3. CHADEMA imebadilisha karata ya ugombea urais baada ya Mbowe kujaribu mara mbili bila mafanikio ndipo ilipomleta Slaa aliyetokea kuwa kipenzi cha wengi tofauti na Lipumba tunayemtarajia tena 2015.
Chama cha CUF kimeibuka kuwa mpinzani mkubwa wa CHADEMA hata katika mambo ambayo chenyewe kilikuwa kikiyaamini kilipokuwa chama kikuu cha upinzani. CUF hawajiulizi ni vipi CHADEMA imepata umaarufu wa ghafla namna hii. Kwa mtazamo wangu, umaarufu wa CHADEMA sio wa ghafla bali ulijengwa taratibu. Zifuatazo ni miongoni mwa tofauti za utaratibu ndani ya vyama hivi.
Ni dhahiri basi CUF wana kazi kubwa ya kurekebisha kuanzia ndani ndipo watoke uwani. Umaarufu wa CHADEMA usiwatie wivu hata wakaamua kuwapinga katika masuala yenye manufaa kwa Watanzania. Kushiriki katika serikali ya Zanzibar kusiwe chanzo cha uswahiba na serikali ya Tanzania na kuwa mpinzani wa wapinzani wenzako.
- Tangu kuanzishwa, CHADEMA imekuwa na wenyeviti watatu na wawili waliostaafu bado ni wanachama wenye kuheshimika ndani ya CHADEMA tofauti na CUF yenye king'ang'anizi asiyependa mabadiliko.
- CHADEMA kimezushiwa kuwa na udini baada ya CCM kuona nguvu yake. Hali ya CHADEMA ni tofauti na CUF ambapo mwaka 1995 mwenyekiti wake alipiga kampeni misikitini wazi wazi na katika mikutano yake utakuta ni vi-barghashia vinatawala.
- CHADEMA imebadilisha karata ya ugombea urais baada ya Mbowe kujaribu mara mbili bila mafanikio ndipo ilipomleta Slaa aliyetokea kuwa kipenzi cha wengi tofauti na Lipumba tunayemtarajia tena 2015.
- Dr. Slaa wa CHADEMA amekuwa maarufu zaidi kwa staili ya yake kulipua mabomu bungeni na kuwataja mafisadi bila woga tofauti na Lipumba ambaye hajawahi kukemea ufisadi kwa besi.
- CHADEMA ni walifanya ujanja kwa kuiga staili ya Obama kufanya kampeni kupitia mitandao ya simu na internet na CUF walifikiri haitawasaidia kwani vijana wengi walionekana kutopenda siasa, ikala kwao.
- CHADEMA walitengua msemo wa nabii hakubaliki nyumbani kwa kuchukua jimbo analotoka mwenyekiti wao na katibu aliyekuwa akigombea urais, tofauti na CUF waliopoteza nyumbani kwa mwenyekiti. Hii inatokana na tofauti ya kuwekeza ambapo CUF wamewekeza zaidi visiwani huku wakiutaka urais wa muungano.
- Wakati CUF wanazinduka kumleta machachari Mtatiro katika siasa zao wanasahau kuwa CHADEMA waliliona hilo mapema na kuwa na vijana kama Mnyika, Zitto, Kafulila, nk
- Wazee wa CHADEMA hawaangalii zaidi wao wanataka nini, bali watu wanataka nini. Ndio maana mwanamuziki Sugu ambaye kwa kauli za awali za wapinzani wake walimwita mhuni, akawekwa kulikwaa jimbo. CCM nao kama CHADEMA walikuwa wakiandamana na kundi kubwa la wasanii wakiongozwa na Joseph Haule. CUF walidhani kipaza sauti pekee kinatosha.
- Nguvu kubwa ya kimaamuzi CCM ipo kwa mwenyekiti, CHADEMA ipo kwa baraza kuu na CUF ipo kwa katibu mkuu.
- CHADEMA, hata kama wanakosea; wana kawaida ya kutoa tamko pale jambo linapojitokeza. Tofauti na CUF ambao wana kawaida ya kusubiri kwanza kuona upepo unavumaje.
