kikiwa imara na chenye mvuto zaidi ya leo hii, hivyo wape pongezi zao..

Sema tatizo la vyama hivi vyote ni uongozi wa ndani. Makosa haya yapo CUF, NCCR na hata Chadema ambako kuna Opportunist, watu wamejipanga kugombea nafasi za kazi na uongozi wajuu wa chama badala ya kujihusisha zaidi na wananchi na hii pekee ndiyo ilomtenganisha Dr.Slaa na viongozi wengine. Kwa upande mwingine Mbowe ameifanya kazi kubwa ya kuweka msimamo wa chama ktk kufikia maazimio walokusudia japokuwa amekuwa na upinzani mkubwa toka ndani..Upinzani ambao hautazami mwelekeo wa chama na agenda zake bali - ULAJI kwa sababu maskini siku zote hutaka shibe kwanza kabla ya kuangalia maswala mengine.

Hizi ndizo siasa za Bongo, nchi maskini ambayo wanajaribu kugawana umaskini kwa kutumia mbinu za matajiri na nchi za Ulaya. Tajiri huwekeza FEDHA zake akitegemea faida kwa kipindi fulani lakini maskini akiwekeza MUDA wake (maana hana mtaji) ndio kaondoa sahani ya chakula mezani.

Vyama vya Upinzani vyote vimejaa opportunist ambao kwa umaskini wao fikra za kuongoza chama ni kupata Ajira, Uheshimiwa na kupendeza ktk kumudu maisha ya nchi ilijaa Maskini, wajinga na wenye maradhi.

Na amini maneno yangu kwamba watu tunaikubali Chadema kwa sababu hakuna chama kinachotumia udhaifu wa CCM kama mtaji wao isipokuwa Chadema lakini haina maana tunakubaliana na bandiko lako. Umezusha mengi kwa fikra zako na kujipa matumaini makubwa lakini Chadema ni chama bado kabisa dhaifu na kinahitaji kujipanua kama chama chenye itikadi na sio kutumia umaarufu wa Dr.Slaa, Mbowe na Zitto kuwa mtaji mkubwa wa chama.
 
Na wewe unajionyesha wazi kwamba ni Mkristu mwenye chuki na Uislaam.. Hali halijifichi na umeliweka wazi...

Mkuu naafiki kabisa miye mkristu, lakini unitake radhi kwa sababu umenizushia kuwa nina chuki na waislamu! Nilikuwa Tabora wakati wa kampeni za 1995 na Lipumba alikuwa akipiga kampeni misikitini. Ndio maana kuna mchangiaji mmoja amesema ana DVD ya Slaa akipiga kampeni kanisani na nikasema si sahihi kama ni kweli. Sasa chuki dhidi ya uislamu iko wapi?

Umezusha mengi kwa fikra zako na kujipa matumaini makubwa lakini Chadema ni chama bado kabisa dhaifu na kinahitaji kujipanua kama chama chenye itikadi na sio kutumia umaarufu wa Dr.Slaa, Mbowe na Zitto kuwa mtaji mkubwa wa chama.

Sasa mkuu weye ulitaka nitumie fikra za nani zaidi ya nilizonazo mwenyewe? Niliyotoa ni mawazo yangu na weye uliyosema pia ni yako kama unavyoyaamini wewe mwenyewe na ndio maana ya jukwaa hili.
 
Mkuu naafiki kabisa miye mkristu, lakini unitake radhi kwa sababu umenizushia kuwa nina chuki na waislamu! Nilikuwa Tabora wakati wa kampeni za 1995 na Lipumba alikuwa akipiga kampeni misikitini. Ndio maana kuna mchangiaji mmoja amesema ana DVD ya Slaa akipiga kampeni kanisani na nikasema si sahihi kama ni kweli. Sasa chuki dhidi ya uislamu iko wapi?
Kama Lipumba alipiga kampeni misikitini, wakati huo yeye ndiye alikuwa mgombea urais wa CUF na Chadema unataka kunambia Chadema nao walikuwa Waislaam wakati huo?.. Je, kama Mzee Mkapa pia alikwenda makanisani utasema alifanya udini?. Huyo mchungaji kwa nini awe na video za waislaam wakati haoneshi zake wakati Mkapa, Mwinyi au JK wanapofanya kampeni makanisani...

