Cryptoqueen: Mwanamke aliyeutapeli ulimwengu kisha kupotea

Cryptoqueen: Mwanamke aliyeutapeli ulimwengu kisha kupotea

Johnny Sins

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
2,536
Reaction score
3,885
RUJA Ignatova alijiita Malkia wa sarafu ya kidigitali al maarufu Crptocurrency, aliwaeleza watu kuwa amebuni sarafu ambayo itatoa ushindani kwa Bitcoin na kuwashawishi kuwekeza mabilioni ya fedha, kisha miaka miwili iliyopita akatoweka.

Jamie Barlett, alitumia miezi kadhaa kuchunguza ni jinsi gani alivyoweza kuwashawishi watu kupitia matangazo ya kibiashara ya kuwekeza katika sarafu za kidigitali na kujaribu kung’amua ni wapi anakojificha

Mapema mwezi Juni, mwaka 2016, mafanyabiashara huyo mwenye miaka 36, aliyejiita Dk. Ruja alisimama jukwaani katika ukumbi wa Wembley mbele ya maelfu ya mashabiki wake.
Kama ilivyokuwa kawaida yake, alikuwa amevalia gauni lenye bei ya tahamni la kuhudhuria hafla za jioni, hereni za ndefu za dhahabu na rangi nyekundu mdomoni.

Aliuleza umati huo kuwa sarafu yake ijulikanayo kama OneCoin, inapigiwa upatu kuwa sarafu kubwa zaidi duniani ya kidijitali ambayo alidia kila mtu ataweza kufanya malipo kokote kule.

Bitcoin ndiyo ilikuwa sarafu ya kwanza ya kidjitali na bado inaslaia kuwa inayotambulika zaidi.

Kupanda kwa thamani yake kutoka mapeni kidogo hadi mamia ya dola kwa kila sarafu, ilipofika katikati ya mwaka 2016, imesababisha msisimko mkubwa miongoni mwa wawekezaji.

Watu wengi walitafuta kujihusisha na fursa hii mpya na ya kipekee.

Dr. Ruja, aliuambia umati katika ukumbi wa Wembley kuwa OneCoin ndiyo itakayoiangamiza Bitcoin akisema katika kipindi cha miaka miwili ijayo, hakuna atakayekuwa akizungumzia tena Bitcoin.
Kote ulimwenguni, watu tayari waliwakuwa wanawekeza katika OneCoin, wakitumai kuwa sehemu ya mageuzi makubwa katika ulimwengu wa fedha za kidijitali.

Nyaraka zilizovujishwa kwa BBC zinaonesha Waingereza walitumia kima cha pauni milioni 30 kuwekeza katika OneCoin katika kipindi cha miezi sita ya kwanza za mwaka 2016, Pauni milioni mbili katika kipindi cha wiki moja pekee na kiwango cha uwekezaji kingeongezeka baada ya maonesho ya Wembley.

Kati ya Agosti 2014 na Machi 2017, zaidi ya Pauni bilioni 4 ziliwekezwa katika mataifa kadhaa. Kuanzia Pakistan, Brazil, Hong Kong, Norway, Canada, Yemen hadi Palestina.
109781586_shutterstock_976.jpeg
 
Kwenye hizi Mambo kuweka hela ni rahisi sana ila kutoa sahau. Niliweka 350,000/= saivi token nilizonazo zina thamani ya milioni 4. Wakatwambia BOA ndo watakua wanatoa hela. Kwamba Mwaka Jana hiyo coin ilitakiwa iende public nikakuta kimyaa. Hahaha sema ilinipa nafasi ya kusoma na kujua kuhusu crypto currency!! Ila ndo nshapigwa haha.
 
Nimeiangalia Documentary inayomuhusu RT wamechimbua sana, mademu wa hivi ndio nawataka sio mazuzu
 
Luna Series Inaitwa "The Startup" Imemzungumzia Huyu Bidada, Ni Nzuri Sana
 
Dooh sa mbona kamuachia mdogo wake msala au hakumpanga...!!
 
Natafuta watu 1000 kama wewe nimalizie ujenzi wa hoteli yangu.
Naamini soko la watu wa type yako bado kubwa sana
Kwenye hizi Mambo kuweka hela ni rahisi sana ila kutoa sahau. Niliweka 350,000/= saivi token nilizonazo zina thamani ya milioni 4. Wakatwambia BOA ndo watakua wanatoa hela. Kwamba Mwaka Jana hiyo coin ilitakiwa iende public nikakuta kimyaa. Hahaha sema ilinipa nafasi ya kusoma na kujua kuhusu crypto currency!! Ila ndo nshapigwa haha.
 
Back
Top Bottom