CRDB yawa ya 8 kwa kutoa huduma Tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CRDB yawa ya 8 kwa kutoa huduma Tanzania!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Jethro, Sep 2, 2010.

 1. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kweli inasikitisha sana kwa Bank kama CRDB kushika nafasi ya 8 kwa kutoa huduma bora kwa wateja wake.

  Matatizo nayo yajua yaweza kuifikisha hapo CRDB kama mie mteja wao ni

  1. Feature plan zao mbovu au haziwakidhi wateja waliopo na kuwavutia wateja wapya
  2. Branch Managers-kwa jinsi mie navyo oona managerz wachache sana wanakuwa makini kwa branch chao na wengi wao wapo pale kujilimbikizi mahela tuu kwanini nasema hivyo utakuata manager wa branch fulani anajifanya ati anabana matumizi kumbe anaba hivyo ili azisukumie kwake huku wafanyakazi wake hata kuwaboreshea vitendea kazi kama viti desks au stationaries za kufanyia kazi anajifanya ati muwe mwaijua cut coast. me na uhakika Kimei akituma jopo la wakaguzi kwa managers watakuja na mambo mengi na wasiwulize managers kupata uhakika wawaulize wafanyakazi wa hizo bank na wateja wanao hudumiwa na mbaya zaidi hakuna suggestion box ikiwepo ni boss ndie anasoma hapo kweli ukweli utamfikia kimei??
  3. Motisha - esp kwa wafanyakazi wa CRDB ni kuwa wanaupendeleo au ndio nini mishahara ni midogo sana na ukizingatia hali ya maisha imeisha anza kuwa ngumu uchumi uko juu sana haulingani na mishahara wanayo pokea,wanakumbwa na matatizo ya usafiri,kodi ya nyumba, sijui wana hisa wa CRDB wanalionaje hilo swala je wao wanafurahi hiloo???
  4. Uchache wa wafanyakazi ndio kabisaaaa sijui siku hizi ndio style ya kufanyisha watu kama kile kipindi cha slave na master? mwategemea mtu mmoja ahudumie customers wanao kuja front dest,Tailor, na sehemu hizo zote ni mtu mmoja au kwa tailor unakuta wako wa wili foleni ya watu zaidi ya 150 hiyo niu asubuhi tu waingiapo.
  5. ....
  6. .....
  7. ......
  8. ,.......
  Wadau changieni zingine zimfike kimei na member board ya CRDB inatuuma sana bank yetu inakuwa ya 8 kwa uzembe wa Board inashindwa jua hali halisi au kumekuwa na siasa nako au watu wamekuja kuchuma pesa CRDB??
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu Jethro kuna thread humu nafikiri mwaka jana iliyoichambua CRDB na Kimei wake kwa kina. Wengi wetu tuliliona hili linakuja kutokana na uozo wa management ya juu ya CRDB. Corporate vision na Mission naona ina matatizo hasa baada ya Denmark kuondoa ubia wake.

  Hili tulilisema sana, lakini wengine wakasema tuna mwazo ya kikoloni na hatujiamini.

  Sasa tunaona uzalendo wa Kimei unapotufikisha, bila kusahau kuwa suala la EPA na CRDB lilijikita tena sana.

  Institutions kama hizi hazendeshwi kisiasa ama sivyo CRDB na NBC ya zamani ni kama nyani wasiochekana kundule.
   
 3. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  "CRDB yawa ya 8 kwa kutoa huduma tanzania haibu hii" Hiki ndicho kichwa kinachobeba mada yako.

  Maswali.
  Source wapi?
  Nani wa kwanza mpaka wa saba?
  Mbona mada iliyoko chini ya hicho kichwa cha habari ni mshahara? Kama future plan na vision ndiyo matatizo, mshahara unahusika vipi?
  Ni tawi gani ambalo Maneger anafanya hayo?

  Majibu yakija nitachangia.

  Respect
   
 4. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Katika pita pita yangu apo Dar last week nilikuwa jengo la HO yao na mambosi kadhaa walikuwa wametoka kwa kikao na walikuwa wengine wakijadiri kuwa CRDB imekuwa ya 8 kwa kutoa huduma. baadae nikamwona mtu nika muuliza mule mule ndani akaniambia ni kweli. sikutaka kuendelea asije akashtukia kuwa na mchunguza saaaana.

