CRDB: Sikio la kufa!?

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,728
2,259
Kuna tetesi miongoni mwa Bankers kuwa CRDB itakabiliwa na wakati mgumu sana wakati wowote sasa.

Hii ni baada ya washirika wake wa DANIDA na wale kutoka Canada kujitoa kutokana na kutokubaliana na uongozi wa Benki hiyo juu ya ushiriki wake katika sakata la EPA.

Washirika hao toka nje walijaribu bila mafanikio kumtosa Dr Kimei na hatimae wametaka na kufanikiwa kurudishiwa hisa zao.

Inaelekea CRDB inaenda ile barabara ya kifoni iliyoikumba NBC ya zamani.

Wana JF mpo hapo?
 
Kwanza ndio unatushtua, Sisi wateja wa CRDB sasa akili kichwani yasije yakawa ya MERIDIAN BIAO BANK
 
Hao DANIDA wana shares ambazo zinaweza kuchukuliwa na wengine wakati wowote zikipelekwa sokoni, sifikiri kwamba hili ni tishio kwa benki yenye kuongoza kwa deposit. Hii hadithi ya DANIDA kuondoka haijaanza leo, nadhani tangu 1998 wamekuwa wakisema jambo hili, lakini wapi-wapo tu na watu wao wanapata kazi hapo benki.
 
DANIDA waondoke bana na wenye fweza za EPA wanunue shares hivyo ndivyo tunavyoweza kurudisha nchini hayo mabilioni waliyoficha nchi za nje.
 
duh, yamekuwa hayo tena. EPA si ina baraka za serikali, waicharukie serikali sio management ya benki ambao ni waajiriwa
 
CRDB can float the same shares through IPO if these investors go! let them go. there was a massive over subscription during the last offer. it is nt a big deal.
 
Mimi ni mteja wa CRDB na sasa kuna makato wameanzisha wanaita Card fee kila mwezi wanakata elfu 3 kwa kweli it is a lot kwa sisi walala hoi. nadhani kuna kituwanafidia kwani kwa wateja waliopo how much they earn
 
Inasikitisha kwamba forum hii ya great thinkers tunazungumzia jambo la uzushi kwa benki ambayo ndio imebeba uchumi wa Tanzania.

Je tunayo elimu ya kutosha kuhusu masoko ya hisa na utendaji wake au tunakurupuka tu? Kwa nini tusiombe wataalamu wakatusaidia?

Hii ni forum nzuri ya kuzungumzia maendeleo ya uchumi wa nchi yetu lakini sio uzushi tujikosoe wenyewe tubadilike.

Mungu Ibariki Tanzania! Mungu ibariki benki yetu ya CRDB
 
Mkuu unachosema ni sawa, lakini usipuuze tetesi kama hizi. Mara nyingi insiders ndio wanapata info kabla hata hazijawafikia hao DSE!!

Nafikiri unakumbuka kuanguka kwa Lehman brothers, Enron and WorldCom!! Haya mambo huwa yanatokea, by the time Regulators wanastuka its too late!!
 
Ndahani, je umeziona published financials accounts za mpaka september za sikio la kufa(CRDB Bank)? wanatisha kweli kweli. Wanaongoza kwa kila kitu. jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Tusiwe makuwadi tu-argue kwa facts sio kwa majungu na uzushi.
 
Well said Mkuu!! Maana unaweza kutishwa ukakimbilia kuuza hisa zako bure!! By the way zile hisa tulizonunua zinaendaje maana tupo nje huku hatuna taarifa...!!
 
Serikali haiwezi kuiachia CRDB ikaanguka kifo cha mende kwasababu serikali yenyewe imepitisha fedha yake nyingi ya STIMULUS package humo humo CRDB!
 
I f the government will allow CRDB to collapse then ,the whole of the Tanzanian economy will be in a mess because a substantial amount of the stimulus funds have passed through the this bank!
 
Ndahani, je umeziona published financials accounts za mpaka september za sikio la kufa(CRDB Bank)? wanatisha kweli kweli. Wanaongoza kwa kila kitu. jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Tusiwe makuwadi tu-argue kwa facts sio kwa majungu na uzushi.