Hizi ni chuki mkuu wangu acheni habari hii kuuchukia Uislaam wakati hatuwafanyi lolote. Viongozi hawa wote huenda misikitini na makanisani kufanya ibada ya sala, hutokea wakati mwingine hupewa nafasi za kutoa hutba hasa wakati wa kampeni inapobidi..Mbona sisi hatuweki video zenu au kwa sababu hatusemi basi imekuwa kosa..

Sasa mkuu weye ulitaka nitumie fikra za nani zaidi ya nilizonazo mwenyewe? Niliyotoa ni mawazo yangu na weye uliyosema pia ni yako kama unavyoyaamini wewe mwenyewe na ndio maana ya jukwaa hili.
Bila shaka umetumia fikra zako kilichotakiwa ni wewe kufanya Uchunguzi na ukapata uhakika wa haya uloandika badala ya kuzungumzia fikra zako kama vile una uhakika na uloyasema. Habari za Pwagu na pwaguzi mkuu wangu hazijengi bali zinabomoa.. face the truth hata kama unauma.
 
Hizi ni chuki mkuu wangu acheni habari hii kuuchukia Uislaam wakati hatuwafanyi lolote. Viongozi hawa wote huenda misikitini na makanisani kufanya ibada ya sala, hutokea wakati mwingine hupewa nafasi za kutoa hutba hasa wakati wa kampeni inapobidi..Mbona sisi hatuweki video zenu au kwa sababu hatusemi basi imekuwa kosa...

Subiri mpaka niseme nawachukia waislamu ndipo useme nina chuki nao! Unalazimisha chuki ambazo hazipo (kwa taarifa yako hata shemeji yako ni mwislamu)....na umeamua kuweka kigingi hapo kana kwamba thread yangu ina point moja tu. Umeacha kabisa mambo kumi niliyoongelea na umejikita kwenye hili la udini. Na hii ndio shida yenu; unataka kubadili mwelekeo wa mjadala ushike sura ya udini. Nategemea baada ya hapa utaachana na hii habari ya udini na kuchangia zaidi ili kusiwe na kusakamana baina ya CUF na CHADEMA ili kujengwe upinzani wa kweli Tz na CCM iwajibike kama bado itaendelea kuwa madarakani.
 
ni ubishi usio na sababu kwani ujweli upo wazi kabisa huku kwe2 slaa alifikia kanisani na alipokewa na mapadre na ndio waliompigia kampeni

acha uongo na unafiki. kwenu wapi huko? kanisani kwetu ni kweli alifika na alipokewa na paroko na kupewa kiti cha mbele kwa kuwa ni kiongozi wa kitaifa hata nilishaona lowasa ingawa sio member wa kanisa letu aliwahi kusali kwetu na kupewa kiti cha mbele.by the way kwa itifaki za kikatoliki dr.bado anatambulika kama padre tene alikuwa na dalaja kubwa labda kuliko hata paroko wetu. nilichoshuhudia ni watu kushangaa sana na baada ya misa watu wengi tulienda kumshika mkono kwa kuwa ni maarufu na kipenzi cha watanzania. la kupigiwa kampeni mimi sikulisikia hata kidogo.na waraka mlioshupalia ilikuwa ni elimu juu ya wapiga kura kwamba tuchague viongozi wazuri (wasio mafisadi).sasa kama kutochagua fisadi ilimanisha kuchagua dr.slaa, hapo sina neno.
 
Bwe.ge wewe! Mi nilidhani naongea na mtu wa maana mwenye ushahidi kumbe ulikuwa unatishia nyau? Ulisema una video za Slaa kanisani akifanya kampeni, ziko wapi? Mimi nilisema kuwa nina video za Lipumba msikitini?
***** mkubwa ni wewe,tushindane kwa hoja sio matusi usitutaftie ban bure,toa ushahidi wa lipumba kufanya kampeni msikitini nami nitaweka cd hadharani,kua mstaarabu kidogo japo si asili yako ustaarabu.
 