  Sikumbuki vizuri ila nilifuatilia hilo nipata kujua kati ya Stanbic au standared Charter Bank ndio mojawapo ilikuwa yaongoza ntakujibu shortly let me go through my Database

  Hapo nilichangia mambo muhimu ambayo ndio chanzo cha CRDB kuporomoka na ndivyo kwa bank zingine na ndio bank nilio izoea sana kwa shughuri zangu

  Kwa matawi niliopita mengi sana eg Dodoma , Mwanza , Musoma, Morogoro, Moshi, Arusha, na nakumbuka pia mwaka jana kuna branch Moja ilitajwa Huko Arusha na mdao wa JF alikutana huduma mbaya mpaka akatoa maelezo ya huyo dada aliye muhudumia ilikuwa ni kati ya Meru au USA-River au Arusha Branck kati ya izo. huko kwingine twayaona mapungufu na kwa ushauri tu wange weka online complain zimfikia Kimei na Top Management yao yote ya CRDB

  Nadhani kwa majibu hayo waweza changia mkuuu na natkupa more updates ukitaka
   
 5. C

  CLAY KITUMBOY Senior Member

  #5
  Sep 3, 2010
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nawaomba sana uongozi wa CRDB Azikiwe wawambie wale askari wanaolinda ile Benki usiku mchanga wasizime taa pale kwenye ATM machines as early as saa 2 usku tu wameshazima taa panakuwa giza inakuwa ni taabu sana kuona una bonyeza nini.

  2.Vilevile ile ATM yao iliyokuwa Temeke Hospital haina umeme kwa takriban wiki moja sasa na sijaona wanachukua hatua yoyote ile

  Sasa hata watu wanapolalamika wana haki ya kufanya hivyo na ushahidi bayana kama huo

  HUO NI UKWELI HAKUNA FITINA HAPO
   
 6. Njaa

  Njaa JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2010
  Joined: Dec 6, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 60
  top seven ni zipi? Maana kwa nilivyokuwa naijua kijuujuu CRDB, sikudhani kama inaweza kupata washindani wengi namna hiyo kwa kutoa huduma bora
   
 7. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  huu sijui kama si udaku na kutaka kuharibiana kibiashara.


  no research no rights of saying
   
 8. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2010
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,624
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 180
  HII INAWEZEKANA,,,LAKINI BANK ZIPI AMBAZO ZIMESHIKA NAFASI YA 1 -7?? MANAKE CRDB INA UNAFUU KIDOOGO INGAWA SIKU HIZI WANAZIDI KUDORORA(eg SIKU HIZI HATA KAMA UPO KATIKA TAWI LAKO,KUSHINDWA KUTOA AU KUWEKA HELA SABABU YA DOWNTIME NI KAWAIDA KABISA,TENA HUWA INA LAST HATA 6 HOURS AU THE WHOLE DAY) ..BENKI NYINGINE ZILIZOBAKI KAMA EXIM NDIO DUH!!!!NI ZIPI HIZO TOP 7 ??
   
 9. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Tatizo lako unapenda kutafniwa kila habari nawe chekecha kichwa mbona wengine wakiweka hapa issue huwa twaitafuta kwa source zetu na twazijaziliza hapa,

  The fact is, i do have the details in PDF and i cant put it here is a risk, ntawapa majina tuu maana mmmmh najua kuna wengine humu wametumwa
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nina hamu ya kujua wa kwanza na nani amefanya iyo research
   
 11. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nakumbuka nimeomba huduma ya SIMBANKING ambayo wanaitangaza sana lakini mwezi wa pili unataka kukatika huduma haipatikani .....sijui tatizo ni nini?

  No feedback, no any communication.....Ukienda kuuliza unaambiwa tutashughulikia. ....Kwa mwendo huu siwezi kushangaa hata wakiwa wa mwisho.
   
 12. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mkuu kwanza nakupongeza kwa sababu umekubali kueleza ukweli wa source yako.

  Niliuliza maswali yote yale kwa sababu ya habari yenyewe ilivyokuwa. kwa kawaida taarifa nzito kama hizo zinatolewa na mashirika makubwa yaliyobobea kwenye tafiti. Taarifa kama hii humu jamvini inaweza kabisa kumshawishi mwingine akaenda kuuza hisa zake. uamuzi ambao unaweza kuwa wa manufaa au hasara kwake.

  Ni vyema basi tukatumia zaidi taarifa ambazo zinatoka kwenye chanzo cha kuaminika na siyo kutoka kwenye baraza za ofisi. Mimi ni mwanahisa kama wewe na hasa kwa CRDB namiliki kiwango cha kutosha kutokana na imani niliyonayo juu yake. taarifa kama hiyo inasumbua kidogo.

  Ila mkuu numekuelewa vizuri tu.

