CUF Dodoma hawamtaki Seif | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF Dodoma hawamtaki Seif

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kurunzi, Dec 19, 2011.

 1. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kwa mujibu wa star tv new, viongozi wa ngazi zote wilaya ya Dodoma mjini wamemtaka kaitibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif kuachia ngazi kwa kushindwa kukikongoza vema chama hicho kwa nafasi yake ya ukatibu mkuu.
   
 2. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kumekucha!
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Huyu Maalim Seif akubali kuwapisha na wengine bana... Tangu nipo mtoto naona yeye tu anaongoza na Lipumba wake.!
   
 4. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwani CUF ina viongozi na wafuasi Dodoma?
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,595
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  natamani ingekuwa NCCR hivi hivi...viva hamad viva...
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  ndo tatizo la kugombea urais kwa miaka 20 mfululizo. Hv hakuna wengine wanaoweza kuongoza humo kafu?
   
 7. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Watu mnaleta mchezo, jamaa alipigika kahangaika kavutwa na CCM sasa yuko mezani, uso umepata nuru, eti aachie ngazi....patachimbika!!!!!
   
 8. K

  Kivia JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hao ni mamluki tu. Wanafuata upepo. Wenzao wa manzese-chechnya washaomba msamaha kuwa walitumiwa bila kujijua.
   
 9. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  But ni kweli jamaa yupo katika nafasi hiyo miaka nenda rudi, its like chama ni lake yeye tu! ndiye mwenye dhamana pia ya kugombea
   
 10. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbona Zambian Hero wenu Satta aligombea zaidi ya mara nne?
   
 11. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=2]CUF Dodoma wamtaka Maalim Seif kuachia Ukatibu Mkuu[/h]


  Na Mwandishi wetu  20th December 2011

  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad


  Mgogoro wa uongozi ulioobuka ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) ukiwahusisha Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, umeendelea kukitafuna chama hicho, baada ya uongozi wa chama hicho mkoa wa Dodoma kutoa tamko kali dhidi ya Maalim Seif.

  Katika tamko hilo lililotolewa jana mjini hapa, viongozi hao walimjia juu Maalim Seif kwa kumtaka aachie ngazi kwenye nyadhifa moja ili wengine waweze kukitumikia chama hicho ipasavyo.

  Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar iliyoundwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, ametakiwa kuachia ngazi katika nafasi ya ukatibu mkuu ili wengine waweze kukiendeleza chama hicho.

  Shinikizo la kumtaka Malim Seif aachie nafasi hiyo lilianzishwa na Hamad Rashid Mohamed, ambaye ni mmoja wa waasisi wa CUF, kwa hoja kuwa Maalim Seif kwa kubakia na nyadhifa mbili inakifanya chama hicho kuendelea kupoteza umaarufu.

  Viongozi wa Dodoma ambao wamewawakilisha wanachama wanzao ni, Haruna Kamwelwe (Mwenyekiti Wilaya), Majid Ally (Katibu), George Mwanjilwa, Mohammed Kimbwangali, Aman Yusuf, Hussein Mkomwa, Farida Abdallah, Juma Ikaba na Omary Lule.

  Tamko hilo lilitolewa jana na Katibu wa chama hicho wilaya ya Dodoma Mjini, Majid Ally, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

  Alisema kofia mbili anazozitumikia Maalim Seif kwa hivi sasa zimemfanya ashindwe kutimiza majukumu yake kwa ufanisi, hivyo kupelekea chama hicho kupoteza hadhi yake hasa upande wa Tanzania Bara.

  Alisema Seif ameshindwa kufanya mkutano hata mmoja wa hadhara hata katika mkoa mmoja katika maeneo ya Tanzania Bara, hali ambayo inasababisha chama hicho kuendelea kupoteza umaarufu na mwelekeo wake.

  Akizungumzia mgogoro uliopo ndani ya chama hicho, Katibu huyo alisema chama hicho kipo katika wakati mgumu, ambapo kama viongozi hao hawatakuwa waangalifu, watawapoteza wanachama hata wale waliobaki.

  "Cuf ilikuwa inashika nafasi ya pili katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2005 ambapo mgombea wetu alipata kura zaidi ya milioni moja, lakini mwaka jana katika Uchaguzi Mkuu chama chetu kiliambulia kupata wabunge wawili tu na mgombea wetu katika nafasi ya urais alipata kura laki sita…hali ambayo inatutisha sana, wanachama hatunabudi kutafuta dawa ya tatizo hili," alisema.

  Aliongeza kuwa ofisi nyingi za chama mikoani pia zimekufa kutokana na uongozi kushindwa kufikisha fedha za ruzuku, hali ambayo imesababisha wilaya nyingi kuendesha ofisi zao chini ya miti.

  Naye mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho wilayani hapa, Hussein Mkomwa, alitoa wito kwa uongozi wa chama hicho taifa kuyasikiliza kwa makini madai ya Rashid Mohamed na kuyapatia majibu na si kuendelea kulumbana.

  Mkomwa alisema kwa kuwa hivi sasa suala la mgogoro lipo katika vikao vya juu linashughulikiwa, wanasubiri kuona nini hatma ya mbunge huyo wa Wawi.