- Siasa ni kama dini ambapo muumini huvutwa na mlengo wa chama. Kimataifa, CHADEMA kimefuata mlengo wa kulia na ndio maana kinahusishwa na vyama kama conservative cha Uingereza na Republican cha Marekani, na CCM mlengo wa shoto kikihusishwa na Labor cha Uingereza na Democrats cha US. CUF kama chama, mlengo wake hauko wazi.
angalizo : mwanzisha sredi sio mwana CUF wala CHADEMA
Utawatambua kwa maneno:Mwandishi ni pure Chadema for comments zake za muda mrefu hapa JF.
CCM ni chama kinachoongoza sana kuisakama CDM mbona hawasemi hao unarukia CUF?
CDM ndo kila Siku inaibua propaganda za kuichafua CUF kila wanaposimama kwenye majukwaa.Kwa vile mwandishi ni CDM iko hivyo ila angekuwa mtu asiye na mlengwa wa chama chochote na anayefikiri sawia kwa fikra kinzani bila shaka thread ingesomeka"CHADEMA IPOISAKAMA CUF"
Chama cha CUF kimeibuka kuwa mpinzani mkubwa wa CHADEMA hata katika mambo ambayo chenyewe kilikuwa kikiyaamini kilipokuwa chama kikuu cha upinzani. CUF hawajiulizi ni vipi CHADEMA imepata umaarufu wa ghafla namna hii. Kwa mtazamo wangu, umaarufu wa CHADEMA sio wa ghafla bali ulijengwa taratibu. Zifuatazo ni miongoni mwa tofauti za utaratibu ndani ya vyama hivi.
- Tangu kuanzishwa, CHADEMA imekuwa na wenyeviti watatu na wawili waliostaafu bado ni wanachama wenye kuheshimika ndani ya CHADEMA tofauti na CUF yenye king'ang'anizi asiyependa mabadiliko.
- CHADEMA kimezushiwa kuwa na udini baada ya CCM kuona nguvu yake. Hali ya CHADEMA ni tofauti na CUF ambapo mwaka 1995 mwenyekiti wake alipiga kampeni misikitini wazi wazi na katika mikutano yake utakuta ni vi-barghashia vinatawala.
- CHADEMA imebadilisha karata ya ugombea urais baada ya Mbowe kujaribu mara mbili bila mafanikio ndipo ilipomleta Slaa aliyetokea kuwa kipenzi cha wengi tofauti na Lipumba tunayemtarajia tena 2015.
angalizo : mwanzisha sredi sio mwana CUF wala CHADEMA
Mtoa mada ktk point no2 umesema cuf walikua wanafanya kampeni zawazi msikitini,pia hata cdm walifanya kampeni zawazi makanisani hasa katoliki,tena na ushahidi wa cd za picha tunao,slaa alikua analala makanisani nakufanyiwa kampeni zawazi namapadri wenzie,ukibisha cd tunazo zakampeni za cdm naslaa makanisani,usitukane mamba kabla hujavuka mto.
sitaki kuanzisha mjadala wa kidini hapa. Nafurahi kuwa hujakanusha Lipumba kufanya kampeni misikitini. Kama una video ya Slaa akifanya kampeni kanisani weka link youtube, nitaondoa point no 2
CUF si ndio mama mwenyenyumba?
CUF ni wake za magamba hivyo huwezi shangaa hilo.
Ziweke mkuu, ili tuone na kutambua kwamba kweli ulimaanisha ulichokisema, au kukiandika humu jamvini.Ukisema kitu weka na ushahidi, kudhihirisha kwamba kweli wewe ni great thinker na ili kuondoa ubishi. Naamini utatekeleza na si kutishia nyau, sawa Mkuu?Mtoa mada ktk point no2 umesema cuf walikua wanafanya kampeni zawazi msikitini,pia hata cdm walifanya kampeni zawazi makanisani hasa katoliki,tena na ushahidi wa cd za picha tunao,slaa alikua analala makanisani nakufanyiwa kampeni zawazi namapadri wenzie,ukibisha cd tunazo zakampeni za cdm naslaa makanisani,usitukane mamba kabla hujavuka mto.
toa wewe kwanza ushahidi kamili kua lipumba alifanya kampeni misikitini namimi ukitoa ushahd kua libumba alifanya kampeni msikitini nami naimwaga cd ya slaa akiomba kura makanisani.sitaki kuanzisha mjadala wa kidini hapa. Nafurahi kuwa hujakanusha Lipumba kufanya kampeni misikitini. Kama una video ya Slaa akifanya kampeni kanisani weka link youtube, nitaondoa point no 2