CUF inapoisakama CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF inapoisakama CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crucifix, Dec 1, 2011.

 1. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Chama cha CUF kimeibuka kuwa mpinzani mkubwa wa CHADEMA hata katika mambo ambayo chenyewe kilikuwa kikiyaamini kilipokuwa chama kikuu cha upinzani. CUF hawajiulizi ni vipi CHADEMA imepata umaarufu wa ghafla namna hii. Kwa mtazamo wangu, umaarufu wa CHADEMA sio wa ghafla bali ulijengwa taratibu. Zifuatazo ni miongoni mwa tofauti za utaratibu ndani ya vyama hivi.


  1. Tangu kuanzishwa, CHADEMA imekuwa na wenyeviti watatu na wawili waliostaafu bado ni wanachama wenye kuheshimika ndani ya CHADEMA tofauti na CUF yenye king'ang'anizi asiyependa mabadiliko.
  2. CHADEMA kimezushiwa kuwa na udini baada ya CCM kuona nguvu yake. Hali ya CHADEMA ni tofauti na CUF ambapo mwaka 1995 mwenyekiti wake alipiga kampeni misikitini wazi wazi na katika mikutano yake utakuta ni vi-barghashia vinatawala.
  3. CHADEMA imebadilisha karata ya ugombea urais baada ya Mbowe kujaribu bila mafanikio ndipo ilipomleta Slaa aliyetokea kuwa kipenzi cha wengi tofauti na Lipumba tunayemtarajia tena 2015.
  4. Dr. Slaa wa CHADEMA amekuwa maarufu zaidi kwa staili ya yake kulipua mabomu bungeni na kuwataja mafisadi bila woga tofauti na Lipumba ambaye hajawahi kukemea ufisadi kwa besi.
  5. CHADEMA ni walifanya ujanja kwa kuiga staili ya Obama kufanya kampeni kupitia mitandao ya simu na internet na CUF walifikiri haitawasaidia kwani vijana wengi walionekana kutopenda siasa, ikala kwao.
  6. CHADEMA walitengua msemo wa nabii hakubaliki nyumbani kwa kuchukua jimbo analotoka mwenyekiti wao na katibu aliyekuwa akigombea urais, tofauti na CUF waliopoteza nyumbani kwa mwenyekiti. Hii inatokana na tofauti ya kuwekeza ambapo CUF wamewekeza zaidi visiwani huku wakiutaka urais wa muungano.
  7. Wakati CUF wanazinduka kumleta machachari Mtatiro katika siasa zao wanasahau kuwa CHADEMA waliliona hilo mapema na kuwa na vijana kama Mnyika, Zitto, Kafulila, nk
  8. Wazee wa CHADEMA hawaangalii zaidi wao wanataka nini, bali watu wanataka nini. Ndio maana mwanamuziki Sugu ambaye kwa kauli za awali za wapinzani wake walimwita mhuni, akawekwa kulikwaa jimbo. CCM nao kama CHADEMA walikuwa wakiandamana na kundi kubwa la wasanii wakiongozwa na Joseph Haule. CUF walidhani kipaza sauti pekee kinatosha.
  9. Nguvu kubwa ya kimaamuzi CCM ipo kwa mwenyekiti, CHADEMA ipo kwa baraza kuu na CUF ipo kwa katibu mkuu.
  10. CHADEMA, hata kama wanakosea; wana kawaida ya kutoa tamko pale jambo linapojitokeza. Tofauti na CUF ambao wana kawaida ya kusubiri kwanza kuona upepo unavumaje.
  11. Siasa ni kama dini ambapo muumini huvutwa na mlengo wa chama. Kimataifa, CHADEMA kimefuata mlengo wa kulia na ndio maana kinahusishwa na vyama kama conservative cha Uingereza na Republican cha Marekani, na CCM mlengo wa shoto kikihusishwa na Labor cha Uingereza na Democrats cha US. CUF kama chama, mlengo wake hauko wazi.
  Ni dhahiri basi CUF wana kazi kubwa ya kurekebisha kuanzia ndani ndipo watoke uwani. Umaarufu wa CHADEMA usiwatie wivu hata wakaamua kuwapinga katika masuala yenye manufaa kwa Watanzania. Kushiriki katika serikali ya Zanzibar kusiwe chanzo cha uswahiba na serikali ya Tanzania na kuwa mpinzani wa wapinzani wenzako.

  angalizo : mwanzisha sredi sio mwana CUF wala CHADEMA
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  chademna kilipoanza kutumia helikopta walisema kinatumia vibaya hela ila mwisho wa siku nao walianza kutumia za kuazima.
   
 3. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 479
  Trophy Points: 80
  Ngojea wenye CUF yao waje!!!
   
 4. Y

  Yetuwote Senior Member

  #4
  Dec 1, 2011
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye red, siyo kweli.
   