Asia ktk zama hizi za creative accounting I'm not surprised to see those figures published! Naamini unajua maana ya kutrade shares kwenye masoko ya hisa, numbers matters alot no matter if they are real or not!!

Kuhusu share za CRDB kuwa oversubscribed during its IPO, si kigezo cha kuuzika kwa share zao tena given the market trend. Niamini mimi, Kama hao jamaa wakichomoa, lazima share za CRDB zitashuka!! Siiombei mabaya CRDB, I'm one of the shareholders there, yet I have to remain cautious!!

The challenge ahead of us is to build a strong CMSA & DSE!!

Tusubiri tuone
 
Mkuu unachosema ni sawa, lakini usipuuze tetesi kama hizi. Mara nyingi insiders ndio wanapata info kabla hata hazijawafikia hao DSE!!

Nafikiri unakumbuka kuanguka kwa Lehman brothers, Enron and WorldCom!! Haya mambo huwa yanatokea, by the time Regulators wanastuka its too late!!

hapa hakuna fact yoyote zaidi ya speculations,huwezi kusema kwamba a leading bank in the country itaanguka na kufa just bcoz DANIDA wanauza shares zao!Kwani shares zikiwa owned na locals huo sio mtaji?when will we wake UP from this Neo-colonialist syndrome?mbona wengine wanaweza?
Au mwekezaji ni lazima atoke ulaya?kwa taarifa yako hata hao DANIDA walikuwa na hisa 20% tu!80% locals.
YES WE CAN
 
CRDB can float the same shares through IPO if these investors go! let them go. there was a massive over subscription during the last offer. it is nt a big deal.
Unazungumzia kufloat, unajua balance ya demand na supply ikoje? Wakifloat zitauzwaje? Bei itakuwaje? Issue si kufloat tu
 
Asia ktk zama hizi za creative accounting I'm not surprised to see those figures published! Naamini unajua maana ya kutrade shares kwenye masoko ya hisa, numbers matters alot no matter if they are real or not!!

Kuhusu share za CRDB kuwa oversubscribed during its IPO, si kigezo cha kuuzika kwa share zao tena given the market trend. Niamini mimi, Kama hao jamaa wakichomoa, lazima share za CRDB zitashuka!! Siiombei mabaya CRDB, I'm one of the shareholders there, yet I have to remain cautious!!

The challenge ahead of us is to build a strong CMSA & DSE!!

Tusubiri tuone
Well said! Hakuna chembe ya siasa ila umeongea kitaalam maana watu wanachanganya na siasa.
 
Mimi ni mteja wa CRDB na sasa kuna makato wameanzisha wanaita Card fee kila mwezi wanakata elfu 3 kwa kweli it is a lot kwa sisi walala hoi. nadhani kuna kituwanafidia kwani kwa wateja waliopo how much they earn

Isae!
Una uhakika kwamba unakatwa elfu tatu kila mwezi?
mimi pia ni mteja mwenye akaunti yangu na ya mtoto,nijuavyo mimi benki ilitukata elfu 3,000 mwezi wa nane kama malipo ya card ya visa!
sidhani kama wateja wote wa CRDB nchi nzima wangekaa kimya kwa kukatwa elfu tatu kila mwezi!kuwa mkweli ndugu yangu
 
Brooklyn,
That is a very serious accussation! Do you have facts that the Bank is cooking its financials? How about other Banks? Hapa mimi naona kwamba huu ni uonezi wa hali ya juu kwa benki ya CRDB ambayo imeuinua uchumi wa nchi hii na watanzania kwa ujumla. Hao wanaouwatuma kuwa makuadi wawe wanawapata na facts. Tuwe professionals tusiwe wazushi, wajinga . Watanzania tumeelimika tuna-analyse mambo sio kusikiliza majungu. kama mtu huna kazi au una personal grudge na mtu au unakuwadi kwa ajili ya benki fulani ukumbuke kwamba benki ya CRDB ni ya watanzania. Unachofanya unawakuza wazungu. Mimi nilinunua share toka benki ilipoanzishwa tena 1996 toka mwaka unafuatia mpaka leo napata dividend yangu kila mwaka na imekuwa ikiongezeka. je wangekuwa wapika mahesabu dividend ingetoka wapi? tena nono? Naomba utupe facts na sio hearsay.
 
Back
Top Bottom