  Respect
   
 13. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mkuu wewe wataka kujua mtu alitefanya research tuuu au unataka kupata majibu au ni Bank gani ilikuwa ya kwanza hadi ya mwishoooo??? hata wewe mwenyewe waweza ifanya research pia ukijitolea ila
  wa kwanza kwa huduma bora na safi na wateja kuridhika kwa kuanzia ni:

  1. Standard Chartered Bank (Na wakapata Tuzo)
  2. .......
  3. ..........
  4. ................
  5. ...................
  Mwendeleee nanyi kufanya research sasa naona mwapenda ambiwa tu ila kuchekecha vichwa hamtakiii jamani au huwa hamuhudhurii kwa bank zetu humu nchini??

   
 14. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Nawashangaa wanaompinga Jethro infact ilikuwa ife hio bank last year imebebwa na fedha za stimulus package
   
 15. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Ewaaaaaah Super Star,

  Maana humu kwa janvi la JF watu hupenda sana kutafuniwa na wao wameze.

  kwa ujumla CRDB huongoza kwa vingine vyote ila tu wanapo shindwa ni Customer service & Care na hapo ndipo Kimei amemwaga pesa nyingi sana ili hiyo huduma ifanyike kwa ustaha zaidi cha ajabu ndio inakwenda vise versa kabisa na hili ni makosa makubwa kwa top management ya CRDB, i doubt hiyo pesa imetoka one way and not both way kwa nini nasema hivyo umetoa pesa kuboresha huduma lakini kwa wale wanaoifanya hiyo huduma iboresheke zaidi hujawawezesha vyema katika maeneo yao ya kazi,kimshahara,overtimes,usafiri nakadhalika

  Na ninashindwa elewa kama jana TBC1 walisema hisa zao zilipanda juu sana ila hawasemi kuwa customer care na service ni mbovu na hao wana hisa wao wana kaaa kimya watakuja shangaa tuuu bank chini na hakuna jibu.

  kwa mfano tuu mwakajana CDRB ilishika nafasi ya 4 kwa kutoa huduma bora siju ni nini kiliwasibu mpaka kupolomoka hadi nafasi ya 8.

  Kimei & Top Management yako (CRDB) watakua responsible na anything once CRDB ikiwa Disintergrate

   
 16. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #16
  Sep 10, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Binafsi mimi ni mteja wa kawaida wa CRDB, sina hakika sana na hiyo nafasi ya nane. Kwa kweli kwa banking industry ndani ya nchi yetu hii CRDB kuwa ya nane ni kama muujiza fulani hivi ingawa chini ya jua kila kitu kinawezekana.

  Uzoefu wangu wa kuwa mteja wa CRDB kwa takribani miaka kumi sasa ni tatizo la kufanya kazi kwa mazoea na ile hali ya kudhani kuwa na foleni ndefu ya wateja ndio kuonyesha kwamba ninyi kama bank mnapendwa sana na wateja na mna credit nzuri sokoni kumbe hali ni kinyume. Nikizungumizia Mbeya kwa mfano kuna teller cage tano sijawahi hata siku moja kukuta zote zina tellers matokeo yake ni kwamba wakati wa malipo ya wanafunzi wa vyuo vikuu dirisha moja hutengwa kwa ajili hiyo na kufanya idadi ya wateja kama mia mbili (200) kwa siku kuhudumiwa na muhudumu mmoja.

  Hii inakuwa ni kazi za shuruba bora kubeba zege, kwa sababu kazi inachosha na inahitaji umakini mkubwa unaweza kwa bahati mbaya na kuchoka ukajikuta umemzidishia mteja pesa. Na hili likitokea kwa risk ya cashier mwenyewe maana huwezi kumwambia meneja kwamba umepata short kwa sababu wateja walikuwa wengi definetely atakwambia ni uzembe wako!

  Mazingira ya kazi ya namna hii hayana hamasa hata kwa wafanyakazi na hii hufanya kuwaona wateja kama maadui vile, kazi haijajengwa katika mazingira ya kumfanya mfanyakazi aipende. Naamini wafanyakazi wa CRDB wanaipenda sana kazi yao na wanaifanya kazi kwa bidii lakini mazingira mabovu na menejimenti isiyojali ndio chanzo cha huduma mbovu ndani ya CRDB. Kwa hiyo kifupi sana staffing ya CRDB haitoshi hili liangaliwe kwa macho mawili, kubana matumizi kunakopelekea kuwafanyisha watu kazi kama punda kuna punguza ufanisi.

  Hapo niliposema kufanya kazi kwa mazoea nilikuwa namaanisha kwamba managers wanafanya kazi bila ubunifu na hali ya kuzingatia mahitaji ya wakati. Mfano hapa Mbeya CRDB ni moja kati ya Benki za mwanzo kabisa kufika baada ya NBC ya (Mwalimu) na THB wakati huo. Lakini cha kusikitisha CRDB ndiyo benki yenye ATM's chache na branch chache kwa hapa mbeya kuliko benki nyingine nyingi zilizokuja hata miaka mitatu tu iliyopita.

