HUGO CHAVES
JF-Expert Member
- Mar 25, 2011
- 2,045
- 547
lakini zile form za kuwekea fedha nazo nadhani zitakuwa na tatizo kwana nadhani hakuna sehemu wameonyesha 10,20,50,100...!!sasa mteja atajaza vipi akiwa na sarafu!!!
Ndugu zangu, katika hali isiyo ya kawaida, leo nimeshuhudia tukio la kusikitisha. Nilikuwa katika Benki ya CRDB, Tawi la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam; nimeshuhudia mhudumu wa dirisha namba 2 akikataa kupokea fedha za mteja mmoja kijana. Kisa ni kwamnba kijana huyo alikuwa na fedha nyingi za Sh 50, 100 na 200 ambazo kwa kawaida ni sarafu. Mhudumu amekataa kuzipokea kwa maelezo kwamba hawapokei "masimbi". Akamtaka kijana huyo azipeleke kwa makondakta wa daladala, azibadili ili wampe noti, au masimbi hayo ayapeleke BoT. Kukawa na vuta nikuvute, mwisho yule kijana akaondoka bila kuweza fedha kwenye akaunti.
Hoja: Hii ni sahihi kwa benki kukataa kupokea sarafu? Je, sarafu hazitambuliwi kama fedha halali hapa nchini? Naomba wadau tulijadili suala hili.
Nawasilisha.
nitaenda kucheki!!ninadhani zinaanzia 500 na kuendelea!!ipo kila form za benki maana ni sheria hupewi leseni bila hiyo.
Haya ndio matokeo ya output za kutoka UDOM. Tutashuhudia mengi.
nitaenda kucheki!!ninadhani zinaanzia 500 na kuendelea!!
Watanzania ushirikiano ni zero kabisa wewe umeshindwa nini kumshauri pamoja na wenzio angalau amuone hata meneja muhusika kuliko kumuacha akaondoka bila kupata huduma?
ok!!!kwa hiyo huyu jamaa akalalamike wapi!!nakumbuka issue kama hii iliwahi kutokea siku za nyuma na ilibidi mhusika azipeleke zile 'simbi' benki kuu!hapana ipo sehemu ya coin....sema tu haisemi 50,100,200 etc
bali unatakiwa uandike una coin za sh ngapi?