Sigma
JF-Expert Member
- Feb 26, 2011
- 5,006
- 1,254
Muhimbili yapunguza gharama za vipimo
Hili punguzo limeleta nafuu kubwa kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Muhimbili na MOI
Na Otilia Paulinus
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), imepunguza gharama za vipimo vya matibabu kwa wagonjwa wa rufaa.
Vipimo vilivyopunguzwa gharama hospitalini hapo ni vipimo vya aina mbili; ambavyo ni MRI na CT Scan ambavyo vinatumika kupima magonjwa ya ubongo sambamba na mishipa ya damu pamoja na tishu.
Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaesha, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, vipimo vilivyopunguzwa gharama ni kiitwacho MRI na CT Scan ambavyo vinatumika kupima magonjwa ya ubongo sambamba na mishipa ya damu pamoja na tishu.
Lengo la kupunguza gharama hizo, Aligaesha alisema ni kuwafanya wagonjwa waweze kumudu gharama za vipimo hivyo na kuanza matibabu mapema.
Awali kipimo cha MRI kilikuwa kinagharimu Sh 350, 000, lakini sasa kimeshuka hadi 100,000 na kile cha CT Scan kilikuwa kinagharimu Sh 170,000 na sasa kitakuwa kikigharimu Sh 50,000 kwa wagonjwa watakaokuwa wamepata rufaa ya kutibiwa hapa Muhimbili wakitokea Hospitali za Wilaya na Mkoa.
Kimsingi punguzo hili limeanza tangu mwezi uliopita na hili limekuja baada ya Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutaka kuifanya Muhimbili kuwa Hospitali Maalum ya kutoa vipimo vikubwa ambavyo hapo awali havikuwapo.
. .
Hili punguzo limeleta nafuu kubwa kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Muhimbili na MOI