CUF-chama cha wananchi Tumebaini mpango wa CCM kuwarubuni madiwani wetu saba 7 Jijini TANGA

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234

THE CIVIC UNITED FRONT

(CUF – Chama Cha Wananchi)

Office of The Secretary General

P.O. Box 10979
Dar Es Salaam, Tanzania



TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI.

CUF-Chama Cha Wananchi kimebaini mpango wa Muendelezo wa Viongozi wa CCM kuwa rubuni na kuwahamisha Madiwani wake Saba (7) wa Jiji la Tanga kijiunga na Chama hicho .



MADIWANI HAO NA KATA ZAO NI

NASSORO MOHAMMED wa Kata ya Tongoni

MOHAMMED ANIU wa Kata ya Tangasisi

MSWAHIRI NJAMA wa Kata ya Chongoleani

HABIBU MPA wa Kata ya Ngamiani Kati

SAIDI ALEI wa Kata ya Masiwani

AKIDA OMARI AKIDA wa Kata ya Ngamiani Kaskazini

SELEMANI LDDY MBAROUK wa Kata ya Majengo.

Waheshimiwa Wananchi na Wanachama wetu , Madiwani tajwa hapo juu wanatarajia kujiunga na CCM kesho kwenye Mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM utaofanyika Tanga Kwa hivyo hampaswi kushtuka bali tukio hilo linapaswa kuwaongezea Chachu na Morali ya kuiondoa CCM kwenye Uchaguzi Mkuu kama mlivyofanya Mwaka 2015.


Upinzani Kwa Jiji la Tanga si Kwa hao wanaotarajiwa kujiunga na CCM bali upinzani upo nyoyoni mwa Wanatanga Kwa kuzingatia historia ya Jiji la Tanga.

Mwisho CUF-Chama Cha Wananchi kinawataka CCM waache kujisumbua Kwa kununua Madiwani wa CUF kwani hilo si suluhisho la chuki ya Wananchi dhidi ya CCM.

CCM inapaswa kujikita katika kuboresha huduma za Jamii , kuzalisha Ajira na kuongeza pato la Mtanzaji na Taifa Kwa ujumla ndio njia pekee itayofanya Wananchi si wa Tanga tu bali maeneo mengi kufikiria kujiunga nao.



ABDUL KAMBAYA

MKURUGENZI WA HABARI

CUF-CHAMA CHA WANANCHI
 
Hahaha ile bodi ya wadhamini ya mahakama wao wanasemaje kuhusu kununuliwa madiwani au ni sehemu ya njia mpya za mapato za chama?!
 
Hawa wajinga wakati wanalindwa pale Buguruni kwa mtutu wa Bunduki walikuwa wanachekelea tu. Hivi unakubali vipi kukumbatiwa na chatu eti kwa kuwa tu unamfuga.

Hao wajinga wameuumiza sana UKAWA kwa faida ya matumbo yao.l
 
Back
Top Bottom