  Umefika wakati tuambiane ukweli tuache longo longo na tufanye kazi za watu kwa mujibu wa mamlaka na taaluma tulizonazo. Hebu fikiria pamoja na uchache wa ATM's lakini bado ATM's zinazoaminika angalau ni hizi zilizopo hapa main branch kwani za soweto na uyole zina weza zikakaa hata wiki hazitoi huduma hii husababisha watu wote wakasongamane kwenye tawi kuu la mjini. Wenyewe tunasema kuna meneja, meneja gani anafanya kazi kwa kiwango kisichojali maslahi ya wateja?

  Ukienda CRDB kama kumekucha vizuri angalau ndio utatumia saa moja kama una fanya Phisical transaction vinginevyo biashara imekukata. Visa card ime expire watakwambia kwamba baada ya mwezi mmoja itakuwa tayari ukweli ni kwamba ikiwahi ni miezi mitatu. Dunia ya leo yenye kila aina ya teknojia, miezi mitatu nini hasa kinafanyika?

  Yakusema yapo mengi leo haya yanatosha mwenye masikio na asikie bank yetu inaboa sio siri. Kinachotugharimu wengine hatuna tabia ya kuhamahama na haka ka uzalendo ka kurithi nayo ni sehemu ya tatizo lakini kwa huduma hizi tunaumia sana.

  CRBB badilikeni, wakati mnaendelea na usingizi weakness zenu ndio inayojenga strength kwa bank za kigeni.

  SHAURI YENU KAMA MMECHAGUA KUFA MTAKUFA KWA KUWA MNA AKILI TIMAMU NA KWA MIKONO YENU MMEAMUA KUNYWA SUMU, KWA HILI SINTO KUFA NANYI HONGERENI KWA UZEMBE WA MAKUSUDI.
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Sep 10, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Benki bora kwa sasa ni efatha bank
   
 18. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #18
  Sep 10, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mkuu kwa kuongezea
  Kuna baadhi ya wafanyakazi wa CRDB wana nyodo sana. Mfano UDSM Branch. Unamuuliza mfanyakazi akupe maelezo ya aina fulani ya akaunti na inafanyaje kazi anakurushia karatasi kama vile wewe umekwenda kuomba hela. Watu wanasahau kusoma na kuelekezwa hasa kwenye mambo ya hela ni vitu tofauti. Kwenye desk la maulizo huwa hakuna utaratibu wowote wa kusikilizwa. Mfano mtu anakuja anakukuta umekaa zaidi ya nusu saa unasubiri kuhudumiwa, anapitisha makaratasi juu ya kichwa chako, baada ya muda unaona pesa zinapitishwa tena juu ya kichwa chako anaondoka
   
 19. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #19
  Sep 10, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu yote haya yanatokana na uozo unaokaribishwa na viongozi kwa kuwa sio kweli kwamba vilio vyote hivi hawavisikii.

  Kama nilivyosema kwenye thread iliyotangulia kuwalimbilikizia wafanyakazi kazi nyingi kuliko uwezo wa kawaida wa kibinadamu matokeo yake ni kuichukia kazi husika.

  Kinachofuata baada ya hali hiyo ni "kazi duka" yaani ile hali ya kufanya kazi ya mwajiri lakini endapo tu ina maslahi binafsi kama vile kutegea kazi na kufanya kazi hasa zile zinazowahusu wateja mnaofahamiana ki binafsi (aka kukuza jina) ndiyo iliyoifikisha CRDB hapo ilipo na hakuna anayejali. Waswahili wanasema "acha litote tugawane mbao"
   
 20. M

  MC JF-Expert Member

  #20
  Sep 18, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mkuu umenikumbusha hivi karibuni nimekwenda kuchukua pesa pale UDSM, nilishangaa sana baada ya kukaa kwenye foleni kwa Takribani saa moja kuambiwa kuwa Acount yangu haiko 'Active'. Nilimwangalia yule mdada nikamwabia jana tu nimechukua USD mlimani city, pia nachukua pesa bank zaidi ya mara tatu kwa wiki kwa kipindi ninachokuwa Tanzania, yeye ananiambia haiko active, ikabidi nimuulize 'hivi CRDB ina matatizo gani? mbaya zaidi kama jana yake nilipokwenda CRDB Mlimani City nikihitaji dola 2,000 niliambiwa dola zimeisha!!!, ikabidi niambulie dola 900.

  Wao wanasahau kuwa wanafanya Biashara badala yake wanaona Mteja ni kama unafaidi saaana na wanakusaidia saana, CRDB amkeni,
   
Loading...