***** mkubwa ni wewe,tushindane kwa hoja sio matusi usitutaftie ban bure,toa ushahidi wa lipumba kufanya kampeni msikitini nami nitaweka cd hadharani,kua mstaarabu kidogo japo si asili yako ustaarabu.

MODS mna kazi......
 
Utawatambua kwa maneno:Mwandishi ni pure Chadema for comments zake za muda mrefu hapa JF.

CCM ni chama kinachoongoza sana kuisakama CDM mbona hawasemi hao unarukia CUF?
CDM ndo kila Siku inaibua propaganda za kuichafua CUF kila wanaposimama kwenye majukwaa.Kwa vile mwandishi ni CDM iko hivyo ila angekuwa mtu asiye na mlengwa wa chama chochote na anayefikiri sawia kwa fikra kinzani bila shaka thread ingesomeka"CHADEMA IPOISAKAMA CUF"

Mimi ni mshabiki wa siasa na kuna mambo yanayonivutia na yanayoniudhi. Mengi yanayoniudhi yanasemwa na kutendwa na CUF. Moja wapo ni pale CUF inapokuwa mstari wa mbele kuisaka CDM. Ubaya wake wengi tunalazimika kuamini kuwa ni muafaka wake na CCM kuisakama CDM.

Wiki iliyopita nilikuwa Zanzibar nilifikia mtaa maarufu kwa CUF. Kwa kawaida yangu nilivaa kaunda suti ya rangi ya kombati, kila asubuhi na jioni wageni kibao wanamuulizia Dr Slaa, Lissu, Mnyika watafika lini Zanzibar. Sababu wamekatishwa tamaa na CUF.

Kwa maoni yangu CUF imewakatisha tamaa wanachama wake pamoja na washabiki wake ushahidi ni uchaguzi wa Igunga. Kwa aliyeandika Thread nionavyo mimi CUF inapoisakama CDM, inaisadia sana. Kwa maoni ya kawaida CUF si chama cha upinzani tena na hawana maelezo ya kuwaeleza wananchi kivinginevyo. Kwa kuhitimisha WAMEPOTEZA TUNU muhimu ambayo wote tulikuwa tunaitegemea
 
Kwa aliyeandika Thread nionavyo mimi CUF inapoisakama CDM, inaisadia sana. Kwa maoni ya kawaida CUF si chama cha upinzani tena na hawana maelezo ya kuwaeleza wananchi kivinginevyo. Kwa kuhitimisha WAMEPOTEZA TUNU muhimu ambayo wote tulikuwa tunaitegemea

Inawezekana ikawa inasaidia, lakini inachelewesha vuguvugu la madiliko ambayo hata wana CCM wanayatarajia
 
CUF inapoisakama CHADEMA
Chama cha CUF kimeibuka kuwa mpinzani mkubwa wa CHADEMA hata katika mambo ambayo chenyewe kilikuwa kikiyaamini kilipokuwa chama kikuu cha upinzani. CUF hawajiulizi ni vipi CHADEMA imepata umaarufu wa ghafla namna hii. Kwa mtazamo wangu, umaarufu wa CHADEMA sio wa ghafla bali ulijengwa taratibu. Zifuatazo ni miongoni mwa tofauti za utaratibu ndani ya vyama hivi.