 5. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,719
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  chadema kinaonekana ni chama cha ukombozi na kimelenga umri wote wakati CUF na CCM kimelenga kwa walioshiba tu.
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,303
  Likes Received: 22,105
  Trophy Points: 280
  CUF si ndio mama mwenyenyumba?
   
 7. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Umesahau...chadema walikuja na stail ya gwanda ambayo imekuwa kivutio kikubwa kwa marika yote....
   
 8. MANGI MASTA

  MANGI MASTA Senior Member

  #8
  Dec 1, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utawatambua kwa maneno:Mwandishi ni pure Chadema for comments zake za muda mrefu hapa JF.

  CCM ni chama kinachoongoza sana kuisakama CDM mbona hawasemi hao unarukia CUF?
  CDM ndo kila Siku inaibua propaganda za kuichafua CUF kila wanaposimama kwenye majukwaa.Kwa vile mwandishi ni CDM iko hivyo ila angekuwa mtu asiye na mlengwa wa chama chochote na anayefikiri sawia kwa fikra kinzani bila shaka thread ingesomeka"CHADEMA IPOISAKAMA CUF"
   
 9. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu, mimi niliiva katika ile kanuni isemayo, "nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko". Hivyo usinihusishe na CHADEMA eti kwa sababu nimewasemea uzuri. Mbona wa CCM wengi tu waisifia CDM? Kusema jambo jema la waislamu haina maana nimeacha wokovu na kusilimu.

  "propaganda" pekee ya CDM kuhusu CUF ni jina jipya CCM B. Lakini CUF inafuatilia mambo ya msingi wanayoamua CDM na kuwashutumu. Mfano viongozi wa CUF walilaani maandamano ya CDM Arusha wakisema eti hiyo ni njia ya kizamani. Njia gani ya kizamani iliyowatoa madarakani marais wa sasa Misri na Tunisia. Msingi wa hoja yangu ni kwa CUF kuacha kuisakama CHADEMA na kumtetea mtanzania kwa kila hali. Juzi tumesikia posho za ma-MP zimepanda. Tayari wabunge wa CDM wameshakoroma. CUF kimya. Lakini waliposikia wenzao wamekunywa juisi ikulu nao hao wako mbioni kwenda. Mengine utamalizia mwenyewe.......
   
 10. M

  Mwera JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada ktk point no2 umesema cuf walikua wanafanya kampeni zawazi msikitini,pia hata cdm walifanya kampeni zawazi makanisani hasa katoliki,tena na ushahidi wa cd za picha tunao,slaa alikua analala makanisani nakufanyiwa kampeni zawazi namapadri wenzie,ukibisha cd tunazo zakampeni za cdm naslaa makanisani,usitukane mamba kabla hujavuka mto.
   
 11. CULCULUS

  CULCULUS Senior Member

  #11
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rekebisha hapo kwenye red.

   
 12. T

  Topical JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Chadema our agent (ccm) to divide upinzani (take it from me)

  Chadema haitaunganisha nguvu za wapinzani kama walivyotaka kufanya CUF

  Kwasababu tunawalipa kwa kugawa wapinzani

  hint Mbowe analipwa na EL, Slaa analipwa na Sabodo, Zitto analipwa na RA

  Wengine watoto tu hawana bei..bendera fuata upepo..
   
 13. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  sitaki kuanzisha mjadala wa kidini hapa. Nafurahi kuwa hujakanusha Lipumba kufanya kampeni misikitini. Kama una video ya Slaa akifanya kampeni kanisani weka link youtube, nitaondoa point no 2
   
 14. T

  Topical JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Waraka wa maaskofu hujasoma, tafuta uko humu ndani..lol
   
 15. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  ccm si ndio baba Fataki kwa vibinti kama tlp, na udp?
   
 16. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #16
  Dec 1, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  CUF ni wake za magamba hivyo huwezi shangaa hilo.
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Dec 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Magamba na wake na nyumba ndogo nyingi ikiwemo chadema
   
 18. y

  yaya JF-Expert Member

  #18
  Dec 1, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ziweke mkuu, ili tuone na kutambua kwamba kweli ulimaanisha ulichokisema, au kukiandika humu jamvini.Ukisema kitu weka na ushahidi, kudhihirisha kwamba kweli wewe ni great thinker na ili kuondoa ubishi. Naamini utatekeleza na si kutishia nyau, sawa Mkuu?
   
 19. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #19
  Dec 1, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Baada ya mseto cuf imekua jumuia ya ccm kama uwt na nyinginezo. Hamna kitu pale!
   
 20. M

  Mwera JF-Expert Member

  #20
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  toa wewe kwanza ushahidi kamili kua lipumba alifanya kampeni misikitini namimi ukitoa ushahd kua libumba alifanya kampeni msikitini nami naimwaga cd ya slaa akiomba kura makanisani.
   
Loading...