Leo nilikuwa naperuzi account yangu ya CRDB through internet banking na nikashtuka kidogo na fees zao. Nimekutana na kitu kama ifuatavyo:
Monthly maintenance fee ........Tshs. 1,000
Card fee June ........................Tshs. 4,000 (hii transaction ya tarehe 9 July)
Card fee June ........................Tshs. 4,000 (hii transaction ya tarehe 13 July)
Withholding Tax .....................Tshs. 63.39
Nilikuwa sijanotice hivi vitax kwa muda na nashangaa kama huu ni utaratibu mpya. Kama wanamfanyia kila mteja namna hii, basi wanatengeneza faida ya hatari sana
Hata mie nilikuta makato ya 4000 mara mbili eti ni card fee...Nilitaka kuwafuata kuuliza kuhusu hili suala. Ila kama ni gharama za visa card, kulikuwa na sababu gani ya msingi ya kukata mara mbili??
OK. Kama uko wilayani sawa ila kama uko Tanga mjini kuna Exim Bank ni wazuri kwa akaunti za watoto pia.
Hata mie nilikuta makato ya 4000 mara mbili eti ni card fee...Nilitaka kuwafuata kuuliza kuhusu hili suala. Ila kama ni gharama za visa card, kulikuwa na sababu gani ya msingi ya kukata mara mbili??
...Mimi Hii ya June Card Fee wamenikata mara tatu yaani 4,000/= x 3 = 12,000/= ! Jamani hapa sasa ninadhani tunapaswa ku-MULIKA MWIIZI!!
Naomba kujua ni bank gani haina makato kiasi hichi, nijitoe fasta wiki ijayo.
Mimi nilitaka kwenda kumfungulia mwanangu JUNIOR ACCOUNT CRDB, mbona mmeanza kunitisha jamani? Nimfungulie bank gani tena?
Mkuu usijisumbue tu kuwapigia, hakuna kilichokosewa hapo!
Hiyo buku kama alivyosema mdau hapo juu ni fee ya internet banking, mi nilishawahi kuwauliza wakaniambia hivyo. Halafu hizo buku nne nne ni gharam ya card yao (8000 kwa mwaka), sema tu wamekata in two instalments. Hiyo 63.39 ni kodi ya TRA
...Mimi Hii ya June Card Fee wamenikata mara tatu yaani 4,000/= x 3 = 12,000/= ! Jamani hapa sasa ninadhani tunapaswa ku-MULIKA MWIIZI!!
Yaani TRA wanaingia mpaka huku tena?
Hee, karib sana babu. Mi niko Korogwe, waenda Tanga mjini? Hakikisha unaenda na bibi please.
mnunulie hisa ama umnulie fixed asset inayo appriciate value kuliko benki za hapa kwetu Tz wamezidi wizi!
Inamaana hiyo buku unakatwa hata kama hautumii huduma ya internate
...Ongeza na hizi:
-Maintenance fee 700/= ( nina hakika hii wameishapandisha!)
- Withdrawal fee 500/= ( pia nadhani imeishapanda!)
- Visa ATM Charges 2000/-QUOTE]
Withdrawal fee nadhani ni Tshs. 1,000/= (not so sure) maana sijawithdrawal physically muda mrefu sasa. Yaani gharama za hawa watu zimeanza kuwa juu na kama alivyosema mdau mmoja, inawezekana kuna ujanja flani umeingizwa.
Mimi nakuja next week old korogwe halafu nitakuwa na manundu
Tanga waijua weye babu Dark City?
Hawaogopagi hata wababu