CRDB Plc imetangaza gawio 2026 kwa wanahisa

CRDB Plc imetangaza gawio 2026 kwa wanahisa

Habari, HIMARS
Ninakujibu hapa na kisha nitafungua thread ili kukujibu na nitakutag kuwapa ushauri wale wote ambao wana imani kama yako.
Kwanza uko sahihi kuwekeza 29M ili upate 900k ni wehu, tena ni ujinga.
Lakini si sahihi kwamba Wawekezaji wanapata 900k, si kweli. Ingekuwa kweli watu wangechukia Hisa, unadhani una akili kuliko maelfu ya wachumi duniani na watafiti wanaosupport uwekezaji katika hisa?

Kukujibu kiufupi, mtu aliyenunua hisa za crdb mwaka uliopita 2025, alinunua hisa moja kwa Tsh 790, leo 2026, April hisa za crdb zina 2940...kwa hiyo ana capital gain ya 2150 kwa kila hisa moja.
Kwahiyo mtu aliyetumia 27M 2025 angenunua 34, 177 shares. Ambazo kwa sasa zinampa thamani ya 73, 480, 550/= (milion sabini na tatu na ushee)
Hii ni 270% capital gain

Kwahiyo kama ungenunua hisa mwaka jana kwa 27, 000, 000, leo portfolio yako ingekuwa inasoma ~100, 480, 550, capital yako ni 73, 480, 550. (270%)
Kisha chukua hiyo pesa jumlisha na gawio ambalo si laki tisa kama ulivyopotosha hapo juu bali ni 3, 000, 000 hivi na ushee.
Hivyo jumla ya faida uliyoipata ni 103, 000, 000 - 27, 000, 000 = 76, 000, 000.

Ni muda wa kuweka hisia pembeni na kuweka data na research mbele. Ingekuwa uwekezaji huu ni wehu zaid ya 55% population ya watu wa America wasingewekeza kwenye hisa.

Pray you have a good day, ni wakati wako kuanza kuwekeza sasa!
RMK,
INDEPENDENT STOCK ANALYST.
 
Back
Top Bottom