  1. Tangu kuanzishwa, CHADEMA imekuwa na wenyeviti watatu na wawili waliostaafu bado ni wanachama wenye kuheshimika ndani ya CHADEMA tofauti na CUF yenye king'ang'anizi asiyependa mabadiliko.
(James Mapalala, Musobi, Lipumba)
  1. CHADEMA kimezushiwa kuwa na udini baada ya CCM kuona nguvu yake. Hali ya CHADEMA ni tofauti na CUF ambapo mwaka 1995 mwenyekiti wake alipiga kampeni misikitini wazi wazi na katika mikutano yake utakuta ni vi-barghashia vinatawala (mjini wanakaa waislam wengi, unapoenda mikoani mchanganyiko wanashiriki mikutano, hata hivyo waislam sio watanzania kuna ubaya gani kusapoti chama wanachotaka), na hiyo ilikuwa sera ya CCM badala ya kueleza sera na mafanikio ya project zao ambazo hawana wakawa wanaligawa taifa kwa misingi ya kidini; sasa inaelekea CHADEMA imechukua kozi ya baba yao CCM (Slaa ameletwa kuua upinzani na ndio maana hata hajapata misukosuko ya kisiasa kama walivyopewa CUF na wananchi kutoka kwa MAHITA; ndio maana wakaanzisha strategy nyengine ili wananchi wapate kujiletea maendeleo yao badala ya kuswekwa jela kila siku)
  2. CHADEMA imebadilisha karata ya ugombea urais baada ya Mbowe kujaribu bila mafanikio ndipo ilipomleta Slaa aliyetokea kuwa kipenzi cha wengi tofauti na Lipumba tunayemtarajia tena 2015 (CUF wanachama wao ndio itakuwa wamewapitisha hao, si waligombea wengi tu).
  3. Dr. Slaa wa CHADEMA amekuwa maarufu zaidi kwa staili ya yake kulipua mabomu bungeni na kuwataja mafisadi bila woga tofauti na Lipumba ambaye hajawahi kukemea ufisadi kwa besi (EPA, Richmond alikemea nani; si ni Hamad Rashid alimpa kazi hiyo Zitto Kabwe bungeni afuatilie masuali ya Richmond, baadae Hamad Rashid akaitikisa serikali kama hawakutoa ripoti ya Richmond Bungeni basi wataitowa wao wapinzani).
  4. CHADEMA ni walifanya ujanja kwa kuiga staili ya Obama kufanya kampeni kupitia mitandao ya simu na internet na CUF walifikiri haitawasaidia kwani vijana wengi walionekana kutopenda siasa, ikala kwao (miaka ya 1995 ni watanzania wangapi walikuwa na simu??).
  5. CHADEMA walitengua msemo wa nabii hakubaliki nyumbani kwa kuchukua jimbo analotoka mwenyekiti wao na katibu aliyekuwa akigombea urais, tofauti na CUF waliopoteza nyumbani kwa mwenyekiti. Hii inatokana na tofauti ya kuwekeza ambapo CUF wamewekeza zaidi visiwani huku wakiutaka urais wa muungano (hapo ndio kwenye tatizo la hao CUF, wanahubiri amani tu, hata cha kwao mpaka wapewe; wakati CCM ni majambazi. Wamepata viti vingi tu mara hii kama vile Tanga, Mtwara, Tabora; ila kwasababu walisubiri kupewa majambazi CCM wakayachukua; CHADEMA ni mtoto wao ambaye karibuni atasulubiwa na majambazi CCM baada ya kumaliza kazi ya kuwaondosha CUF, ndio kazi walopewa CHADEMA na CCM).