  Alisema kama uongozi utamvua uanachama mbunge huyo, wao wataendelea kumfuata popote atakapoelekea.

  "Hamad amekuwa akiuliza pesa zilizobaki katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Igunga ambapo zilibaki Sh. milioni 500 ambazo hazionekani wapi zilipo…pamoja na kuuliza vitu ambavyo ni vya msingi, lakini anaonekana kama analeta vurugu," alisema Mkomwa.

  Hamad Rashid ameshaeleza nia yake ya kuanzisha chama kipya ikiwa uongozi wa CUF utamng'oa.  CHANZO: NIPASHE
   
 12. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kazi ipo jiungeni na chama makini CDM, tatizo la wanacuf wengi ni elimu duni mindset zao zilikuwa zinashikiwa na seif sasa seif amepata alikuwa kuwa anakihitaji wamebaki njiapanda inamaana hata huyo HR akiwasaliti au kwenda CCM mtamfuata? Hakili za kushikiwa bwana!
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad


  Mgogoro wa uongozi ulioobuka ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) ukiwahusisha Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, umeendelea kukitafuna chama hicho,

  baada ya uongozi wa chama hicho mkoa wa Dodoma kutoa tamko kali dhidi ya Maalim Seif.


  Katika tamko hilo lililotolewa jana mjini hapa, viongozi hao walimjia juu Maalim Seif kwa kumtaka aachie ngazi kwenye nyadhifa moja ili wengine waweze kukitumikia chama hicho ipasavyo.


  Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar iliyoundwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, ametakiwa kuachia ngazi katika nafasi ya ukatibu mkuu ili

  wengine waweze kukiendeleza chama hicho.

  Shinikizo la kumtaka Malim Seif aachie nafasi hiyo lilianzishwa na Hamad

  Rashid Mohamed, ambaye ni mmoja wa waasisi wa CUF, kwa hoja kuwa Maalim Seif kwa kubakia na nyadhifa mbili inakifanya chama hicho kuendelea kupoteza umaarufu.

  Viongozi wa Dodoma ambao wamewawakilisha wanachama wanzao ni, Haruna Kamwelwe (Mwenyekiti Wilaya), Majid Ally (Katibu), George Mwanjilwa, Mohammed Kimbwangali, Aman Yusuf, Hussein Mkomwa, Farida Abdallah, Juma Ikaba na Omary Lule.


  Tamko hilo lilitolewa jana na Katibu wa chama hicho wilaya ya Dodoma Mjini, Majid Ally, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.


  Alisema kofia mbili anazozitumikia Maalim Seif kwa hivi sasa zimemfanya ashindwe kutimiza majukumu yake kwa ufanisi, hivyo kupelekea chama hicho kupoteza hadhi yake hasa upande wa Tanzania Bara.

  Alisema Seif ameshindwa kufanya mkutano hata mmoja wa hadhara hata katika mkoa mmoja katika maeneo ya

  Tanzania Bara, hali ambayo inasababisha chama hicho kuendelea kupoteza umaarufu na mwelekeo wake.

  Akizungumzia mgogoro uliopo ndani ya chama hicho, Katibu huyo alisema chama hicho kipo katika wakati mgumu, ambapo kama viongozi hao hawatakuwa waangalifu, watawapoteza wanachama hata wale waliobaki.


  “Cuf ilikuwa inashika nafasi ya pili katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2005 ambapo mgombea wetu alipata kura zaidi ya milioni moja, lakini mwaka jana katika Uchaguzi Mkuu chama chetu kiliambulia kupata wabunge wawili tu na mgombea wetu katika nafasi ya urais alipata kura laki sita…hali ambayo inatutisha sana, wanachama hatunabudi kutafuta dawa ya tatizo hili,” alisema.


  Aliongeza kuwa ofisi nyingi za chama mikoani pia zimekufa kutokana na uongozi kushindwa kufikisha fedha za ruzuku, hali ambayo imesababisha wilaya nyingi kuendesha ofisi zao chini ya miti.

  Naye mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho wilayani hapa, Hussein Mkomwa, alitoa wito kwa uongozi wa

  chama hicho taifa kuyasikiliza kwa makini madai ya Rashid Mohamed na kuyapatia majibu na si kuendelea kulumbana.

  Mkomwa alisema kwa kuwa hivi sasa suala la mgogoro lipo katika vikao vya juu linashughulikiwa, wanasubiri kuona nini hatma ya mbunge huyo wa Wawi.


  Alisema kama uongozi utamvua uanachama mbunge huyo, wao wataendelea kumfuata popote atakapoelekea.

  “Hamad amekuwa akiuliza pesa zilizobaki katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Igunga ambapo zilibaki Sh.

  milioni 500 ambazo hazionekani wapi zilipo…pamoja na kuuliza vitu ambavyo ni vya msingi, lakini anaonekana kama analeta vurugu,” alisema Mkomwa.

  Hamad Rashid ameshaeleza nia yake ya kuanzisha chama kipya ikiwa uongozi wa CUF utamng’oa.  CHANZO: NIPASHE

   
 14. M

  Marytina JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Tunazubili kauri sa balasa la maulama
   
Loading...