  6. Wakati CUF wanazinduka kumleta machachari Mtatiro katika siasa zao wanasahau kuwa CHADEMA waliliona hilo mapema na kuwa na vijana kama Mnyika, Zitto, Kafulila, nk (walikuwa nao wengi, lakini vijana ndio mhimili wa taifa hili; badala ya kuwapa fursa majambazi kuwasweka jela CUF imewataka vijana wafanye kazi ili waokoe uchumi wa taifa hili,; lakini kwa mtoto wa nyika CDM haguswi kwasababu lengo ni lile la kuumaliza upinzani wa kweli - CUF ambao ndio alternative ya kuendesha nchi hii)
  7. Wazee wa CHADEMA hawaangalii zaidi wao wanataka nini, bali watu wanataka nini. Ndio maana mwanamuziki Sugu ambaye kwa kauli za awali za wapinzani wake walimwita mhuni, akawekwa kulikwaa jimbo. CCM nao kama CHADEMA walikuwa wakiandamana na kundi kubwa la wasanii wakiongozwa na Joseph Haule. CUF walidhani kipaza sauti pekee kinatosha.
  8. Nguvu kubwa ya kimaamuzi CCM ipo kwa mwenyekiti, CHADEMA ipo kwa baraza kuu na CUF ipo kwa katibu mkuu (CUF nguvu iko kwa wananchi, Baraza kuu ni kutia baraka zao tu baada ya kutoka kwa wananchi).
  9. CHADEMA, hata kama wanakosea; wana kawaida ya kutoa tamko pale jambo linapojitokeza. Tofauti na CUF ambao wana kawaida ya kusubiri kwanza kuona upepo unavumaje (busara na hekima ni kitu muhimu zaidi hasa unapozungumzia usalama wa wananchi wa taifa hili, na ndio tatizo la baadhi ya vyama kukurupuka tu bila ya kuangalia outcome itakuwaje. CUF ilipoona CCm hawana nia njema ndio wakabadilisha mkakati ili vijana wa taifa hili wasiuliwe na kuswekwa rumande bure. CUF ndio inayoweka misingi ya demokrasia; CDM sasahivi wanakula hayo matunda ambayo yameanzishwa na CUF. Hakuna jipya linalofanywa na CDM sasahivi; hata sera za kuiga tu, hawana za kwao hasa).
  10. Siasa ni kama dini ambapo muumini huvutwa na mlengo wa chama. Kimataifa, CHADEMA kimefuata mlengo wa kulia na ndio maana kinahusishwa na vyama kama conservative cha Uingereza na Republican cha Marekani, na CCM mlengo wa shoto kikihusishwa na Labor cha Uingereza na Democrats cha US. CUF kama chama, mlengo wake hauko wazi (usishangae ikawa ni chama kinachotumiwa na agency za kijasusi, manake mara nyingi hupata misaada kutoka USA, kuja kumaliza hizo resources zilizobaki, usijeukashangaa wakajawakataifisha mali zote za nchi na kuwapa hao mabeberu. CUF wao wana sera ya utajirisho; socialist [sio mabepari kuchukua kutoka kwa masikini, wala sio makomunisti ambao pia wanatumia nguvu za wananchi kujilimbikizia mali]).
Ni dhahiri basi CUF wana kazi kubwa ya kurekebisha kuanzia ndani ndipo watoke uwani. Umaarufu wa CHADEMA usiwatie wivu hata wakaamua kuwapinga katika masuala yenye manufaa kwa Watanzania. Kushiriki katika serikali ya Zanzibar kusiwe chanzo cha uswahiba na serikali ya Tanzania na kuwa mpinzani wa wapinzani wenzako. (tayari wao wana misingi mizuri tu; unaona hata katiba walishadraft zamani; hata hao CCM hujui wanachokitaka nini; CDM wao wanarukia tu kama kawaida yao; hem waulize wanayo wao draft yao atleast inayoonyesha nini wanataka; wanarukia tu kama walosutufu karibuni. CDM wamewakanusha wapinzani wote, hawataki mashirikiano hata na hao NCCR angalau; wanatutilisha aibu kwa ukuaji wa demokrasia ya Tanzania).

Alojibu mada hii ni mwanademokrasia halisi, hajawahi kuwa na chama chochote cha siasa; ni mpenzi mkubwa wa demokrasia na mpira wa miguu. Lengo la kujibu ni kuwa tuleteni maendeleo katika jamii yetu; hata kama ni CHADEMA wewe basi tuwekeni strategy zetu za kuliletea maendeleo taifa hili (CCM hawaleti; CHADEMA wamekuja na stile ile ile ya CCM) sasa hawa wananchi watapata lini maendeleo. Au tuwashirikishe kwenye mikutano tu kila siku wakati wao wanachukua maposho; wananchi wanashindwa hata kwenda kondeni kulima, halafu wanalala na njaa. Tuamkeni WaTanzania, maendeleo hayaji kwa siasa uchwara, bali ni mikakati mizuri. Hata kama CDM wakiwa na mikakati mizuri basi wanaweza kuleta maendeleo wakiwa ni wapinzani (nakumbuka CUF/CDM walikuwa na sera ya kuondosha karo kwa wanafunzi, na zile sehemu walizoshinda kwenye serikali za mitaa wamefanya vizuri), sasa hayo ndio muhimu.
 
Alojibu mada hii ni mwanademokrasia halisi, hajawahi kuwa na chama chochote cha siasa; ni mpenzi mkubwa wa demokrasia na mpira wa miguu. Lengo la kujibu ni kuwa tuleteni maendeleo katika jamii yetu; hata kama ni CHADEMA wewe basi tuwekeni strategy zetu za kuliletea maendeleo taifa hili (CCM hawaleti; CHADEMA wamekuja na stile ile ile ya CCM) sasa hawa wananchi watapata lini maendeleo. Au tuwashirikishe kwenye mikutano tu kila siku wakati wao wanachukua maposho; wananchi wanashindwa hata kwenda kondeni kulima, halafu wanalala na njaa. Tuamkeni WaTanzania, maendeleo hayaji kwa siasa uchwara, bali ni mikakati mizuri. Hata kama CDM wakiwa na mikakati mizuri basi wanaweza kuleta maendeleo wakiwa ni wapinzani (nakumbuka CUF/CDM walikuwa na sera ya kuondosha karo kwa wanafunzi, na zile sehemu walizoshinda kwenye serikali za mitaa wamefanya vizuri), sasa hayo ndio muhimu.

Pamoja na kukugongea kibatani cha 'like' bado nina hoja kwa majibu yako Mak2


  1. James Mapalala alikwisha kimbia siku nyingi na kuunda chama kingine bila mafanikio. Musobi baada ya kushindwa na Lipumba hajasikika tena. Wastaafu ni hazina katika chama, so ni vyema kuenziwa kwa ajili ya uhai wa chama.
  2. Tatizo la waumini wa dini Fulani kukipenda zaidi chama Fulani ni dalili kuwa c hama hicho kina ajenda Fulani na dini hiyo na sijambo jema kwa mustakabali wa umoja na amani ya nchi yetu. Leo hii Tz, rais ni muislamu na makamu ni muislamu na mambo yanaendelea. Jambo hilo haliwezekani kule Nigeria kwenye mpasuko wa kidini na ndipo tutakapoishia kama CUF itaendelea kuwavutia zaidi waislamu.
  3. Unaposema ni sahihi CUF kung'ang'ania yule yule kwa sababu wanachama ndio wanamchagua tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi ni sahihi, lakini anapaswa kupima mvuto wake kwa jamii ya wapiga kura kama alivyofanya Mbowe na kuamua kuchukua ubunge anaoweza kushinda kuliko urais.
  4. Umesema vema kuwa EPA, Richmond aliyekemea sana ni Hamad Rashid. Sasa mbona kapigwa chini hata uongozi wa kambi isiyokuwa rasmi na CUF. Kwa nini asingepewa nafasi zaidi ili kuijenga CUF? Na hapo ndio tofauti na CHADEMA inapoonekana wazi. Wasemaji sana ndio wanapata nafasi. Unapomwengua Hamad na kumweka Mnyaa ndio najenga nguvu ya upinzani?
  5. Umeuliza mwaka 1995 ni watanzania wangapi waliokuwa na simu. Tuachane na 1995, vipi kuhusu 2010? Usikimbie hoja kwa kurudisha tarehe nyuma. CUF ilikosa ubunifu wa kuwavutia vijana kwa kudhani vipaza sauti vinatosha wakati wenzao wanafanya kampeni hadi ‘feisbuku'
  6. Nadhani badala ya kuendelea kulalamika kuibiwa kura, jaribu kujiuliza nini kimeiondoa CUF nafasi ya pili hadi ya tatu?
  7. Umesema CUF ina vijana wengi machachari…naomba majina
  8. Naona hoja #8 imekushinda
  9. Unaposema nguvu kubwa ya maamuzi ipo kwa wananchi una maana gani? Au unaungana na kaulimbiu ya CDM ya people's power? Usikimbie ukweli, nguvu ya maamuzi ktk CUF ipo kwa Maalim Sharif Hamad
  10. Sijaelewa unaposema CHADEMA wanakula matunda ya CUF…fafanua
  11. Nimefurahi kusikia kuwa CUF wana sera ya utajirisho, sasa ni kazi kwa kuiuza kwa wapiga kura ili tuifahamu. Wakiikalia kwenye mabuku yao itaendelea kula kwao
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom